Mtumishiwetu
Senior Member
- Jul 13, 2022
- 196
- 346
Waziri wa Fedha, Mwigulu Lameck Nchemba Madelu ametoa tamko bungeni Septemba 20 2022 na kutangaza rasmi kufuta tozo mbalimbali za miamala ya kielektoniki bila kueleza ni kikao gani cha kisheria kilichoruhusu mchakato huo wa kufutwa kwa mapato ambayo tayari yamekadiriwa kwenye bajeti ya Serikali na kuidhinishwa na Bunge la Bajeti la Mwaka 2022/23. Sisi kama Wanasheria tunajiuliza maswali mengi bila majibu.
Mwigulu amefuta mapato yatokanayo na tozo za miamala ya simu na benki bila kupitia utaratibu wa Bunge kama Sheria inavyomtaka, lakini pia ametangaza kupunguza matumizi ya chai, vitafunwa, semina, mafunzo, warsha, matamasha, safari za ndani na nje na misafara ya viongozi mafungu ambayo yalipitishwa na Bunge.
Ninavyojua mimi Waziri wa Fedha alipaswa kuwasilisha bungeni Muswada au Azimio la Bunge linaloliomba Bunge kufuta au kuazimia mabadiliko hayo badala ya kusoma Kauli ya Mawaziri ndani ya Bunge ambayo kimsingi haina mjadala na haiamuliwi na Bunge na hivyo si sehemu ya maamuzi ya Bunge ni kama kiini macho tu na danganya toto kwa wananchi.
Waziri wa Fedha hana nguvu yoyote kisheria kufuta mapato yaliyopitishwa na Bunge, kufanya hivyo ni kuvunja Sheria za nchi ambazo ameapa kuzilinda. Sheria ya Bajeti, Sheria ya Fedha na Sheria ya Matumizi (The Appropriation Act), kwa nini wabunge hili wameliruhusu na uvunjaji wa sheria kufanyika ndani ya Bunge?
Waziri wa Fedha katika tamko lake hajaeleza ni mapato kiasi gani yatapungua kwenye Bajeti ya Serikali kutokana na maamuzi yake ya kufuta tozo kama Sheria inavyotaka. Maamuzi haya yamefanyika kienyeji sana bila kujali kuwa yanaenda kuathiri bajeti, mapato yanapungua na matumizi yanapungua
Kwenye maelezo yake Waziri wa Fedha ameshindwa kueleza vyanzo mbadala vya mapato vitakavyofidia hayo aliyoyafuta na badala yake ameagiza kupunguzwa kwa matumizi ya kawaida ya semina, warsha, matamasha, safari za ndani na nje ya nchi, kukata misafara ya viongozi ambapo pia hakueleza ni fedha kiasi gani zinakwenda kupunguzwa katika matumizi hayo aliyoyaita hayana ulazima.
Mwigulu ameshindwa kusema ni fedha kiasi gani zilikadiriwa katika matumizi hayo na yanaenda kupunguzwa kwa kiasi gani? Kiufupi Waziri wa Fedha hana uhakika namna mapato hayo yatakavyofidiwa na badala yake ametoa maelezo yasiyoeleweka.
Waziri wa Fedha amefuta tozo na kodi ambapo kipindi cha bajeti licha ya ushauri aliopewa na wabunge yeye aling’ang’ania tozo na kodi hizo ziwepo, tozo za miamala ya mabenki, simu na utaratibu wa ulipaji property tax ulikataliwa. Lakini Waziri alitangaza bungeni kuwa ni bora awe unpopular minister lakini tozo ni lazima.
Mwigulu amewahadaa watanzania kupitia Bunge kuwa timu ya watalaamu wa Wizara ya Fedha Idara za Bajeti na Sera wamefanya uchambuzi wa kina kufikia maamuzi hayo lakini baadaye kwenye maelezo yake anatangaza kumuelekeza kupitia Bunge Mlipaji Mkuu wa Serikali kukaa na maafisa masuuli wote na kuyaangalia upya mafungu ya matumizi mengineyo (OC) na kuyapunguza jambo ambalo linaonekana ni mzaha wa hali juu kwa watanzania jambo la kusikitisha wabunge wetu wako kimya.
