Utata wa kiswahili

Utata wa kiswahili

Joined
Jul 17, 2013
Posts
5
Reaction score
0
Utata wa kisarufi ni kitu cha kawaida sana katika lugha zote duniani.. Utata huo waweza tokea kwa sababu mbalimbali.
Lakin kwa lugha yetu ya kiswahili utata huo wa kisarufi umezidia mipaka kiasi cha kukanganya fikra na mitazamo lukuki kwa wanahisimu na watumiaji wa lugha hii.
¡)Aina za maneno~ wengine wanasema kuna aina 7, 8, na wengine 9
¡¡)Uhesabuji wa silabi hasa ktk maneno kama mbwa, nje, nge n.k
¡¡¡)Uchanganuz wa sentensi
Hiyo ni baadhi tu ya mifano inayodhihirisha utata huo wa kisarufi.
SABABU HASA NI NINI?, NA NINI KIFANYIKE ILI WALAU KUPUNGUZA TATIZO HILO
 
kiswahili ni lugha pouwa
lets be proud like wat chinese are doing with their lang:smile-big:
 
Utata wa kisarufi ni kitu cha kawaida sana katika lugha zote duniani.. Utata huo waweza tokea kwa sababu mbalimbali.
Lakin kwa lugha yetu ya kiswahili utata huo wa kisarufi umezidia mipaka kiasi cha kukanganya fikra na mitazamo lukuki kwa wanahisimu na watumiaji wa lugha hii.
¡)Aina za maneno~ wengine wanasema kuna aina 7, 8, na wengine 9
¡¡)Uhesabuji wa silabi hasa ktk maneno kama mbwa, nje, nge n.k
¡¡¡)Uchanganuz wa sentensi
Hiyo ni baadhi tu ya mifano inayodhihirisha utata huo wa kisarufi.
SABABU HASA NI NINI?, NA NINI KIFANYIKE ILI WALAU KUPUNGUZA TATIZO HILO

Hebu funguka zaidi ili tujadili. Kwa mfano, unaposema 'kuna aina 7 za maneno' hebu zitaje kwanza tujue uanishaji huo.
Juu ya kuhesabu silabi, je unatumia kigezo gani? Na juu ya uchanganuzi, kuna 'utata' gani?
Tujulishe.
 
Mimi sioni kama kuna utata wowote ndani ya lugha ya Kiswahili kwa namna wewe unavyotaka kuuleta. Utata tunauleta siye tunaotaka kuiumba lugha kwa kutumia hesabu basi tukagawa, tukamjulisha, tukatoa mpaka tukapata sentensi ambayo kwa mtazamo wetu kisarufi imekaa sawa lakini ukimpa mswahili mwenye lugha yake tangu asili asipate maana ya kilichoandikwa japo kinasomeka.

Watu wengi ambao kiswahili ni lugha yao ya asili ukiwaambia wachanganue sentensi hawawezi, hasa kwa sababu hawakuisoma kama ni lugha ngeni kwao. Wale wanaosoma kiswahili kama lugha ngeni ama kama lugha ya pili baada ya lugha ya kinyumbani wao ndio hujibidiisha kukijua Kiswahili kwa kufuata mifumo hiyo unayoieleza hapo juu.

Basi hao ndio wanaoleta utata kwenye lugha ya Kiswahili na kukifanya Kiswahili kionekane kina utata.

Hebu soma ubeti huu ambao babu wa babu yangu aliachiwa na bibi yake, kisha unambie utata wa lugha hii uko wapi? Utata utaletwa tu na yule ambaye Kiswahili si lugha yake ya asili bali ni lugha ya darasani

"Kucha na kupambauka zamani hizi ni mara
Kuzinga na kuzunguka duni ni duara
Moyo sijifanye jura ni mengi tuweleyao"
 
Back
Top Bottom