Utata wa Kesi za Ugaidi na Mtihani wa Taswira ya Tanzania Kuelekea AFCON

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
267
Reaction score
1,014
Tanzania inapokipiga kambi katika ukurasa wa historia ili kuwa mwenyeji wa matukio makubwa ya kimataifa, ikiwemo mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), taifa hili linajikuta katika njiapanda ya kipekee.

Upande mmoja ni hitaji la msingi la kuhakikisha ulinzi na salama wa raia, wageni, na miundombinu. Upande wa pili ni shinikizo la kulinda misingi ya demokrasia, utawala wa sheria, na uhuru wa maoni.

Hivi karibuni, hatua za vyombo vya ulinzi na usalama kuwakamata watu zaidi ya 130 na wengine kufunguliwa mashtaka mazito ya ugaidi zimeibua mjadala mzito unaogusa hisia za kisiasa, kisheria, na kijamii nchini.

Je, operesheni hizi ni sehemu ya kulinda amani kuelekea AFCON, au ni turufu ya kisiasa inayolenga kulazimisha ajenda ya maridhiano?

Kesi za Ugaidi na Shaka ya "Ajenda ya Maridhiano"

Katika jicho la sheria na siasa, mashtaka ya ugaidi dhidi ya wanaharakati, wanasiasa, na wasomi yameibua mtazamo kinzani.

Kwa mujibu wa wachambuzi wa mambo na wanasheria wanaona wimbi hili la kesi nzito lina sura na mlengo wa kisiasa.

Hoja hii inajengwa kwenye misingi ya nani hasa waliojikuta mikononi mwa dola; wengi wakiwa ni wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), pamoja na wanataaluma kama Dk. Malikisedeki Kaijage, mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Hoja kuu inayoibuliwa hapa ni "ajenda ya maridhiano." Kulingana na mtazamo huu, kesi hizi huenda sio matokeo ya tishio halisi ya ugaidi wa kutisha, bali ni mkakati wa makusudi wa mamlaka kutengeneza ombwe la hofu ili kuwatia kitanzini viongozi wa vyama vya upinzani.

Pindi wanachama wao wanapokabiliwa na mashtaka yanayoweza kuzuia dhamana na kutishia uhuru wao wa kudumu, viongozi hao hulazimika kukaa mezani na Serikali kufanya "maridhiano." Swali la msingi linalohojiwa na wananchi ni: Je, maridhiano haya yanahusu nini, na wahusika wakuu ni akina nani katika mchezo huu?

Kasoro za Kisheria na Tafsiri ya "Ugaidi"

Akiijadili Sheria ya Kuzuia Ugaidi, Sura Na. 19 ya Tanzania (kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2023), mwanasheria, Patience Mlowe anasema kesi nyingi za ugaidi zinazofunguliwa katika mazingira haya hazina msingi wa kisheria.

“Kifungu cha 4(4) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi (Sura ya 19, Marekebisho ya 2023) kinasema wazi kuwa: kitendo chochote kinachoharibu utolewaji wa huduma za kijamii, au kimefanywa kwa dhamira ya mgomo, maandamano, au kuzuia kazi, hakitachukuliwa kama kitendo cha ugaidi kwa mujibu wa tafsiri iliyotolewa na sheria hiyo.

“Kwa nyongeza, Kifungu cha 4(2) cha sheria hiyo kinaweka msisitizo kwenye uzito wa dhamira (intent). Kitendo lazima kiwe cha ukubwa wa kiwango cha juu (sheria inatumia neno la Kiingereza "seriously"),” anasema Mlowe.

Anadokeza kuwa namna watuhumiwa wengi walivyokamatwa kwa makosa yanayotokana na harakati za siasa, mikusanyiko, au ukosoaji inafanya iwe vigumu mno kisheria kuthibitisha ni kwa kiwango gani vitendo vyao vilifikia vigezo vya kuhatarisha taifa "seriously" kiasi cha kuitwa ugaidi.

CHADEMA wang’aka wanachama wao kukamatwa kwa ugaidi

HECHE JF.jpg
Julai 25, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza, alieleza kuwa hatua za kuwakamata wanachama wake Zaidi ya 50 na kuwapa kesi za ugaidi, haitapita kimya kimya kama "masuala ya kawaida ya kiusalama."

