TUJITEGEMEE
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 25,225
- 25,488
Niliwahi kumsikia Mheshimiwa David Cleopa Msuya akieleza kuwa (nitanukuu si neno kwa neno), wakati fulani tupo kwenye vita na Idd Amini wa Uganda, ndugu zetu wa Zanzibar kama raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nao walishiriki kumpiga Idd Amini. Sasa wakati ndugu zetu hawa wakati wanasafirishwa kutoka Dar es Salaam kwenda uwanja wa Vita, na ilikuwa mara yao ya kwanza kwenda maeneo ya Kagera, walipitishwa njia ya Arusha wakazungushwa na maeneo ya Musoma. Msuya anaongeza kusema kuwa walipofika maeneo ya Arusha wakamuuliza aliyekuwa anawaongoza kwenye gari kuwa wanakaribia kufika, Muulizwaji akawajibu ni kama tumefika nusu ...! Ndugu zetu wakaishiwa pozi...wakamweleza Muongozaji kuwa Tanzania ni kubwa sana kwa eneo, kwa hiyo hako kakipande alikochukua Idd Amin huku Kagera tumuachie maana eneo letu kubwa sana...!!!Lengo la mada hii ni kufuta ujinga na kuacha kukumbatia ujinga katika taifa letu. Ujinga haujawahi kuwaacha watu salama. Kukaririshwa ujinga mashuleni ndio kumeua elimu yetu na kuzaa wajinga wengi wenye vyeti.
Sasa hapo Tafakari ungekuwa muongozaji ungewazaje? Sitaki ndugu yangu ujipime juu ya mawazo yako kuhusu mpaka wa Tanzania na Malawi.