Utata kuhusu mirathi ya watoto wa familia iliyoishi bila ya kuoana

Utata kuhusu mirathi ya watoto wa familia iliyoishi bila ya kuoana

Kwenye masuala ya ndoa, ukiishi na mwanamke kwa zaidi ya miaka miwili, presumably kutakuwa na ndoa, s. 160 of Law of Marriage Act. Lakini endapo itafanikiwa kuonyeshwa kwamba mmoja kati ya hao wanandoa walikuwa na ndoa halali na ambayo bado haijavunjwa hiyo dhana ya ndoa basi itakufa.
Lakini kwenye maswala ya mirathi ni tofauti kidogo kwa sababu wanaangalia kama huyo aliyefariki alikuwa na ndoa ya aina gani, mfano; ndoa za kimila, ndoa za kidini(kikristo na islam) pamoja na ndoa za bomani.

Na zaidi wataangalia marehemu alitaka mali zake zigawiwe kwa aina gani (hii hutokea pale marehemu alipoacha waraka) Basi kwa yule aliyeidhinishwa ndani waraka kuwa msimamizi wa mirathi ataomba mahakamani kuwa msimamizi halali wa hiyo mirathi akiambatanisha huo waraka kwenye maombi yake mahamakani(katika eneo ambapo marehemu alipata umauti wake)
Na endapo hakuna waraka basi wataangalia aina ya maisha aliyoishi yule marehemu. Na hapo basi kikao cha familia kitakaa na kumchagua msimamizi wa mirathi na kuandika barua ya uteuzi ambapo aliyeteuliwa atafanya maombi mahakamani kuomba kuwa msimamizi wa mirathi
 
Back
Top Bottom