Soma pia: Heche: Tutawaandikia barua FIFA na CAF kuwaeleza Serikali imesema kuna 'Ugaidi' wasilete Watu AFCON

Alisema wataziandikia barua taasisi za kimataifa kulalamikia ukamataji huo, yakiwamo mashirika ya kimataifa ya mpira wa miguu ikiwemo FIFA na CAF na taasisi za kimataifa za haki za binadamu.

“Tumesema tutawaandikia Amnesty International, tutawaandikia UN Human Rights Commission, tutawaandikia kila mtu na sio kwamba tunaandika lini, tumeshaandika barua na zitakuwa mtaani… kuanzia Jumatatu (Julai 27) zitakuwa kwenye ofisi zinazohusika,” alisema.

Aliyaomba mashirika ya utetezi wa haki za binadamu kama Kituo cha Sheroa na Haki za Binadamu (LHRC), Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) kuwaongezea nguvu kwa kuwapa mawakili wa kutetea kesi za makada wao waliokamatwa.

Hoja ya Heche ni kwamba usalama wa nchi hauwezi kujengwa kwa kudharau haki za binadamu, na matumizi ya nguvu za vyombo vya dola yanaweza kuipakaza tope nchi machoni pa ulimwengu, hususan katika nyakati ambazo jicho la dunia linaiangalia Tanzania kupitia lenzi ya michezo.

Kwa upande wake, Mwanasheria mkuu wa CHADEMA, Dk. Rugemeleza Nshala, ameahidi kuwa jopo la wanasheria wa chama hicho linatolea macho mchakato mzima wa kisheria unaoendelea.

Nshala alitaja misingi mitatu isiyokwekwa ambayo watapambana kuilinda ambayo ni haki ya kufikishwa mahakamani kwa wakati bila kuwekwa kizuizini kinyume na sharia, haki ya kupata dhamana kwenye makosa ambayo sheria inaruhusu, haki ya uwakilishi wa kisheria na kusikilizwa.

Nshala alibainisha wazi kuwa kutumia mashtaka ya ugaidi dhidi ya raia ni jambo zito lenye athari za kisaikolojia, kijamii na kiuchumi. Kwa hiyo, serikali inapaswa kutenda kwa weledi na uaminifu mkuu ili sheria ifuate mkondo wake badala ya kuonekana inanyanyasa wakosoaji.

Serikali yahaha kujinasua kwenye “Ugaidi”

KATAMBI JF.png
​

Katika hali inayoonyesha kujutia mashitaka ya ugaidi, Serikali imeanza kutoa ufafanuzi, huku pia ikipinguza hali ya hifu iliyokuwa imetanda.

Soma pia: Katambi: Tanzania hakuna Ugaidi, kunaweza kuwa na viashiria
Akitoa ufafanuzi kuhusu ukatwaji wa wananchi na mashitaka ya ugaidi Julai 29, 2026, visiwani Zanzibar, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi alisema kuna upotoshaji unaoendelea kwenye mitandao ya kijamii, akiwaweka wazi wananchi kuwa nchi ipo salama na shughuli za maendeleo zinapaswa kuendelea kama kawaida.

Waziri Katambi alisema hakuna kinga ya jinai kwa wanasiasa.

Alisema, mtu yeyote anayekiuka sharia, awe mwanasiasa, mfanyabiashara, au kiongozi wa dini, atachukuliwa hatua.

Katambi alibainisha wazi kuwa utawala wa sheria na uhuru wa mahakama vinaheshimiwa, lakini hakuna mtu aliye juu ya sheria.

Kuhusu ugaidi, Katambi alisisitiza kuwa Tanzania haina ugaidikwa maana ya matukio makubwa ya kigaidi kama milipuko au utekaji wa kutisha, lakini akasema kuna "viashiria vya matendo ya kigaidi."

Alivitaja viashiria hivyo vikijumuisha vipengele kadhaa vya makosa (elements of offense) ikiwamo kupanga, kuratibu, na kula njama za uvunjifu wa Amani, kutishia au kutekeleza vitendo vinavyoweza kuleta madhara, kuandaa zana zinazoweza kuzuia shughuli za kiuchumi za nchi.

Waziri alieleza kuwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao sio kwa sababu ya vyama vyao au itikadi zao, bali kumetokana tu na ushahidi na taarifa za kiusalama zilizopatikana.

Alisema ni wajibu wa Polisi kumnasa mtuhumiwa yeyote, kisha kuliachia jukumu la kupima uthibitisho na kutoa haki mikononi mwa Mahakama.

