Utata wa mpaka wa ziwa Nyasa: Google map wako sahihi kwa 100%, serikali ya Tanzania msipotoshe na kutisha watu

Lengo la mada hii ni kufuta ujinga na kuacha kukumbatia ujinga katika taifa letu. Ujinga haujawahi kuwaacha watu salama. Kukaririshwa ujinga mashuleni ndio kumeua elimu yetu na kuzaa wajinga wengi wenye vyeti.
Niliwahi kumsikia Mheshimiwa David Cleopa Msuya akieleza kuwa (nitanukuu si neno kwa neno), wakati fulani tupo kwenye vita na Idd Amini wa Uganda, ndugu zetu wa Zanzibar kama raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nao walishiriki kumpiga Idd Amini. Sasa wakati ndugu zetu hawa wakati wanasafirishwa kutoka Dar es Salaam kwenda uwanja wa Vita, na ilikuwa mara yao ya kwanza kwenda maeneo ya Kagera, walipitishwa njia ya Arusha wakazungushwa na maeneo ya Musoma. Msuya anaongeza kusema kuwa walipofika maeneo ya Arusha wakamuuliza aliyekuwa anawaongoza kwenye gari kuwa wanakaribia kufika, Muulizwaji akawajibu ni kama tumefika nusu ...! Ndugu zetu wakaishiwa pozi...wakamweleza Muongozaji kuwa Tanzania ni kubwa sana kwa eneo, kwa hiyo hako kakipande alikochukua Idd Amin huku Kagera tumuachie maana eneo letu kubwa sana...!!!

Sasa hapo Tafakari ungekuwa muongozaji ungewazaje? Sitaki ndugu yangu ujipime juu ya mawazo yako kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi.
 
Nakuelewa vizuri.
 
Ukweli ni kwamba mipaka yote iliwekwa na wakoloni.
Na kanuni ya kugawana makoloni ilikuwa hivi-:
Ukiwa mpaka ni mto, Ziwa ama bahari basi mpaka ni Kati Kati ya mto au ziwa na si yo pwani ya ziwa.
Mf. Ziwa Tanganyika ni la Tz, DRC, Burundi, na Zambia hivyo ilivyo kwenye ziwa Victoria.
Malawi wangetaka kutupokonya ziwa basi wangeanzia Kyela
 
Ukweli usemwe na sio kupotoshwa.
Ziwa Nyasa ni mali ya Malawi kisheria, Tanzania mpaka leo tunaendelea kudai haki ya kudhurumiwa kupata sehemu ya ziwa. Hicho ndio google map wamefanya.
Sheria ipi hiyo ndugu? Tunaomba utusaidie kuiweka hapa ili hoja yako iwe na uzito na pia kuweka kumbukumbu vizuri.
 
Asante kwa ufafanuzi mkuu, kama hutojali naomba mfano mwingine wa kufanana na huu(nchi yenye mpaka wa mto ama ziwa na kuwa na umiliki wa asilimia 100) nipo kujifunza pia.
 
'Wezi' hao hao unaosema walikaa kule ulaya kutengeneza mipaka ya kihuni, ndio walitengeneza huu 'uhuni'

-Waliamua Tanzania bara kuchukua eneo la ardhi kubwa kuliko jumla ya eneo lote la Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia nk

-Walioamua mlima Kilimanjaro kuwa Tanzania bara na sio Kenya (Nenda katazame ramani uone jinsi ilivyopindishwa kimakusudi ili mlima Kilimanjaro uwe Tanzania bara na sio Kenya).

-Wakaamua Ziwa Victoria kwa sehemu kubwa limilikiwe na Tanzania bara

-Wakaona hiyo haitoshi wakaamua mbuga za serengeti, Ngorongoro, Manyara zote ziwe Tanzania.

Hakika hawa wahuni walikuwa na asili ya Tanganyika, maana sio kwa upendeleo huo wote. Wahuni oyeeeee!
 
Ukiwa mpaka ni mto, Ziwa ama bahari basi mpaka ni Kati Kati ya mto au ziwa na si yo pwani ya ziwa.
Unachosema siyo kweli. Hujui kwamba Tanzania tunamiliki sehemu kubwa ya ziwa Victoria, wakati Uganda wansmiliki sehemu ndogo, na Kenya sehemu ndogo zaidi?
 
