UTATA WA MATUKIO. Orando pirates vs Simba Sc hapo jana.

kaka-blaza

Member
Joined
Nov 7, 2019
Posts
96
Reaction score
141
Kwanza kabisa napenda kusema kuwa sina taaluma yoyote ya Uamuzi(referee) katika soka, bali mimi ni mfuatiliaji wa soka...

napenda wataamu mnisaidie hapa

1: goli walilofungwa Simba, kwa mtazamo wangu niliona kama ni offside, kwani sio tu kwamba yule mfungaji wa Orando alizidi mkono tu, bali hata kichwa kilikuwa offside.

2: kipindi cha kwanza kuna mchezaji wa Orando alisukumwa kwa Nyuma ndani ya boksi la 18 ya Simba, lakini mwamuzi hakutaka kujiridhisha kwenye VAR, badala yake akaamuru adhabu iende kwa Orando .

3: kuna mchezaji mmoja wa Simba(jina limenitoka kidogo) alipigwa kiwiko cha makusudi kipindi cha pili mwishoni, wakati ambao Simba ameshafungwa na goli tayari. ajabu mwamuzi akatoa kadi ya njano pasipo kwenda kuangalia kwenye VAR, pengine ingekuwa ni Red Card.

4: Shomari Kapombe alionekana kuunawa mpira ambao ulipigwa kwa kichwa katika dakika ya mwisho ya mchezo , ikiwa ni shambulizi la kushtukiza na la mwisho kwa Orando . lakini mwamuzi hakutaka kwenda kujiridhisha kwenye VAR, . ambapo pengine ilistahili kuwa penati.

5: Joash Onyango alionekana kuunawa mpira ndani ya 18 . lakini mwamuzi akawasiliana a watu wa VAR na kuamua kuwa haikuwa penati,. hapo nikajiuliza au labda mkono unaanzia wapi katika soka. . maana ile haikuwa kwamba sijui mpira umefuata mkono, bali mkono ndio ulifuata mpira.

6: tukio la kwanza la Chris Mugalu alilopewa kadi ya njano, ukiangalia kwa makini, Mugalu alipiga mchezaji wa Orando kwa kiwiko, tena kwa kukusudia ,. ila akapewa njano . japo mbeleni alikuja kupewa red card ambayo ilikuwa halali pia.

7: Mohammed Hussein kupewa kadi ya njano alipokuwa anamuambia mwamuzi kwenda kujiridhisha kwenye VAR, ile hali yeye ni nahodha wa timu,. nadhani haikuwa uungwana


Mwisho... Weka akili za ushabiki pembeni, changia ki uanamichezo.

[emoji120][emoji120][emoji1241][emoji120][emoji120]
View attachment 2199835
 
Ndio ishatokea, sisi tunajipanga kwa michezo ijayo, na vema kujipanga kwa msimu ujao, kupunguza WATU na kuongeza WATU WA MAANA.

hata tuimbe vipi hakuna kitakachobadilika, man city vs everton, kuna ishu ya penati ilitokea refa akagoma, baada ya game kuisha bosi wa marwgmfa anapiga simu kwa bosi wa everton kumtaka radhi kwamba ile ilikuwa penati, ndio itakuwa hayo ya South africa.
 
1. Ndio ilikuwa offside lakini hakuna jinsi kama waamuzi wa VAR hawakumwambia refa aende kutizama.

2. Push ilikuwa ndogo sana jamaa ali dive kumdanganya refa.

3. Sikuiona hio lakini kumbuka refa hawezi kwenda kuangalia VAR mpaka wale waamuzi wasaidizi wa VAR wakiona maamuzi ya refa yana shaka wanamwita aje kutizama hili afanye maamuzi sahihi. Mchezo unakwenda kwa kasi sana sio rahisi refa kuona kila kitu.

4. Hile pale mkono ulikuwa kwenye natural position hakuna kubwa zaidi angeweza kufanya kuukwepa ule mpira kwa mtazamo wangu. Hakufanya maksudi.

