Utata: Hivi kweli Mungu anamchukia/hapendezwi na shetani au lao moja?

Utata: Hivi kweli Mungu anamchukia/hapendezwi na shetani au lao moja?

katib mkoa

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2015
Posts
1,574
Reaction score
2,161
Kwanini hamchukulii hatua shetani ?

Shetani ana nguvu kumliko?

Anafurahishwa na matendo ya shetani?

Wana lengo moja?

Hana njia yoyote ya kumzuia mpaka binadamu tumsaidie?

Kama Gwajima, Mwamposa kweli wanatoa mapepo/mashetani ndani ya watu yeye anashindwa nini kumtoa duniani kabisa?

Mbona binadamu tukikosea anashusha magharika eg. Nuhu, Sodoma, Babeli
ameshindwa kumpelekea taflani shetani akaangamia? au hajui halipo?

Mwisho binadamu tuache kiherehere cha kumchukia shetani ilihali Mungu na uwezo wote anamungalia tu lao moja
 
unauliza swali na unaconclude? sasa ni swali au ulikua unatuhabarisha?
 
Kwa Mungu siku moja ni kama siku elfu moja na siku elfu moja ni sawa na siku moja! kwahiyo wakati wa shetani bado.
kwaio mungu hana tatizo na shetani wakati huu? mpaka mda wake ukifika
 
Usiwe na haraka, shetani anaujua wakati wake na anakimbizana na muda, na wewe fahamu wakati wako.
Choices ni mbili tu: Moto au Mbingu. MUNGU hapangiwi lini atoe adhabu.

Wale kuku wako pale nyumbani huwa wanakupangia lini umchinje yupi?

Sisi wote ni viumbe wake na keshaamua kuwa asiyekubali njia zake kiberiti kinamuhusu. Kazi kwako.
 
m

mfano wa kuku hauendani!

ulitakiwa uchukulie mfano wa nyoka akiwa ndani kwako utaendelea kumlea lea ?na ndani kuna watoto uwapendao wasiojua kitu

au magugu shambani unaweza kuyavumilia wakati yanakuharibia mazao yako?
 
Ndugu yangu, mfano wa kuku nimekupa ili uone nguvu ya umiliki. Ss kuku ww umenunua ila hawakupangii unawachinja kwa mtindo upi, au unawatunza kwa mtindo upi, sasa imagine anayekumiliki kwa kukuumba.
 
Back
Top Bottom