Lina faida gani kiuchumi hadi ligombaniwe tuanzie hapo!au ndio mambo ya Prestige and glory
 
Mpaka leo hii Tanzania tunadai kupata haki ya kumiliki karibu nusu ya Ziwa Nyasa lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa Malawi bado wana umiliki wa Ziwa Nyasa lote katika mpaka wake na Tanzania.
Hii umeipata wapi mkuu 'Zanzibar ASP'
Kwamba "sheria
map yenye kuonyesha mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye ziwa Nyasa ulipo kutumika kufundishia mashuleni. Kwenye ramani hiyo ya google inaonyesha mpaka wa kisheria uko pwani ya Ziwa Nyasa
Kwa nini usiseme, au Google hiyo hiyo isiseme "mpaka unao daiwa na Malawi ulipo; na mpaka unaodaiwa na Tanzania ulipo"; huo wa "kisheria" ume upata wapi wewe?

Jambo la kukusikitikia wewe binafsi ni kutaka watoto wetu nao tuwafundishe tunaouona kuwa ni upotofu? Sasa wewe niambie matokeo yake yatakuwa vipi; na kwa nini tuendelee kudai mpaka wetu ulipo iwapo tayari tume waandaa watoto wetu, raia wa kesho wa nchi hii kukubali unayo yaita wewe "sheria"!
Hapa unataka tuwafundishe watoto wetu kuwa sisi, nchi yetu ya Tanzania ni wavunja sheria. Tutajenga taifa la namna gani katika hali hiyo!

Natambua tumevurugikiwa sana wakati huu kama taifa kutokana na hali yetu ya kisiasa ndani ya nchi yetu, lakini yanaokuja maswala kama haya; na wewe ujitokeze na mada ya kiajabu sana kama hii; inasikitisha sana.
 
Asante kwa ufafanuzi mkuu, kama hutojali naomba mfano mwingine wa kufanana na huu(nchi yenye mpaka wa mto ama ziwa na kuwa na umiliki wa asilimia 100) nipo kujifunza pia.
HUO MPAKA UMEWEKWA NA NANI?
Mpaka uliwekwa na wakoloni, na ndio mipaka hiyo hiyo tumeirithi karibu sehemu zote hapa Afrika.
Kabla ya mkoloni hakukuwa na nchi ya Tanganyika.
 
Sio mleta mada tu anayefungana na Zanzibar, hata Rais wa Tanzania (ambaye ndiye mwenye dhamana ya kumiliki rasimali zote za Tanganyika) naye ana mafungamano na Zanzibar kwa 100%.
Sasa amua mwenyewe, kunyoa au kusuka.
Usimlishe Samia Binti Ally Hassan Mwinyi, Mzaramo wa Nkuranga maurojo ya kiunguja.
 
Usichokielewa ni hiki, kushindwa kutofautisha kati ya Ukweli halisi na uhalali unaozaa umiliki. Mimi nimeandika ukweli uliopo, bila kuongeza hisia zangu au maoni yangu kuhusu uhalali unaozaa umiliki.
Na huo ndio watoto wetu wanapaswa kufundishwa mashuleni, tusifundishe watoto wetu uongo, ujanja ujanja na ujinga.

Google wamesema ukweli halisi uliopo na unaotambulika duniani kimataifa na kisheria.
Google map wameonyesha mpaka wa kimataifa wa ziwa Nyasa, na hapo hapo wakaweka mpaka ambao Tz tunautambua (mpaka wa mchongo)
 
Wewe hujawa mtu wa kwanza kulitambua hili swala. Limekuwepo hata kabla hujazaliwa; halafu uje kusema unao "ukweli" wewe wa kuwafundisha wanao historia unayo ijuwa wewe!
Wafundishe hao wanao, lakini waTanzania usiwapotoshe na jambo ambalo haliko katika uwezo wako binafsi.

Kama wewe unatambua "mchongo" hilo ni lako. Liache la waTanzania kama nchi libaki lilivyo.

