Utaratibu wa trafiki kunakili kosa pamoja na taarifa za dereva una lengo gani?

Planett

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2014
Posts
10,497
Reaction score
16,180
Wakuu hbari,

Juzi kati nilikua na safari ya kwenda mikoa ya kusini sasa kila askari akinisimamisha kama nikiwa na kosa naandikiwa risiti na kuna huu utaratibu nimeuona mpya WA KUNAKIRI KOSA PEMBENI KWENYE NOTEBOOK PAMOJA NA TAARIFA ZA DEREVA.

Sijajua huu utaratibu mpya umewekwa kwa malengo gani ila nina wasiwasi askari wasio waadilifu akiona siku hajakamata mtu anaweza tumia hizo taarifa kubambikia mtu kosa.

Naomba kufanamishwa kwa anaejua ni nini lengo la huu utaratibu wa kurekodi kosa pamoja na taarifa za mkosaji pembeni.

Nawasilisha.
 
mkuu nadhani mkosaji ni dereva na taarifa za dereva ziko kwenye leseni.
Shida iko wapi maana akishachukua namba ya leseni anakuwa na kila kitu konachomuhusu mkosaji au kuna kitu sijaelewa mkuu.
 
Utanyanganywa leseni ukiwa na makosa mengi nadhani!
Bado hatujafikia maendeleo hayo, nani atachangia ujenzi wa barabara kama wengi watanyangwanywa leseni? Wahanga wakubwa ni wale wenye shughuli za moja kwa moja na vyombo vya usafiri, ambapo matajiri hawajali kuhusu ubora wa gari, muhimu hesabu ya siku. Si utakimbiza wote hao kwenye ajira zao!
 
Ndio hapo buku mbili huwa inahusika,sasa jifanye unaijua haki sana.kama hujakabidhi leseni na kwenda kulala na mkeo maskani.
 
mkuu nadhani mkosaji ni dereva na taarifa za dereva ziko kwenye leseni.
Shida iko wapi maana akishachukua namba ya leseni anakuwa na kila kitu konachomuhusu mkosaji au kuna kitu sijaelewa mkuu.
yaani wanachofanya ukikamatwa anakupa ile risiti ya fain ukalipe then anakua na notebook anaandika jina lako, namba ya leseni, namba yako ya simu na kosa ulilofanya, ndio nauliza why wanakua wanafanya hivyo!?
 
Hii kitu imenikuta week iliyopita sikuelwa lengo la yule askari barabarani..kaandika mpaka namba ya simu, mimi pia sikuelewa ila kwa kuwa nilkuwa na haraka zangu nikaona acha niondoke asinipotezee muda
 
yaani wanachofanya ukikamatwa anakupa ile risiti ya fain ukalipe then anakua na notebook anaandika jina lako, namba ya leseni, namba yako ya simu na kosa ulilofanya, ndio nauliza why wanakua wanafanya hivyo!?
Huu ni utaratibu ni wakimfumo ni kwaajili ya kuendelea kufwatilia mwenendo wa Dereva kwaajili ya kukukata point kwenye liseni yako waliutambulisha huu mwongozo kipindi kamanda Muslim anaaza kazi ya ukuu wa Trafiki, shida wanaufanya kienyeji vile vimashine vya kurekodia wanajua wenyewe waliko vitupa sasa wanarekodi kwenye vi note book, shida ni kwamba hii Elimu ya kukatwa point waliifanya kama yakuwa bania mno madereva wa mabasi ya mikoani.
 
yaani wanachofanya ukikamatwa anakupa ile risiti ya fain ukalipe then anakua na notebook anaandika jina lako, namba ya leseni, namba yako ya simu na kosa ulilofanya, ndio nauliza why wanakua wanafanya hivyo!?
Kataa maana taarifa zote ziko kwenye lesseni.
 
Wakuu hbari,

Juzi kati nilikua na safari ya kwenda mikoa ya kusini sasa kila askari akinisimamisha kama nikiwa na kosa naandikiwa risiti na kuna huu utaratibu nimeuona mpya WA KUNAKIRI KOSA PEMBENI KWENYE NOTEBOOK PAMOJA NA TAARIFA ZA DEREVA.

Sijajua huu utaratibu mpya umewekwa kwa malengo gani ila nina wasiwasi askari wasio waadilifu akiona siku hajakamata mtu anaweza tumia hizo taarifa kubambikia mtu kosa.

Naomba kufanamishwa kwa anaejua ni nini lengo la huu utaratibu wa kurekodi kosa pamoja na taarifa za mkosaji pembeni.

Nawasilisha.
Kuna bonus wanapata kwenye kila kosa linalopita muda wa kulipa
Ndo mana askari akikusimamisha na akukute unakosa lime bet lazima ulipe na atachukua kumbukumbu namba ili a claim bonus
 
Utanyanganywa leseni ukiwa na makosa mengi nadhani!
Wakitaka kuchukua points kwa leseni yako hawaihitaji kukuomba , system inayotumika kuandika fines ina records zote za kila leseni na kila gari .
Huu utaratibu wa kuandika leseni namba na details zako kwenye notebook ni utaratibu wa nje ya system , kwa ajili ya manufaa yao ya kulipana bonus kwa kila fine iliyobet inapolipwa .
 
Hawa jamaa wakinikamata na najua nimefanya kosa huwa sipotezi muda kujieleza sana. Ninavyompa leseni naambatanisha ya kiwi basi mchezo umeishia hapo. Kwanini nilipe 30k wakati naweza kumpa 5k maisha yakaendelea.
 
Back
Top Bottom