Utaratibu wangu wa namna ya kupiga mswaki ni usafi au mtazamo tu?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Kati ya vitu vilivyonisumbua, hasa miaka ya nyuma nilipokuwa nikienda ugenini vijijini, ni suala la kuswaki kwa kutumia maji yaliyowekwa kwenye beseni/ndoo ya kuogea. Tokea nikiwa mdogo, nilishajizoesha kuwa maji ya kwenye ndoo ya kuogea "hayafai" kuswakia.

Lakini kama wasemavyo, "msafiri kadiri", katika tembea zangu vijijini, nilikutana na mazingira ambapo unapotengewa maji ya kuogea Asubuhi, unatarajiwa utumie yayo hayo kuswakia.

Hauelekezwi kufanya hivyo, lakini unapoona wenyeji wako wakifanya hivyo, kwamba, labda, baba mwenye nyumba alipoingia bafuni kuoga alienda na mswaki wake akamaliza kila kitu huko, wewe unapaswa kufanya nini?

Kwa kuwa nilishajijengea imani kuwa hayo maji hayafai, nilikuwa naenda kuoga, nikishatoka bafuni, najifanya nilikuwa nimesahau kwenda na mswaki wangu. Nilikuwa siwaambii ukweli kuwa siyaamini maji yaliyopo kwenye ndoo ya kuogea kuwa yanafaa kusafishia kinywa. Kwa hiyo nikitoka tu bafuni, ama nilikuwa navuta muda kidogo au papo hapo huomba maji masafi kwenye jagi kwa ajili ya kwenda kuswakia.

Ni miaka mingi sasa imeshapita bila kukutana na hayo mazingira! Lakini unafikiri huo mtazamo wangu ulikuwa sahihi?

Au, kwa usahihi zaidi, nipo sahihi? Kwa sababu hata sasa bado imani yangu ni iyo hiyo!

Ni usafi au mtazamo tu?
 
Upo sahihi kabisa mkuu, maji ualiyopo kwenye ndoo ya kuogea unayapelekaje kinywani? Kumbuka ndoo ya kuogea inakaa chooni ambapo kuna uchafu pamoja na harufu mbaya, hadi hapo kwa mtu alie timamu kichwani hawezi kutumia hayo maji kuswakia.

Mimi sijawahi kukutana na kadhia hiyo, labda kwasababu sijakulia kijijini...

Mimi kuna ile tabia moja inanihuzunisha sana, ukienda ugenini kikatengwa chakula basi maji ya kunawa yanawekwa kwenye bakuli halaf mnanza kunawa mmoja mmoja kwa kupokezana, utakuta hadi inafika zamu yako kunawa maji yashakua meusi, yaani unanawa uchafu wa wengine.

Huwa najiuliza hivi watu wanashindwa vipi kung'amua huu utaratibu hauko sawa?
 
Kati ya vitu vilivyonisumbua, hasa miaka ya nyuma nilipokuwa nikienda ugenini vijijini, ni suala la kuswaki kwa kutumia maji yaliyowekwa kwenye beseni/ndoo ya kuogea. Tokea nikiwa mdogo, nilishajizoesha kuwa maji ya kwenye ndoo ya kuogea "hayafai" kuswakia.

Lakini kama wasemavyo, "msafiri kadiri", katika tembea zangu vijijini, nilikutana na mazingira ambapo unapotengewa maji ya kuogea Asubuhi, unatarajiwa utumie yayo hayo kuswakia.

Hauelekezwi kufanya hivyo, lakini unapoona wenyeji wako wakifanya hivyo, kwamba, labda, baba mwenye nyumba alipoingia bafuni kuoga alienda na mswaki wake akamaliza kila kitu huko, wewe unapaswa kufanya nini?

Kwa kuwa nilishajijengea imani kuwa hayo maji hayafai, nilikuwa naenda kuoga, nikishatoka bafuni, najifanya nilikuwa nimesahau kwenda na mswaki wangu. Nilikuwa siwaambii ukweli kuwa siyaamini maji yaliyopo kwenye ndoo ya kuogea kuwa yanafaa kusafishia kinywa. Kwa hiyo nikitoka tu bafuni, ama nilikuwa navuta muda kidogo au papo hapo huomba maji masafi kwenye jagi kwa ajili ya kwenda kuswakia.

Ni miaka mingi sasa imeshapita bila kukutana na hayo mazingira! Lakini unafikiri huo mtazamo wangu ulikuwa sahihi?

Au, kwa usahihi zaidi, nipo sahihi? Kwa sababu hata sasa bado imani yangu ni iyo hiyo!

Ni usafi au mtazamo tu?
Ubibini kwenu wapi?
 
Vijijini hakuna ndoo ya maji ya kuoga au maji ya kunywa zote zinafanya kazi moja ni jambo LA kawaida na maisha yanaenda
Kijijini wapi huko hamtofautishi ndoo za kuogea na za maji ya kunywa?
 
Back
Top Bottom