Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Wagonjwa wa saratani hupitia changamoto kubwa ya ulaji inayotokana na maudhi ya dawa wanazotumia au tiba wanayopatiwa.
Matibabu yao huzongwa na vipindi virefu vya kubadilika kwa hamu ya kula na uzito wa mwili. Baadhi ya tiba huwafanya wapoteze hamu ya kula hivyo kusababisha kupungua kwa uzito wa mwili huku zingine zikiwafanya waongezeke sana uzito.
Mabadiliko kidogo ya uzito wakati wa matibabu siyo mabaya. Hata hivyo, ulaji wa lishe bora pamoja na utumiaji wa maji mengi hushauriwa sana wakati huu.
Kwa kuwa kipindi hiki hutawaliwa na changamoto kubwa zinazohusisha mfumo wa chakula hasa kupoteza hamu ya kula, kuharisha pamoja na kutapika, mgonjwa anashauriwa kufanya mambo yafuatayo-
Miongoni mwa faida za kufuata utaratibu huu unaohusisha lishe na mazoezi ni kupungua kwa maudhi yatokanayo na tiba pamoja na uwezekano wa kuugua sonona, kutunza uzito sahihi wa mwili, kuimarisha kinga ya mwili pamoja na kupunguza uwezekano wa kuugua magonjwa mengine sugu wakati wa matibabu.
Chanzo: Cancer.Net / Cancer Treatment Centers of America

- Ikiwa hawezi kunywa maji ya kutosha, vyakula vyenye mjumuiko wa maji mengi vinapaswa kutumika. Mfano ni tikiti maji, supu, chai au maziwa.
- Pata lishe bora iliyokamilika. Zingatia uwepo wa makundi yote ya chakula, pia zingatia unywaji wa maji ya kutosha
- Punguza ulaji wa vyakula vilivyoandaliwa viwandani pamoja na vyakula vya haraka (fast foods)
- Viungo vya ziada viongezwe wakati wa uandaaji wa chakula ili kuongeza ladha. Baadhi ya viungo vinavyoweza kuongeza ladha ni vitunguu saumu, mdalasini na ndimu (limao)
- Badala ya kula milo mikubwa mitatu, mgonjwa anashauriwa kula milo midogo 6 kwa siku ili apate nishati ya kutosha pamoja na kupunguza adha ya kutapika na kiungulia.
- Ikiwa midomo imetengeneza vidonda, mgonjwa anashauriwa kupunguza matumizi ya vyakula vyenye asili ya uchachu.
- Fanya mazoezi. Huongeza utimamu wa mwili pamoja na kuongeza hamu ya kula.