Ngwasa Omuyaya
JF-Expert Member
- Feb 13, 2014
- 2,650
- 2,776
Baada ya kifo cha mwl, Nyerere tuliona kasi ya uwekezaji ilivyoshika kasi na mikataba rahisi kwenye uwekezaji huo sijui nyuma ya pazia kuna siri gani.
Kitabu cha Msekwa chamtumbukiza ?katikati? ya mzozo
Maelezo yake na wasaidizi wa Mwl. Nyerere hayafanani
UTATA umeibuka kuhusu ni lini hasa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alipoteza fahamu alipokuwa akiumwa nchini Uingereza, baada ya kupatikana kwa taarifa mbili tofauti katika siku za karibuni.
Spika wa Bunge mstaafu na mmoja wa wanasiasa mashuhuri nchini, Pius Msekwa, ameandika kitabu anachodai kwamba alizungumza na Mwalimu kwa muda wa saa moja na nusu wiki moja kabla ya kifo chake; lakini wasaidizi wa Mwalimu wanadai kuwa Mwalimu alipoteza fahamu walau wiki mbili kabla ya kifo chake.
Kitabu hicho kiitwacho Uongozi na Utawala wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kinachoeleza kuhusu miaka 25 ya utumishi wa umma chini ya uongozi wa Mwalimu Julius Kambarage, kilichapwa mwaka 2012 lakini sasa ndipo mkanganyiko umeanza kujitokeza.
Maelezo hayo ya Msekwa yako katika ukurasa wa 33 wa kitabu hicho anapoeleza kuhusu mara yake ya mwisho kuonana na Mwalimu Nyerere mwaka 1999. Kimsingi, Msekwa ameandika katika kitabu hicho kwamba yeye ndiye kiongozi wa mwisho wa ngazi za juu nchini kuzungumza na Mwalimu kabla ya kifo chake.
Msekwa ambaye ni mmoja wa wanasiasa wanaoheshimika hapa nchini, ameandika kwamba alifanikiwa kuonana na Mwalimu Nyerere Oktoba 9, mwaka 1999 katika Hospitali ya St. Thomas jijini London, Uingereza na kuzungumza naye kwa muda usiopungua saa moja na nusu na ndipo akaondoka.
?Nilipangiwa utaratibu wa kumwona mahali alipokuwa amelazwa. Nikapata nafasi ya kuongea naye vizuri kwa muda usiopungua saa moja na nusu hivi, kuanzia saa sita na nusu mchana. Kutoka hapo, nilkwenda moja kwa moja Uwanja wa Ndege wa Gatwick kupanda ndege ya kurejea Dar es Salaam,? aliandika Msekwa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania kuanzia mwaka 1994 hadi mwaka 2005.
Hata hivyo, waliokuwa wasaidizi muhimu wa Mwalimu waliokuwa naye hospitalini London, wanasema kwamba haiwezekani Msekwa alipata nafasi hiyo ya kuzungumza na Nyerere. Hii ni kwa sababu wakati huo, tayari Mwalimu alikuwa hana fahamu.
?Sikiliza ndugu mwandishi, Mwalimu alikuwa kwenye comma (hakuwa na fahamu) kwa walau wiki mbili hivi kabla hajafariki dunia. Tarehe 9 Oktoba ni chini ya wiki moja kabla ya kifo cha Mwalimu kilichotokea Oktoba 14 mwaka huo. Ni wazi hapo Msekwa hakusema kweli,? alisema msaidizi huyo ambaye kwa sasa Raia Mwema haliwezi kutaja jina lake kwa sababu ya unyeti wa suala lenyewe.
Maelezo hayo ya msaidizi huyo yanafanana na maelezo ya msaidizi mwingine aliyesema kwamba uwezekano wa Mwalimu kuzungumza na yeyote katika wiki yake ya mwisho duniani haupo, kwa sababu ya hali aliyokuwa nayo wakati huo.
?Hapo mzee Msekwa atakuwa amewadanganya wasomaji wake kwa sababu ambazo sijazijua hadi sasa. Mimi nilikuwa London muda wote ambao Mwalimu alikuwepo na kwa uhakika kabisa naweza kukwambia kuwa hakuwahi kuzungumza na yeyote kwenye wiki yake ya mwisho,? alisema msaidizi huyo mwingine ambaye gazeti hili lilimtafuta kwa sababu ya kujiridhisha na maelezo ya mhojiwa wa awali.
Siku za mwisho za Mwalimu
Kwa sababu ya kutafuta ukweli wa habari hii, Raia Mwema lilizungumza na waliokuwa wasaidizi hao wa Mwalimu Nyerere kueleza kuhusu siku za mwisho za Baba wa Taifa zilivyokuwa ndani ya Hospitali ya Mtakatifu Thomas.
Gazeti hili limeambiwa kwamba kiongozi wa juu wa mwisho kuonana na Mwalimu na kuzungumza naye alikuwa Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, ambaye alimtembelea hospitalini hapo Septemba 25 mwaka 1999.
Hata hivyo, kwa uhakika, Raia Mwema limeambiwa kwamba Mwalimu alikuwa na shida ya kuzungumza na kwamba Mkapa ndiye aliyekuwa akimsemesha kwa kumtia moyo, kumfariji na kusali. Gazeti hili halijaweza kuthibitisha moja kwa moja kama Nyerere alizungumza chochote kwa Mkapa wakati huo.
