Simba mundu
JF-Expert Member
- Feb 16, 2018
- 767
- 1,058
Moderate
Moderator ondoeni huu upuuzi kweny jf Kwa masilah mapana ya taifa letu ,,na huyu mbuzi agongwe burn!! Haiwezekan mtu kutoka huko sjui kuchanga chekundu ambapo hata elemu Hana na kisogo chake Chenye pasi aje aongee ujinga ,Hana hata ushahid alafu Uzi wake uachwe, lazma tuwe na wivu na taifa letu ,,, ukwel gani huyu kisogo bapa anajua kuhusu historia ya mpka wetu ??Serikali ya Tanzania imetoa tamko la marufuku ya kuzuia matumizi ya google map yenye kuonyesha mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye ziwa Nyasa ulipo kutumika kufundishia mashuleni. Kwenye ramani hiyo ya google inaonyesha mpaka wa kisheria uko pwani ya Ziwa Nyasa upande wa Tanzania na hapo hapo kuonyesha mpaka ambao Tanzania inadai ambao uko katikati ya Ziwa Nyasa. Kimsingi google map wako sahihi kwa 100%. Huo ndio ukweli ambao umekuwepo siku zote kabla hata ya kupata Uhuru na baada ya kupata uhuru.
Mpaka leo hii Tanzania tunadai kupata haki ya kumiliki karibu nusu ya Ziwa Nyasa lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa Malawi bado wana umiliki wa Ziwa Nyasa lote katika mpaka wake na Tanzania. Ni ukweli mchungu dhidi ya Tanzania na ukweli usio wa haki. Lakini ndio ukweli halisi. Tuna haki ya kudai ubadilishwe lakini hatuna haki ya kuupotosha.
Zama za kuwadanganya watu kielimu na kuwatisha wasijifunze kujua nini dunia inasema na kutambua (tofauti na vile walivyoaminishwa awali) kuhusu jeografia, historia na sayansi zimepitwa na wakati.