Ninachokiona hapa uamuzi huo wa Mwigulu wa kudai amefuta tozo umefanyika bila kuwashirikisha maafisa masuuli wa Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali lakini awali kwenye taarifa yake amesema maamuzi haya yameshirikisha wadau nashindwa kuelewa Daktari wa uchumi anakwamaje kiasi hiki.
Mwigulu kama aliju matumizi ya chai, vitafunwa, mafunzo, warsha, semina, matamasha, safari za ndani na nje na misafara mikubwa ya viongozi hayana umuhimu kwa taifa kwanini yalitengewa fedha kwenye bajeti na kupitishwa na Bunge na kutusabibishia wananchi mzigo mkubwa na kwa tafsiri nyingine kwa mujibu wa Mwigulu inamaana tozo hizi zilianzishwa kwa ajili ya kufanikisha matumizi ya anasa serikalini na sio miradi ya maendeleo ya wananchi kama tulivyoaminishwa watanzania hapo awali.
Watanzania wote tunakumbuka Waziri Nchemba kwa kipindi kirefu tangu ameteuliwa kushika wadhifa huo amekuwa akitoa kauli tata na za kejeli kubwa sana sana kwa wananchi hizi ni baadhi ninazozikumbuka mimi wengine mtaongezea.
(i) Wananchi wengi tulipolalamikia tozo kubwa yeye akajibu niko tayari kuwa unpopular Minister lakini tozo ni lazima na Mtanzania yoyote anayeona Burundi kuna unafuu wa maisha basi aende Burundi kauli ambayo ilileta simanzi kubwa kwa wananchi.
(ii) Wananchi walipokosoa uanzishwaji wa tozo, alisema kuwa tozo zote zimewekwa kwa mujibu wa Sheria na zimepitishwa na Bunge yeye kama Waziri hana uwezo wa kufanya chochote na amefungwa mikono lakini leo anaziondoa tozo hizo bila ridhaa ya Bunge na kwa kuvunja Sheria.
(iii) Watanzania walipolalamikia ugumu wa maisha, alisema suala la ugumu wa maisha tusilaumiane, Waziri huyo hakuna hatua zozote alizowahi kuchukua kukabiliana na ugumu wa maisha na alitaka watanzania wamlaumu nani kama sio Waziri wa Fedha na Mipango
(iv) Waziri wa Fedha aliendelea kutoa kauli tata juu ya wananchi wanaomlaumu kwa utendaji wake mbovu na yeye akasema kwani wao hawakoseagi majumbani kwao
Kauli hizi tata zinazotolewa na Waziri Mwigulu zinathibisha ukosefu mkubwa wa maadili na nidhamu kama Mtumishi wa Umma na pengine hafahamu vizuri Sheria za nchi.
Kwa ufupi Mwigulu amevunja Sheria za nchi na amewathibitishia watanzania kuwa hana uwezo kumudu wadhifa alionao wa Waziri wa Fedha na alipaswa kujipima na kuachia ngazi kwa manufaa ya umma.
Sambamba na hilo Kamati ya Bunge ya Bajeti inayomsimamia Waziri wa Fedha ilipaswa iwe imevunjwa na Spika wa Bunge kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake iliyokasimiwa na wananchi tukashangaa tunatangaziwa imevunjwa Kamati ya LAAC peke yake.
Spika alijifanya kumbana Waziri kwenye Swali la TRAB na TRAT bungeni lakini ukweli Spika ndiye amechangia kutowajibika kwa Mwigulu kwani Kamati ya Bunge inayotuwakilisha wananchi ni kama imeamua kutusaliti kwa masilahi yao na Mwigulu na sio masilahi mapana ya taifa letu pendwa la Tanzania
uchambuzi wetu wanasheria.
COPY & Paste