Hata hivyo, ni hali hiyo ya Baba wa Taifa aliyokutwa nayo na Mkapa ndiyo iliyomfanya Rais huyo wa Awamu ya Tatu, ambaye kama ilivyo kwa Msekwa, alikuwa na historia ndefu binafsi na Mwalimu, aliamua kumwacha mkewe, Anna, London kwa ajili ya kuifariji familia katika wakati huo mgumu.
Raia Mwema limeambiwa kwamba hata Kingunge Ngombale Mwiru, aliyekuwa Waziri katika Serikali ya Mkapa na aliyetumwa kwenda kumtazama Mwalimu na kuwa mwakilishi wa serikali, hakupata fursa ya kuzungumza naye kwani alifika wakati Baba wa Taifa tayari amepoteza fahamu.
Akizungumzia madai hayo ya wasaidizi wa Mwalimu, Msekwa aliliambia gazeti hili juzi Jumatatu kwamba ni kweli yeye alizungumza na Mwalimu Nyerere wakiwa watu watatu tu; yeye, Baba wa Taifa na Mama Maria Nyerere.
?Hao wanaosema sikuzungumza na Mwalimu Nyerere ndiyo wanaokupotosha. Mimi nilizungumza naye na Mama Maria (mjane wa Mwalimu) alikuwepo. Nilipomaliza mazungumzo nikaondoka. Ninachofahamu ni kwamba nilipoondoka ndiyo hali ikabadilika na Mwalimu akapoteza fahamu.
?Nilipofika Dar es Salaam, moja kwa moja nilikwenda kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Frederick Sumaye , kumweleza kuhusu hali ya Baba wa Taifa kama nilivyomwona. Nakumbuka nilimweleza kuwa hali yake inatia matumaini. Zilipokuja baadaye habari kwamba Mwalimu ana hali mbaya, Sumaye aliniuliza mbona nilimwambia hali ni nzuri. Nikamwambia hali ilibadilika wakati nilipoondoka,? alisema.
Kwa mujibu wa kitabu hicho cha Msekwa ambacho ameruhusu Raia Mwema lianze kukichapa gazetini kuanzia Januari mwakani, Spika huyo mstaafu alipita London akitokea nchini Trinidad na Tobago alikokwenda kuhudhuria mkutano wa kila mwaka wa wabunge wa nchi zilizo kwenye Jumuiya ya Madola.
Katika mkutano huo, Msekwa alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola; akiwashinda wapinzani wake wawili ?mmoja kutoka Canada na mwingine Cyprus.
Credit: Raia Mwema newspaper
Mtizamo wako ni majungu lakini mtizamo wa wengi si majungu bali ni kutaka kupata Ukweli harisi .Mtazamo wangu sijapata hasa kisa chenye uzito cha kuweza kumuua Baba yetu wa taifa, wenzenu wanatumia hizi rumours / majungu kwa faida tofauti kabisa kwa kucheza na uwelewa wa jamii yetu pia tusisahau raia mwema kwa hii heading ni copy ngapi atauza ? ?
1. Kumbuka kuwa URAIS sio mkapa tu ni Institution na ni system of instituitions
2. Kumbuka London sio Tanzania kwamba serikali ingeweza kufanya hayo kwa at least 90% SIRI au hopt ya serikali
3.Jiulize kwa sasa muda woote huo bado mna bahatisha bahatisha kama kungekuwa na genuine Information huko huko london ungeyasikia yakiwa wazi wazi hasa magazetini.
4.Kumbuka Information kama hizo zina thamani kubwa sana, huwezi kuzizuia hata kwa pesa yapo makampuni makubwa sana kazi ni hiyo tu.
Nacho aamini mm ni kuwa watanzania tulimpenda/tunampenda sana baba yetu wa taifa na alitutoka kwa ghafla bila kutarajia na ni kawaida sana kwa jamii yetu kwa vifo vya ghafla huzua MAJUNGU MENGI lakini HAKUNA LOLOTE
M
Baada ya kifo cha mwl, Nyerere tuliona kasi ya uwekezaji ilivyoshika kasi na mikataba rahisi kwenye uwekezaji huo sijui nyuma ya pazia kuna siri gani.
Mkuu umeongea mambo mazito sana kumuhusisha mutu yeyote na kifo cha Nyerere si neno dogo
Kwa upole kabisa naomba nijibu swali hili ukiombwa ushahidi wa hayo uliuoyasema unaweza kuutoa?
Kama taifa tutakuwa tumepata pa kuanzia.
mkuu utawekwa korokoroni,ooh......
Kwa 100% Nyerere hakufa Kwa mapenzi ya mungu bali ilibidi Afe kuondoa kiwingu watu wapige pesa kirahisi pasipo kuwekewa Usiku.
Mmmh!! hapa kuna harufu ya kuliwa fedha nyingi kwa kuundwa TUME !!! "ULAJI" unaandaliwa... !!
the banker
Duh mkuu kuwa makini
Huyo msekwa na wew uliiweka hii habari wote ni majipu
Ngoja niwasiliane na mtumbuaji ajisogeze karibu yenu