Utata kuhusu kifo cha mwanafunzi aliyedaiwa kupigwa na mwalimu

Kitu cha kwanzaa Hakuna Jino linaweza kutoa damu mpaka mtu anakufa bila hawa wazazi wake kujuaaa bora wangesema internal bleeding sio jino... Alafu why mwalimu atumie Ngumi na makofi kumpiga mwanafunzi??? Aisee waalimu stress za maisha zitawauaaa
 
Mi sijaelewa. Huo ugonjwa husabisha damu itoke yenyewe tu bila sababu?!
Uongooo tuuu yani Cancer ya damu na jino kut9a damu wapi na wapiii uongoooo... Cancer ya damu sio kitoto hivyooo yani mwenye cancer ya damu maumivu yake hamuwezi kulalaa..!! Madaktari wametumika.kuficha ukweli
 
Walimu wote wazingatie hili wataishi vema
 
Kwani walimu huwa wanapata Faida gani kuchapa wanafunzi?? Unajua yaani sielewi eti nitoke nyumbani niende kazini kuchapa viboko mtu
 
Nenda ukafanye uchunguzi wewe, pengine una utaalamu zaidi ya [emoji61]‍[emoji3603]na daktari kwanini upingane na ripoti?
 
Kama Walimu ni vichaa, na wewe umefundishwa na hao vichaa hadi ukaweza kuandika hapa jf, basi amini na wewe ni kichaa
 
Huyo mwl ahame huko mtwara aseehhh...litamkuta jambo hawajui wamakonde huyooo
 
Sikuiz kila mtu anatembea na kifo chake ambacho kinatafuta sababu msipende kupiga watoto wa watu jaman

Sisi tumesoma pale jitegemee mtu unapigwa mpka ukitoka unajiuliza kweli nipo hai
 
Sijui waalimu wa Tz wanatumia Nini hawana tofauti na Vichaa , Mtu hujalala nae ,sio mwano , sio ndugu yako ...lakini unaamua kumpa mijeredi mikali Hadi anapoteza Fahamu kifo ulemavu * nk*
waalimu ndio walezi wa watoto wetu,tukisimamia nafasi zetu kama wazazi kisawasawa tunapunguza mikwaruzano isiyo ya lazima kati ya waalimu na watoto wetu.

kuna watoto kama mwalimu ukiwapuuza,unafanua na wengine wazuri 3 waharibike sababu yao.

NOTE :naunga mkono hoja kwamba si busara kupiga piga watoto kila wakati.
 
Mie ndio maana siku hizi sihangaiki na mtoto wa mtu.
 
Polisi huenda wamenyofoa karatasi za ripoti kamili ya daktari.
Polis wapi sajhihi tuache kuwa na mtazamo hasi dhidi ya waalimu.

Mwisho WA Siku waalimu watawasusia watoto wenu.

Hakuna mwalimu anayeweza kumpiga mtoto et Kwa mangumi na mateke.
 
Ah Kuna siku moja Niko form two nilikula hela ya mtihani kwahiyo matokeo yangu ya kuelekea form three hayakuja. Hata hivyo nikawa naendaga shule hivyohivyo nabaki pale form 2 D na wale ambao walifeli na wamekubali kurudia. Basi hiyo siku mbaya mwalimu Mapusu ( si jina lake) akanikamata nimedoji. Akanivuta wee mpaka eneo la paredi akaanza kunioshea kwa mademu. Sela son Mimi nikawa mdogo ka pirton . Napigwa vibao kila mahali. Ila akayumba sehemu moja akanishika nyuma kwenye suruali kipolisipolis huitwa Tanganyika jeki. Duh moyo ukajawa na hasira nikageuka Kama kimbunga nikamshika mwalim Mapusu shati lake na kumn'gan'gania asiendelee kunidhalilisha. Basi shati lake la khaki hivi mifuko miwili mbele likachanika. Ikawa taabu walimu wengine ka nyuki wanakuja kunichangia kwanini nampiga mwenzao. Baada ya siku mbili nikafukuzwa shule. Yule mwalim akanitia laana eti we dogo hutafaulu mitihani popote kuanzia form , four form six , na chuo hutafika kabisa eh bwana we nikapata shule nyingine nikasoma basi nikafaulu form four, six , chuo na Leo Niko na masters.
Mwalimu Mapusa ye yupo Kuna siku tulikutana kikaoni ananichekea eti anajisifu mwanafunzi wangu huyoo...
 
Polis wapi sajhihi tuache kuwa na mtazamo hasi dhidi ya waalimu.

Mwisho WA Siku waalimu watawasusia watoto wenu.

Hakuna mwalimu anayeweza kumpiga mtoto et Kwa mangumi na mateke.
Nilishapigwa kibao na mwalimu nikaamkia ward namba 6 hospitali Mt. Meru Arusha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…