Polisi wasema Usalama Umerejea Kikamilifu

Katika taarifa ya Julai 29, 2026, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) David Misime, DCP Misime alieleza kuwa hali ya usalama nchini ni shwari kabisa matokeo ya hatua madhubuti za vyombo vya ulinzi na usalama kudhibiti mipango ya wahalifu.

Polisi walifafanua kuwa katika kipindi kilichopita, kulikuwa na viashiria vya kuhatarisha amani vilivyowafanya wawashauri waandaaji wa mikutano ya kisiasa kuahirisha makongamano yao. Hata hivyo, baada ya "kurejea kikamilifu kwa usalama," Jeshi la Polisi sasa liko tayari kupokea taarifa za mikutano ya hadhara kutoka vyama vya siasa na wadau wengine, ilimradi watoe taarifa na kufuata utaratibu mbele ya Wakuu wa Polisi wa Wilaya (OCD). Misime aliwashukuru wananchi kwa ushirikiano wao wa kukataa kuchochewa na kundi lolote linalotaka kuvuruga amani.

Prof. Shivji: Mashtaka ya Ugaidi ni Silaha ya Hofu

Katika Makala yake, "Terrorising Academic Freedom in Tanzania", Profesa wa Sheria, Issa Shivji amejadili kukamatwa kwa Dk Melkisedeki Kitunzi Kaijage, mhadhiri msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), akisema ukamatwaji huo unalenga kuzua hofu kwa wanataaluma na wananchi kwa ujumla.

Shivji anaeleza kuwa hati ya mashtaka dhidi ya Kaijage (iliyodai alitishia kuchoma majengo ya umma na nyumba za polisi) imekosa ushahidi na maelezo ya msingi. Anasisitiza kuwa mashtaka haya makubwa hayana lengo la kutenda haki, bali ni mbinu ya kuwaadhibu na kupandikiza hofu ili kunyamazisha wasomi na wanataaluma wengine.

Kuhusu mazingira ya ukandamizaji nchini, Profesa Shivji amesema ukamataji unaoendelea nchini ni na wimbi pana la ukandamizaji nchini Tanzania, akitolea mfano wahadhiri wengine wawili wa Chuo Kikuu cha St. John's (UDOM) waliokamatwa baada ya kufundisha kuhusu kashfa za ufisadi wa kihistoria.

Pia anagusia mauaji ya vijana wengi wakati wa uchaguzi wa Oktoba 2025 na kesi za uhaini/ugaidi zinazowakabili viongozi na wanachama wa CHADEMA.

Profesa Shivji amehitimisha kwa kusema kuwa jumuiya ya wasomi barani Afrika ipo njiapanda kutokana na mifumo ya kiimla na changamoto za kijamii.

Anatoa wito kwa wanataaluma kuchagua ama kunyamazishwa na kupotea, au kuendelea kupaza sauti za upinzani na kuwajibika kwa jamii, bila kujali gharama zake.

AFCON na Mtihani wa Taswira ya Tanzania Kimataifa

Maandalizi ya Tanzania kuwa mwenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ni heshima kubwa iliyopokewa na kila Mtanzania.

Huu ni mtihani unaojaa fursa lukuki za kiuchumi, kitalii, na kidiplomasia. Hata hivyo, katika ulimwengu wa utandawazi wa sasa, mafanikio ya michuano hii hayataishia katika kupima ubora wa nyasi kwenye viwanja vipya, hoteli za kisasa, au uwingi wa mashabiki watakaofurika uwanjani.

Dunia ya sasa inapima usalama wa nchi pamoja na viwango vya utawala bora. Nchi yoyote yenye tishio la uvunjifu wa amani inao wajibu mtakatifu wa kuchukua hatua makini na za mapema dhidi ya uhalifu—lakini hatua hizo zinapokosa uwazi, kipimo, na kuheshimu mipaka ya haki za binadamu, husomwa haraka kama zana za ukandamizaji.

Serikali imeshikilia bango kuwa "Tanzania iko salama na ipo tayari kuwapokea wageni wote wa AFCON" na kwamba usalama ndio kipaumbele nambari moja. Kwa upande mwingine, jumuiya ya watetezi wa haki za binadamu na asasi za kimataifa zinatazama kama hatua hizo zitatekelezwa kwa namna inayoimarisha uhuru wa kujieleza badala ya kuufubaza.
 
Hu sio Ugadi?
Ukipelekwa mahakamani utajibu kabisa kuwa huo ni ugaidi?
 
Screenshot_20260616-173300~2.png
 
Back
Top Bottom