Utata kuhusu kifo cha mwanafunzi aliyedaiwa kupigwa na mwalimu

Utata kuhusu kifo cha mwanafunzi aliyedaiwa kupigwa na mwalimu

Kitu cha kwanzaa Hakuna Jino linaweza kutoa damu mpaka mtu anakufa bila hawa wazazi wake kujuaaa bora wangesema internal bleeding sio jino... Alafu why mwalimu atumie Ngumi na makofi kumpiga mwanafunzi??? Aisee waalimu stress za maisha zitawauaaa
 
Mi sijaelewa. Huo ugonjwa husabisha damu itoke yenyewe tu bila sababu?!
Uongooo tuuu yani Cancer ya damu na jino kut9a damu wapi na wapiii uongoooo... Cancer ya damu sio kitoto hivyooo yani mwenye cancer ya damu maumivu yake hamuwezi kulalaa..!! Madaktari wametumika.kuficha ukweli
 
Licha ya kuwa Kuna baadhi ya walimu wanakosea, watu wengi Wana chuki binafsi na walimu

Kuna matukio mengi makubwa yanaendelea kwa madaktari, wanasiasa, mapolisi nk ila kesi ikiwa kwa walimu ndio huwa inakuwa multiplied mara 100

Kuna watu humu kuwalea watoto wao tu wanashindwa, then assume unakuwa na watoto 200 walioshindikana kwa wazazi wao

Wakati huo huo mkumbuke, Kuna mikakati ya kiwilaya na kimkoa inataka shule zifanye vizuri, zisipofanya vizuri huwa walimu au shule inawajibishwa

Yaani hapo ukiwa serious utakutana na matukio kama haya, ukiwa free utakuja kusemwa na wazazi, walimu na wanafunzi hawana Nidhamu, wanafelisha, yaani hakuna la afadhali


Kuna mwalimu alikuwa na slogan yake " BORA SHULE IFELI KULIKO MAMBO YANGU YAFELI"


Ni muda Sasa wa walimu kubadilika, hakuna haja ya kujichosha, fundisha kibosi, mwanafunzi asipoelewa achana naye ataelewa kwenye chumba Cha mtihani, fika shuleni mawazo yako yawe kwenye miradi yako

Wanafunzi wakifeli, hasara sio yako, wakifaulu faida ni yake na wazazi wake, hamna haja ya kujitesa na kuingia kwenye risk
Walimu wote wazingatie hili wataishi vema
 
Kwani walimu huwa wanapata Faida gani kuchapa wanafunzi?? Unajua yaani sielewi eti nitoke nyumbani niende kazini kuchapa viboko mtu
 
Riport ya [emoji61] hipo kisiasa Wala haina mantiki mkuu .


Naomba huyo Mwalimu Apewe kesi yake akapambane huko Mahakamani , kila siku tunawafundisha kuwa wasiwapige wanafunzi , lakini wanajitoa ufahamu na kuendeleza Viboko na kuua wanafunzi .


Mtu hujui History health background yake , lakini una-mu-Attack Hadi unamtoa uhai!! unanswered cries
Nenda ukafanye uchunguzi wewe, pengine una utaalamu zaidi ya [emoji61]‍[emoji3603]na daktari kwanini upingane na ripoti?
 
Hapa ndo unapoona ukichaa wa waalimu. Ripoti ya daktar iliyotoa taarifa ya sababu ya kifo cha marehemu. Inasema marehemu alifariki kwasababu ya kupoteza damu nyingi ambayo pia inatokana na ugonjwa wa saratani ya damu.

Sasa unajiuliza sababu ya marehemu kutokwa na damu ilikuwa ni nini? Au marehemu alikuwa na tatzo la kutokwa na damu pasipo kuwa na jeraha? Na kama kuvuja kwa damu kulisababishwa na uwepo wa jeraha je jeraha lilisababishwa na Nani?

Acheni ufala waalimu.
Kama Walimu ni vichaa, na wewe umefundishwa na hao vichaa hadi ukaweza kuandika hapa jf, basi amini na wewe ni kichaa
 
Huyo mwl ahame huko mtwara aseehhh...litamkuta jambo hawajui wamakonde huyooo
 
Sikuiz kila mtu anatembea na kifo chake ambacho kinatafuta sababu msipende kupiga watoto wa watu jaman

Sisi tumesoma pale jitegemee mtu unapigwa mpka ukitoka unajiuliza kweli nipo hai
 
Sijui waalimu wa Tz wanatumia Nini hawana tofauti na Vichaa , Mtu hujalala nae ,sio mwano , sio ndugu yako ...lakini unaamua kumpa mijeredi mikali Hadi anapoteza Fahamu kifo ulemavu * nk*
waalimu ndio walezi wa watoto wetu,tukisimamia nafasi zetu kama wazazi kisawasawa tunapunguza mikwaruzano isiyo ya lazima kati ya waalimu na watoto wetu.

kuna watoto kama mwalimu ukiwapuuza,unafanua na wengine wazuri 3 waharibike sababu yao.

NOTE :naunga mkono hoja kwamba si busara kupiga piga watoto kila wakati.
 
Mie ndio maana siku hizi sihangaiki na mtoto wa mtu.
 
Polisi huenda wamenyofoa karatasi za ripoti kamili ya daktari.
Polis wapi sajhihi tuache kuwa na mtazamo hasi dhidi ya waalimu.

Mwisho WA Siku waalimu watawasusia watoto wenu.

Hakuna mwalimu anayeweza kumpiga mtoto et Kwa mangumi na mateke.
 
Ah Kuna siku moja Niko form two nilikula hela ya mtihani kwahiyo matokeo yangu ya kuelekea form three hayakuja. Hata hivyo nikawa naendaga shule hivyohivyo nabaki pale form 2 D na wale ambao walifeli na wamekubali kurudia. Basi hiyo siku mbaya mwalimu Mapusu ( si jina lake) akanikamata nimedoji. Akanivuta wee mpaka eneo la paredi akaanza kunioshea kwa mademu. Sela son Mimi nikawa mdogo ka pirton . Napigwa vibao kila mahali. Ila akayumba sehemu moja akanishika nyuma kwenye suruali kipolisipolis huitwa Tanganyika jeki. Duh moyo ukajawa na hasira nikageuka Kama kimbunga nikamshika mwalim Mapusu shati lake na kumn'gan'gania asiendelee kunidhalilisha. Basi shati lake la khaki hivi mifuko miwili mbele likachanika. Ikawa taabu walimu wengine ka nyuki wanakuja kunichangia kwanini nampiga mwenzao. Baada ya siku mbili nikafukuzwa shule. Yule mwalim akanitia laana eti we dogo hutafaulu mitihani popote kuanzia form , four form six , na chuo hutafika kabisa eh bwana we nikapata shule nyingine nikasoma basi nikafaulu form four, six , chuo na Leo Niko na masters.
Mwalimu Mapusa ye yupo Kuna siku tulikutana kikaoni ananichekea eti anajisifu mwanafunzi wangu huyoo...
 
Polis wapi sajhihi tuache kuwa na mtazamo hasi dhidi ya waalimu.

Mwisho WA Siku waalimu watawasusia watoto wenu.

Hakuna mwalimu anayeweza kumpiga mtoto et Kwa mangumi na mateke.
Nilishapigwa kibao na mwalimu nikaamkia ward namba 6 hospitali Mt. Meru Arusha.
 
Back
Top Bottom