Utata wa Katiba:hakuna kimbilio zaidi ya Nyerere?

Utata wa Katiba:hakuna kimbilio zaidi ya Nyerere?

Jackbauer

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Posts
6,053
Reaction score
2,207
Kuna mkongwe ameniambia kuwa kipindi kile cha vuguvugu la G55 na Tanganyika,mzee ruksa alituma kikosi kazi kwenda kumuona Mwalimu Nyerere ili atoe ufafanuzi juu ya misingi ya katiba/serikali mbili.
Mwalimu alitoa suluhisho na hatimaye vuguvugu hilo likapoa!

Nikiangalia mwenendo wa majadiliano yanayoendelea kuhusu katiba/serikali mbili au tatu naona hakuna kimbilio la msulihishi zaidi ya hayati baba wa Taifa.
 
Mnazidi kuwafanya Wananchi wajute kulipa kodi ,mnadai kodi kwa kishindo ,hizo hela hizo za posho si ajabu wanachi wakadai mzirudishe !
 
"Labda ni vizuri kukumbuka kwamba shabaha ya baadhi yetu ilikuwa ni kuziunganisha nchi za Afrika Mashariki ziwe Nchi Moja. Na wakati Zanzibar na Tanganyika zinaungana, Kenya, Uganda na Tanganyika zilikuwa katika mazungumzo ya kutafuta uwezekano wa kuungana. Kama jambo hilo lingetokea, nina hakika kabisa kwamba mfumo wa nchi mpya ambayo ingezaliwa ungekuwa ni wa Shirikisho: ama Shirikisho la Nchi Tatu zenye Serikali Nne, au Shirikisho la Nchi Nne zenye Serikali Tano. Kwa kweli hata kesho Nchi za Afrika Mashariki zikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye Serikali mbili - ya Zanzibar na ya Tanganyika - kuliko Tanzania yenye Serikali mbili, ya Tanzania na Zanzibar. Wapendao Utanganyika watakuwa wazalendo zaidi, badala ya kuwa wasaliti, wakiazimia Afrika ya Mashariki iliyoungana kuwa Nchi Moja, kuliko Tanzania iliyotengana ikawa nchi mbili" - Julius K. Nyerere's (1995: 16-17)
Uongozi Wetu Na Hatima ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom