KWENYE PESA HAKUNA ADUI
JF-Expert Member
- Dec 16, 2014
- 225
- 349
UMEWAZA SANAMitanzania mingine bwana....wewe unatumia kiakili chako kilichofungwa kudraw conclusion ya jambo kubwa kama hili halafu cha ajabu unajiona upo sahihi. Tuelimikeni tuacheni kujifanya wajuaji. Tuwe open minded....
Open a discussion and learn from others. Tufike Mahali tujue athari ya maandiko tunayoandika bila kufanya kautafiti.....ni kweli upo entitled na maoni yako lakini unatakiwa ku-declare haya ni maoni binafsi.
Mkuu ningependa kujua kama serikali ya Tanzania imeshawasiliana na Google kuhusu utata ulioko kwenye mpaka wa Ziwa Nyasa na kuwataka wasiuonyeshe ulivyo. Aidha, kuna hatua zozote rasmi zinazoendelea kujadili suala hili kati ya wahusika wakuu (GTZ na GM) ikiwa ni pamoja na taasisi husika kimataifa?Sahihi kwa mjibu wa nini, vigezo gani? Wewe unakimbilia kusema "sheria", nani aliye weka hiyo sheria? Sasa unakimbilia kulaumu kuwa nachanganya mambo, wakati wewe mwenyewe huelewi maelezo unayo pewa?
Walicho takiwa kufanya Google,; mahali palipo na utata wa mpaka, ni aidha kutoonyesha alama ya mpaka kabisa, au kuweka mipaka miwili na kuonyesha mpaka unao daiwa na wahusika.
Hata hivyo, katika hili letu la mpaka na Malawi, ni sisi wenyewe (viongozi wetu) wanao stahili lawama, kwa kuruhusu Malawi kujitangazia mpaka ulipo. Malawi kafanya juhudi kubwa katika kufanya hivyo. Sisi tumeishia kupinga zaidi 'locally' bila ya
Hili ndilo ninalo kueleza hapa kwamba elimu yako uliyo pata huko ni ya kukariri, haikukupa uwezo wa kufikiri na kuona tofauti iliyopo katika maswala husika.
Ni wazi hili ni tatizo kwako. swala kwa uzito unao stahili.
Google wangesikia upande wetu, hizo ramani ulizo funzwa huko ulikokuwa 'brainwashed', wasinge thubutu kuweka ramani hizo na kupotosha swala zima.
Mipaka ya kikoloni hiyo ukimeet terms and conditions zao unaweza kua kama Israel.Serikali ya Tanzania imetoa tamko la marufuku ya kuzuia matumizi ya google map yenye kuonyesha mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye ziwa Nyasa ulipo kutumika kufundishia mashuleni. Kwenye ramani hiyo ya google inaonyesha mpaka wa kisheria uko pwani ya Ziwa Nyasa upande wa Tanzania na hapo hapo kuonyesha mpaka ambao Tanzania inadai ambao uko katikati ya Ziwa Nyasa. Kimsingi google map wako sahihi kwa 100%. Huo ndio ukweli ambao umekuwepo siku zote kabla hata ya kupata Uhuru na baada ya kupata uhuru.
Mpaka leo hii Tanzania tunadai kupata haki ya kumiliki karibu nusu ya Ziwa Nyasa lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa Malawi bado wana umiliki wa Ziwa Nyasa lote katika mpaka wake na Tanzania. Ni ukweli mchungu dhidi ya Tanzania na ukweli usio wa haki. Lakini ndio ukweli halisi. Tuna haki ya kudai ubadilishwe lakini hatuna haki ya kuupotosha.
Zama za kuwadanganya watu kielimu na kuwatisha wasijifunze kujua nini dunia inasema na kutambua (tofauti na vile walivyoaminishwa awali) kuhusu jeografia, historia na sayansi zimepitwa na wakati.
Mkuu mipaka ya kikoloni ndio iliyoidhinishwa na OAU kuwa mipaka halisi ya nchi zote za kiafrika zilizopata uhuru. Kumbuka pia ili kuipata ardhi kati ya makoloni ilikuwa ni kwa mapigano ya kivita. Anayeshinda ndiye anapata nchi au kwa makubaliano ya kuuziana.Mkuu ningependa kujua kama serikali ya Tanzania imeshawasiliana na Google kuhusu utata ulioko kwenye mpaka wa Ziwa Nyasa na kuwataka wasiuonyeshe ulivyo. Aidha, kuna hatua zozote rasmi zinazoendelea kujadili suala hili kati ya wahusika wakuu (GTZ na GM) ikiwa ni pamoja na taasisi husika kimataifa?
Huko nyuma, Nyerere alianza lakini akalipa uzito mdogo kwa vile hakukuwa na mgogoro. Kikwete pia alianza mazungumzo. Inaelekea hayakufika popote. Kwa vile maisha yanaendelea kawaida naona serikali haioni ulazima wa kusumbukia sana suala hilo.
Kisheria Google wako sahihi lakini huwa wanaweza kutilia maanani masuala ya kisiasa (penye utata) wakiwasilishiwa facts za msingi rasmi na kuweka footnote. Km wadau walivyosema wanaweza wasiweke mpaka wowote na kuweka majina yote mawili ya ziwa.
Google ni kampuni ya kiteknolojia sio ya kiutawala au kisiasa. Haimiliki taarifa. Inazionyesha tu. Inafanyia kazi facts rasmi zilizopo katika kutengeneza documents zao. Kama serikali haijawasiliana nao kuhusu hizo ramani na utata wa kihistoria katika hilo ziwa basi si vyema kuwajia juu kama vile wamefanya kosa.
Mkuu 'Drifter', mimi sijui, kwa sababu sipo huko serikalini; lakini ni wazi kabisa kuna uzembe mkubwa sana kwa wahusika huko serikalini kuhusu jambo hili. Wizara ya Mambo ya nje ni dhahiri haitimizi wajibu wake sawasawa kuhusu jambo hili.Mkuu ningependa kujua kama serikali ya Tanzania imeshawasiliana na Google kuhusu utata ulioko kwenye mpaka wa Ziwa Nyasa na kuwataka wasiuonyeshe ulivyo. Aidha, kuna hatua zozote rasmi zinazoendelea kujadili suala hili kati ya wahusika wakuu (GTZ na GM) ikiwa ni pamoja na taasisi husika kimataifa?
Hapana. Huko nyuma Kamuzu Banda alipo jaribu kulazimisha alionyeshwa wazi asithubutu kufanya hivyo. Kuna vimashua vyake vilizamishwa ziwani. Kwa hiyo halikuwa jambo dogo na wala halikupewa "uzito mdogo".Huko nyuma, Nyerere alianza lakini akalipa uzito mdogo kwa vile hakukuwa na mgogoro. Kikwete pia alianza mazungumzo. Inaelekea hayakufika popote. Kwa vile maisha yanaendelea kawaida naona serikali haioni ulazima wa kusumbukia sana suala hilo.
Mpaka HUO uliwekwa HIVYO na wakoloni baada ya mWALIMU Nyerere kuwaondoa wakoloni. Google earth hawako SAHIHI, NI wachonganishiSerikali ya Tanzania imetoa tamko la marufuku ya kuzuia matumizi ya google map yenye kuonyesha mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye ziwa Nyasa ulipo kutumika kufundishia mashuleni. Kwenye ramani hiyo ya google inaonyesha mpaka wa kisheria uko pwani ya Ziwa Nyasa upande wa Tanzania na hapo hapo kuonyesha mpaka ambao Tanzania inadai ambao uko katikati ya Ziwa Nyasa. Kimsingi google map wako sahihi kwa 100%. Huo ndio ukweli ambao umekuwepo siku zote kabla hata ya kupata Uhuru na baada ya kupata uhuru.
Mpaka leo hii Tanzania tunadai kupata haki ya kumiliki karibu nusu ya Ziwa Nyasa lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa Malawi bado wana umiliki wa Ziwa Nyasa lote katika mpaka wake na Tanzania. Ni ukweli mchungu dhidi ya Tanzania na ukweli usio wa haki. Lakini ndio ukweli halisi. Tuna haki ya kudai ubadilishwe lakini hatuna haki ya kuupotosha.
Zama za kuwadanganya watu kielimu na kuwatisha wasijifunze kujua nini dunia inasema na kutambua (tofauti na vile walivyoaminishwa awali) kuhusu jeografia, historia na sayansi zimepitwa na wakati.
Sawa. Lakini katika dunia ya leo si rahisi kuanzisha vita kugombea mipaka. Maazimio ya AU na UN yanatosha kuweka mambo sawa.Mkuu mipaka ya kikoloni ndio iliyoidhinishwa na OAU kuwa mipaka halisi ya nchi zote za kiafrika zilizopata uhuru. Kumbuka pia ili kuipata ardhi kati ya makoloni ilikuwa ni kwa mapigano ya kivita. Anayeshinda ndiye anapata nchi au kwa makubaliano ya kuuziana.
Wakoloni wa kiingeleza na wajerumani walipeana maeneo ziwa Nyasa lote likagawiwa kwa Malawi 1890. Huu mgawanyo wa mipaka ya majini umekuja baadaye. Kwa maana hiyo hata ukienda kwenye mahakama za kimataifa mshindi ni Malawi ndio wenye ziwa lao.
Kumbuka pia Nyerere mwenyewe alikiri kuwa mipaka ya kikoloni ilituathiri kwani mpaka wetu ni pwani ya ziwa Malawi, ukiingia kwenye maji ujue uko Malawi.
Mgogoro huu unahitaji kutatuliwa kidiplomasia aidha tuwape malawi eleo la pwani yetu au bandari ya Mtwara ili tupate access ya ziwa Malawi au tuanzishe command ya jeshi la wanamaji liwe eneo la kijeshi tayari kwa vita
Mkuu sio rahisi kutatua mgogoro huu kwa kupitia channels za UN wala AU kwa sababu maamuzi ya kikoloni yalifanyika kibabe hata kabla ya hiyo UN au AU zamani OAU. Njia pekee inayoweza kutumika ni kwa nchi hizi mbili kukubaliana kuachana na mikataba ya kikoloni na kukubali kumiliki ziwa kwa pamoja au kuuziana kwa kubadilishana mali kwa mali.Sawa. Lakini katika dunia ya leo si rahisi kuanzisha vita kugombea mipaka. Maazimio ya AU na UN yanatosha kuweka mambo sawa.
Hata Malawi wanajua ule mpaka wa enzi za wakoloni hauna uhalisia. Ndio maana wametulia na kuacha ziwa litumike upande wa Tanzania.
Kinachotakiwa ni kwa serikali yetu kuweka msimamo kuhusu eneo letu halali la ziwa na kuwasilisha nia ya majadiliano na Malawi. Period.
Kuhusu Google ni juu ya serikali kuwasilisha hoja kuhusu utata uliopo na kukubaliana namna ya kufanya marekebisho kwenye machapisho yao bila kuathiri facts zilizoko.
South Sudan ilikuwepo katika mipaka ya Uhuru wa Sudan.Unajua kwamba OAU walikubaliana kuwa mipaka ya kikoloni ndio iendelee kutumika baada ya uhuru?
Yani unataka kusema kwamba nchi za Afrika tuna busara sana kwahiyo tuanze kuchora upya mipaka. Unazijua akili za Mwafrika kweli mkuu?
Yani turudie kuchora, Uganda wapendekeze kupata Kagera salient, Kenya wapendekeze kupata mlima Kilimanjaro pale ambapo ramani ilipindishwa ili mlima uwe Tanzania, Zanzibar wadai pwani ya bara maana kuna Sultan aliwahi sema anaimiliki na akiwapa Wajerumani sijui, Tanzania tudai sehemu ya Masai Mara ya Kenya ili Wamasai wote wawe Tanzania, Kenya wapendekeze waongezewe sehemu ya ziwa Victoria wawe nayo nyingi maana Tanzania imechukua kipande kikubwa zaidi, Burundi nao waombe sehemu kubwa zaidi ya ziwa Tanganyika. Hapo ni sisi tu, bado sehemu nyingine za Afrika.