Historia ya swala hili ipo wazi na ramani za hao wakoloni wa kijerumani wenyewe zipo na ni utata mtupu tokea huko; lakini wewe kwa sababu zako unataka "sheria" unayo itambua wewe!
 
Suala la mpaka kuwa katikati ya Ziwa hilo limeletwa na umoja wa mataifa baada ya ukoloni kutokomezwa.
Mkoloni alikuwa anaweka mipaka kwa maslahi na mapatano binafsi tu, na ingeweza kubadilika mara kwa mara kwa maafikiano, vita nk. Mkoloni hakuwa na general rule ya kutumika kwenye mipaka yote ya maji.

Mfano mzuri ni Ziwa Victoria ambapo mipaka iliwekwa na mkoloni ambapo......
Tanzania 49%
Uganda 45%
Kenya 6%

Ziwa Tanganyika
Tanzania 41%
DRC 45%
Burundi 8%
Zambia 6%
 
Hakuna mtu mwenye umiliki wa ukweli, ukweli ni mali ya watu wote, upo siku zote, na hauwezi kujificha.

Mada yangu hapa ni kukosoa uamuzi wa Tanzania kutaka kuzuia watoto wetu kujifunza na kuujua ukweli wa mpaka wa Ziwa Nyasa.

Narudia tena kuandika hapa, walichokiandika Google Map ndio ukweli uliokuwepo na ndio uliopo duniani kote.
 
Malawi wasichokoze moto , niko tiyari fia vitanani , kama nchi ,tunaweza ifuta Malawi kwenye uso wa dunini , hizi chokochoko za Malawi sio za leo ,ila wajue tz sio nchi nyepesi kivile , nimatumain yangu mzee Kikwete yupo anapita mafail maana hii kitu anaijua vizuri , sasa wajichanganye tu , kama vipi Malawi wanasema ni ziwa lao ,wasombe maji yote kwenda kwao vinginevyo mda ni mwalim
 
Hakuna mtu mwenye umiliki wa ukweli, ukweli ni mali ya watu wote, upo siku zote, na hauwezi kujificha.
Kama ilivyo kwa uongo; au siyo!

Mkuu 'Zanzibar ASP', niseme wazi hapa, leo unanishangaza pakubwa kweli juu ya swala hili la mpaka.
Kweli unataka sisi Tanzania tuwafundishe watoto mipaka ya nchi yao kwa kutumia taarifa za utata kama hizo za 'Google'?

Huo "ukweli' unao ung'ang'ania wewe, umeshushwa toka mbinguni, kwamba hakuna binaadam yeyote wa kuuhoji?
Kwani maswala haya ya utata wa mipaka baina ya mataifa , ni hili tu la Tanzania ndilo unalo ona wewe "ukweli" wote pasipo na shaka yoyote ; kiasi kwamba tuwaambie watoto wetu "ukweli" huo unao uona wewe?

Kama unatambua kuwa mpaka huo unalo tatizo; kwa nini ufundishe watoto bila hata ya kuzungumzia tatizo lililopo.
Wewe hujui kwamba hili swala liko kwenye usuluhishi/mazungumzo/taratibu za kulishughulikia hata kisheria..., ila unataka tu "ukweli" ufundishwe? Tanzania ikubali mipaka ya 'Google'!
Inashangaza sana.
 
Unaweza kuwa ulipata au kuiona hata copy ya makubaliano tuliyoafikiana?

Nakumbuka yule Rais mama alitushitaki tukaitikia wito, na ikiwa kulikuwa na makubaliano ya kujadiliana nje ya mahakama huwa yanaafikiwa na pande zote mbili husika, na baada ya maamuzi upande ambao haujaridhika unaweza kukataa na kujitoa kwenye makubaliano, na kuendelea na kesi mahakamani.

Kama hatukuafikiana, bila shaka Malawi waliendelea na kesi, na labda walishinda kimya kimya, ndio maana google hufanya wafanyavyo.

Kama sio hivyo labda serikali itatujulisha watanganyika, maana hili sio la chama cha ccm bali la watanganyika wote, maana ulinzi wa mipaka yetu ni jukumu letu wananchi.

Maamuzi haya yawekwe wazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…