5. Mpira Uligonga bega. Sheria mpya ya “T-shirt line rule” ni kwamba bega na mkono unatengenishwa na mwisho wa T-shirt.

6. Ni sahihi kadi nyekundu. Refa hakuona ubaya wa rafu akatoa kadi ya njano lakini waamuzi wa VAR Waliona ni rafu ya kadi nyekundu, ndio wakamuomba Refa aende kutizama hili afanye maamuzi sahihi.

7. Ni vigumu kujua kama kadi ya njano ilitokana na hilo tu au alimtukana refa.

Huo ni mtazamo wangu kwenye maswali yako, zaidi ya hapo ndio mpira makosa madogo madogo yapo. Vijana walijitahidi sana na walicheza vizuri kwa pamoja tujiendeleze tulipoishia.
 
Nazungumzia matukio manne
1.Picha za marudio zilionesha goli la Orlando lilikuwa clear offside
2.Matukio ya kunawa mpira yote mawili ilikuwa mkono Ulikuwa sehem sahihi kwa wakati sahihi na aliegusa hakufaidika na kugusa huko kwa Bahati mbaya.

3.Kagere alipigwa kiwiko refa akavunga Ile it's clear rescard

4.Hata penalty ya mkude kipa hakuwa kwenye eneo sahihi,ilitakiwa irudiwe
 
Dah analysis yako ime base sana kwa timu moja ile nyingne wao hawakudhulumiwa?
 
Tukio lililonishangaza ni Simba kufanya ule upuuzi katikati ya uwanja kabla ya game kuanza, kama uchawi unasaidia katika mpira, mbona Sumbawanga hawana timu ligi kuu.? Nani aliwadaganya uchawi unapanda ndege😀😀😀

 
Dah analysis yako ime base sana kwa timu moja ile ny
Ni kweli offside lakini kama mshika kibendera na VAR wote walikaa kimya ulitaka refa afanyaje wakati position yake uwanjani haikumuezesha kuona kama ni offside?

Huo ndio mizengwe haikosi tuangalie mbele.
 
kilicho nishangaza Zaidi ni kwanini simba hawakufungwa 5 na hali walizidiwa kila idara????
 
Duh
Hiki kiwango cha umbumbumbu kimepitiliza.
 

Wanaota moto, kule Sauzi baridi sana kipindi hiki 😂😂
 
Usikute hii ndio ilikuwa salama yao kudilute makafara ya Orlando, kumbuka huo ni uwanja wao Orlando wanafanya wanachotaka mkiingia kichwa kichwa 5 zinakuhusu.

Hivi ndio vitu nasisitiza sisi Yanga tujifunze kwa Simba, ndipo ilipo siri yao, tusiwabeze.
 
kwenye namba nne hapo nakukatalia ndugu. kipa alidaka akiwa kwenye eneo sahihi kabisaa. mguu wake wa kulia ulikuwa umegusa mstari wa goli muda ambao Mkude anapiga ile penati.
 
Jemedari tumekusoma
 
Mganga nasikia aliwadanganya mkichoma ubani pale katikati hakuna atakaye waona,hata camera.....nasikia mmempa kipigo mganga wenu kisa mmeonekana mnawanga katikati ya kiwanja.
 

Yote uliyoyaongea ni sahihi isipokuwa Namba 5.
Kwenye Namba 5 mpira uliomgonga Onyango Kuna Sheria ya Handball imebadilika nadhani hujapata update.
Mpira ukigusa kwenye Sleeve sikuhizi sio handball, Handball inaanza mwisho wa sleeve karibu n Kiwiko.
 
Yote uliyoyaongea ni sahihi isipokuwa Namba 5.
Kwenye Namba 5 mpira uliomgonga Onyango Kuna Sheria ya Handball imebadilika nadhani hujapata update.
Mpira ukigusa kwenye Sleeve sikuhizi sio handball, Handball inaanza mwisho wa sleeve karibu n Kiwiko.
Iweke hiyo Sheria hapa jukwaani kwa faida ya wote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…