Utaratibu wa maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu kila Alhamisi ulifia wapi?

Utaratibu wa maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu kila Alhamisi ulifia wapi?

inchaji

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2019
Posts
2,671
Reaction score
5,476
Serikali hii inapenda sana kufanya mambo yake uvunguni. Rais kanyamaza, Waziri Mkuu kanyamaza kana kwamba kila kitu kipo sawa. Wameachiwa wapayukaji kina Makonda kila siku kuongea pumba huku watu tunaotegemea wanaweza kuongea mambo ya maana wakiwa wamekimbia korona.

Nauliza hivi, ule utaratibu wa maswali ya papo kwa hapo ulioanzishwa na Mzee Lowassa, ambao kwa muono wangu ulikuwa mzuri sana kwa kuwa ulikuwa unatoa updates za kitu gani kinaendelea katika nchi angalau kwa siku 7 zilizopita umeishia wapi?

Yaani hii nchi ingekuwa na raia kama Guinea saivi tungekuwa na uongozi mwingine maana hawa watawala wetu wametuzoea mno.
 
Hata hivyo Kasimu sio mahiri kujibu maswali ya papo kwa papo kama alivyojuwa Mzee Mizengo, alikuwa anayapatia sana! Awamu hii ina spika kilazer sidhani kama anaona umuhimu wa hii kitu! Yeye ana waza kupambana na Chadema mle mjengoni!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Bunge, Spika alitangaza baadhi ya mabadiliko kutokana na Janga la Corona, katika mabadiliko hayo alisema hakutakuwa na maswali kwa Waziri Mkuu kila Alhamisi.
 
Back
Top Bottom