GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Kati ya vitu vilivyonisumbua, hasa miaka ya nyuma nilipokuwa nikienda ugenini vijijini, ni suala la kuswaki kwa kutumia maji yaliyowekwa kwenye beseni/ndoo ya kuogea. Tokea nikiwa mdogo, nilishajizoesha kuwa maji ya kwenye ndoo ya kuogea "hayafai" kuswakia.
Lakini kama wasemavyo, "msafiri kadiri", katika tembea zangu vijijini, nilikutana na mazingira ambapo unapotengewa maji ya kuogea Asubuhi, unatarajiwa utumie yayo hayo kuswakia.
Hauelekezwi kufanya hivyo, lakini unapoona wenyeji wako wakifanya hivyo, kwamba, labda, baba mwenye nyumba alipoingia bafuni kuoga alienda na mswaki wake akamaliza kila kitu huko, wewe unapaswa kufanya nini?
Kwa kuwa nilishajijengea imani kuwa hayo maji hayafai, nilikuwa naenda kuoga, nikishatoka bafuni, najifanya nilikuwa nimesahau kwenda na mswaki wangu. Nilikuwa siwaambii ukweli kuwa siyaamini maji yaliyopo kwenye ndoo ya kuogea kuwa yanafaa kusafishia kinywa. Kwa hiyo nikitoka tu bafuni, ama nilikuwa navuta muda kidogo au papo hapo huomba maji masafi kwenye jagi kwa ajili ya kwenda kuswakia.
Ni miaka mingi sasa imeshapita bila kukutana na hayo mazingira! Lakini unafikiri huo mtazamo wangu ulikuwa sahihi?
Au, kwa usahihi zaidi, nipo sahihi? Kwa sababu hata sasa bado imani yangu ni iyo hiyo!
Ni usafi au mtazamo tu?