KERO Utaratibu wa wanafunzi kwenda shule hadi Jumapili udhibitiwe

KERO Utaratibu wa wanafunzi kwenda shule hadi Jumapili udhibitiwe

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Sema bongo jau sana,
Yan mtu anajitoa kwa ajiili ya watoto wake, ila bado wazazi wake wanapiga kelele
Wikendi mtoto wangu haendi shule. Likizo hakuna kufanya assignment wala homework. Ni muda wa kupumzika na kujifunza mengine ya maisha. Form four kapata div II ya point 18 ikamtosha sana kuendelea na masomo
 
Tabia hizi hasa walimu wa mijini,angalau vijijini walimu wanalima,wanafuga na wengine wamenunua bodadboda wanapiga kazi siku za weekend..Walimu wa mijini wana tamaa
Mjini kuna mwalimu anaenda shule weekend?
 
Sema bongo jau sana,
Yan mtu anajitoa kwa ajiili ya watoto wake, ila bado wazazi wake wanapiga kelele
Anajitoa bure?. Tena wengine wanafundisha mada kabisa kisha hazirudiwi kwenye vipindi vya kawaida inakula kwa watoto wasio na uwezo. Hii haikubaliki.
 
Watoto mnawalazimisha kwenda mpaka Jumapili wasipokuja mnawachapa.

Jumamosi na Jumapili watoto wanaenda ibadani nyinyi mnawaza kufundisha tuu sijui akili zenu zikoje. Tafuteni kazi nyingine nje ya ualimu mnatia aibu mpaka nafasi za kuandikisha daftari la kudumu la wapiga kura mpoo.

Mnafosi watoto waje na buku Kila weekend wasipokuja nayo mnawapiga Sasa mtoto amepata wapi pesa, mmeshindwa kudai maslahi yenu hasira mnapeleka kwa watoto.

Kuweni na adabu
Kama umekurupushwa vile kwenye handaki la nguruwe pori. Si dhani kama kuna watoto wanalazimishwa kusoma hadi hizo siku na kama ipo basi kuna shida kubwa hapo unaposema.Kwahiyo kwenye hiyo shule kuna mtoto wako anasoma hapo? Au umeletewa kero na wazazi? Au kulikuwa unapita jumapili karibu na shule ukaona hayo yanayoendelea?
 
Back
Top Bottom