Utata wa mpaka wa ziwa Nyasa: Google map wako sahihi kwa 100%, serikali ya Tanzania msipotoshe na kutisha watu

Moderate
Moderator ondoeni huu upuuzi kweny jf Kwa masilah mapana ya taifa letu ,,na huyu mbuzi agongwe burn!! Haiwezekan mtu kutoka huko sjui kuchanga chekundu ambapo hata elemu Hana na kisogo chake Chenye pasi aje aongee ujinga ,Hana hata ushahid alafu Uzi wake uachwe, lazma tuwe na wivu na taifa letu ,,, ukwel gani huyu kisogo bapa anajua kuhusu historia ya mpka wetu ??
 
Stupid and silly thinking,,Bora taifa likutoe kafara Kwa Majin wanted damu Yako tujenge hata daraja au calvat
 
Vyovyote iwavyo, usuruhishi au kesi, maamuzi yalikuwaje, au tulikubaliana nini kuhusu huo mpaka?

Nakumbuka Marehemu Membe alisema tulishinda, sasa sijui maamuzi ya hiyo arbitration yalikuwaje.

Unaweza kutuletea hapa?
Ukweli ni huu.
Hakuna kesi yoyote rasmi iliyofunguliwa na Tz kudai haki ya umiliki wa ziwa (Tz tulikurupuka kutaka kufungua kesi) na hivyo hakuna hukumu iliyotoka, kilichoendelea ilikuwa ni mazungumzo (to slow down the pressure between 2countries, to buy time, na kupiga pesa!).

Hizo blah blah za Membe achana nazo. Kwanini? Hukumu za kimataifa zikitoka huwekwa hadharani na dunia nzima itajua.
 
Wakati huo mpaka unawekwa, Tanzania na malawi yalikuq yote ni makoloni ya Britain, Hivyo hakuona kama kuna athari kama mpaka utakua katikati, pembeni au mwishoni.

Naamini, kama ingekua Mlawi na Tanzania wako chini ya makoloni tofauti pangeanza kuchimbika since then.
 
Bila shaka mtoa mada ana mafungamano na Zanzibar.
Sio mleta mada tu anayefungana na Zanzibar, hata Rais wa Tanzania (ambaye ndiye mwenye dhamana ya kumiliki rasimali zote za Tanganyika) naye ana mafungamano na Zanzibar kwa 100%.
Sasa amua mwenyewe, kunyoa au kusuka.
 
Maneno matupu hayavunji mfupa. Piga domo usiku utalala.
 
HUO MPAKA UMEWEKWA NA NANI?
 
Ukweli usemwe na sio kupotoshwa.
Ziwa Nyasa ni mali ya Malawi kisheria, Tanzania mpaka leo tunaendelea kudai haki ya kudhurumiwa kupata sehemu ya ziwa. Hicho ndio google map wamefanya.
SHERIA IPI?
 
Well said

Umenipunguzia kazi ya kuandika/kukoment
Ila inavyoonekana politicians huko Malawi wanaitumia vibaya hiyo kadhia kuwachota voters
Tz baada tu ya kumchapa Idd Amin, Wamalawi wakajua kituo kinachofuatia ni Malawi, wenyewe wakaanza kuomba poo
 
Ni kweli heligoland treaty inaipa Malawi umiliki wa hilo ziwa kwa 100%. Lkn Sisi watanzabia hatukubaliani na huo mkataba, na kamwe hatutakiwi kukubaliana no matter the cost.
 

Tena mipaka iliyowekwa na wapumbavu wakati sisi hatupo?
Sijui UN , Sijui Hegoland treaty to hell. Yale ya ZIWA VICTORIA na huku lazima yashughulikiwe.
 
Kwanini Malawi ndo wawe na umiliki asilimia 100 kwa upande wa Tanganyika tu na sio hadi mozambique?
 
Sisi tunashikilia ya UN kwamba endapo nchi ni majirani na wanashare water bodies hivyo inatakiwa mpaka uwe katikati na si vinginevyo..
Kweli,
Mantiki hapa ni kuwa jamii zote wanaopakana na ziwa kila upande (kila nchi) hulitumia kwa shughuli kadhaa za kiuchumi (livelihood) ikiwemo uvuvi, usafiri (mitumbwi, mashua, nk), umwagiliaji wa mazao ya kilimo, nk. Ukienda hata ziwa Tanganyika utakuta hivyo: upande wa Tanzania wananchi wanatumia ziwa, na upande wa DRC ni hivyo hivyo.

Haiwezekani ghafla tu uwaambie wananchi wa upande mmoja kuwa ziwa haliwahusu, ni la nchi nyingine wakati mababu zao vizazi vyote walilitumia miaka yote.
 
Matusi hapa JF hayarusiwi na wala hayana mchango wowote katika kujenga hoja au kujibu hoja.

Lakini kwa hekima na busara nitajibu baadhi ya hoja zako muhimu.

1. Kwanza hii mada unazungumzia usahihi wa google map katika kutoa habari zinazohusu mpaka wa Tz na Malawi kuhusu ziwa Nyasa, na wala sio uhalali wa mpaka kuwa wapi. Dunia nzima, kimataifa inafahamika rasmi mpaka wa Tz na Malawi uko pwani ya ziwa upande wa Tz, na hauko katikati ya Ziwa.

2. Uwepo wa sheria za kimataifa kuhusu mipaka baina ya nchi na nchi zinazopakana kwa maji (mpaka kuwa katikati ya ziwa) haufuti wala kuingilia mipaka ya kisheria iliyowekwa na kurithiwa na wakoloni. Mfano mzuri ni mipaka wa Ziwa Victoria (ambapo Tz, Kenya na Uganda hawajagawana ziwa sawa sawa, Tz akichukua sehemu kubwa zaidi), ziwa Tanganyika (ambapo Tz, DRC na Burundi hawajagawana sawa sawa). Kwanini? Mkoloni aliweka mipaka ya kisheria ambayo ndio tumeirithi. Hiyo sheria ya kimataifa ya kugawana nusu kwa nusu itatumika pale tu ambapo hakukuwa na mipaka rasmi ya kisheria.
 
Kwanini Malawi ndo wawe na umiliki asilimia 100 kwa upande wa Tanganyika tu na sio hadi mozambique?
Japokuwa ni nje ya mada, lakini nitakujibu.
Issue iko hivi, kihistoria, mkoloni aliipa Malawi 100% umiliki wa ziwa lote la Nyasa. Na baada ya uhuru kila nchi ikarithi hivyo. Mozambique wakakaa mezani na Malawi kuomba sehemu ya umiliki wa ziwa kwa kuwapa fidia ya eneo lingine la Mozambique. Kwa hiyo Mozambique 'alinunua' eneo la ziwa la Nyasa kutoka Malawi kwa gharama ya kutoa ardhi yake au kwa lugha nyingine Malawi 'alinunua' sehemu ya ardhi ya Mozambique kwa gharama ya kutoa yake ya umiliki ya sehemu ya ziwa Nyasa.
 
Duh hapo ndio naonaga muungano hauna tija..why uwepo? Faida zake ni za..kisiasa au kiuchumi au Kiusalama?
Muungano haujawahi kuwa na faida hata kwa sisi wazanzibar, ni kongwa la utumwa wa kitanganyika. Hatuutaki, hatuutaki hatuutaki kabisa!
Sasa kama watanganyika wamelala usingizi mzito wa nusu kaputi, unadhani wazanzibar watabakia kushangaa tu ndani ya muungano? Ni kujipakulia tu minyama ya kitanganyika.
 
Kwanini? Mkoloni aliweka mipaka ya kisheria ambayo ndio tumeirithi.
Usiseme mipaka ya KISHERIA.
Wale wezi na wanyang'anyi waliokaa kule Berlin 1884/5 na kugawana maeneo ya Afrika hawakuwa wanasheria na hawakutumia sheria yoyote. Walifanya uporaji. Sheria ingezingatiwa wenye ardhi zao (Waafrika) wangeshirikishwa kwa mujibu wa matakwa ya kisheria
 
Lengo la mada hii ni nini? Kwa kuwa ulitaka kudai pwani za Tanzania Bara ndiyo isababishe kuleta suala la ziwa Nyasa? Wewe ni mtanzania kweli? Umevuka mipaka
Lengo la mada hii ni kufuta ujinga na kuacha kukumbatia ujinga katika taifa letu. Ujinga haujawahi kuwaacha watu salama. Kukaririshwa ujinga mashuleni ndio kumeua elimu yetu na kuzaa wajinga wengi wenye vyeti.

Serikali ya Tz haina uwezo wa kubadilisha Global georgraphy&history. Utambulisho wa mipaka baina ya nchi na nchi ni mambo ya kimataifa, na sio utashi wa taifa moja moja. Google map huzingatia hayo katika kufanya location ya maeneo mbalimbali ikiwemo yenye migogoro.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…