Kiuhalisia ukisoma Helligoland treaty na mkataba mwingine, hakuna ushahidi unaoonyesha Tanzania tunamiliki nusu ya ziwa Nyasa. Hata Wajerumani waliokuwa wanatawaka Tanganyika ramani yao inaonyesha Nyasa nzima ni ya Malawi.
Sisi Tanzania tunakuwa na claim kuwa wazungu walikubaliana kama kuna chanzo cha maji mpakani basi kigawanywe kila nchi inayopakana ipate kiasi chake. But that wasn't the case kwa ziwa Nyasa. Tukienda mahakama ya usuluhishi, zikaletwa mikataba na mashahidi wakoloni Tanzania tunashindwa asubuhi na mapema kabisa.
Nimemaliza.Someni hili andiko la kiuanazuoni halafu tulijadili.
"Oil Under Troubled Waters: Some Legal Aspect of the Boundary Dispute Between Malawi and Tanzania"
Wewe google imekuja lini na Ziwa lilikuwepo tangu lini? Ina maana watu wakipindi hiko chote walikuwa hawajui?Ukweli usemwe na sio kupotoshwa.
Ziwa Nyasa ni mali ya Malawi kisheria, Tanzania mpaka leo tunaendelea kudai haki ya kudhurumiwa kupata sehemu ya ziwa. Hicho ndio google map wamefanya.
Kwa sababy hujui sheria za kimataifa kuhusu mipaka ya majini. Kwa mfano kina cha ziwa kikipunguka mpaka utakuwa wapi.Ni kweli kwenye heligoland treaty muingereza alitumia influence yake kupata ziwa upande wa Tanganyika na kwa sababu inasemekana mjerumani hakuwa na interest kwenye water bodies. Wala hakujali ndio maana pande zote zingine kama msumbiji walipewa haki za mipaka yao
Ubaya zaidi tanganyika na malawi zilikuja kusimamiwa na muingereza kwa muda mrefu zaidi. Kwa hiyo kusingekuwa na njia ya yeye kugawa hilo eneo
Ila ukifuatilia vigezo vilivyotumika Berlin kugawa maeneo, natural geographical bodies kama maziwa, milima na mito ndivyo vilitumika kupima mipaka. Ukianzia ziwa Victoria, tanganyika hadi mto kagera.. Hiyo ndio ilikuwa criteria ya ugawsji Ila neglection ya mjerumani kutojali maziwa ndio ilisababisha yote hayo
Na ndio maana sheria ya mipaka hadi leo bado inatambua hizi geographical structures kama mpaka sahihi.. Kingine ukisema malawi wamiliki ziwa lote, utakuwa na assurance gani kwamba hawatokuja kudai na pwani
Shida ni hiyo mkuu neglection ya mjerumani na muingereza kutofuata vigezo vya ugawaji mipaka ndio chanzo cha yote
Nyasaland ni Malawi between 1907 - 1964 wakati wa utawala wa Muingereza, kama kuna makubaliano yalikaa kuset upya labda yalifanyika baadae....Ziwa ni lao, thats naked truthWeka hapa Source ya huo 'ukweli' wako.
Au unataka tukuamini wewe broo..!
Ukoloni hakuna tena, hivyo bado maamuzi tunayo.Mpaka uliwekwa na wakoloni, na ndio mipaka hiyo hiyo tumeirithi karibu sehemu zote hapa Afrika.
Kabla ya mkoloni hakukuwa na nchi ya Tanganyika.
TruthUkoloni hakuna tena, hivyo bado maamuzi tunayo.
Wasione tupo kimya wakahisi wanatumuduWana utani sio kidogo mazee ile Isongole yote wanasema yao pamoja na huku kwa kina Nyoni..
Kuzichapa huwa ni option ya mwisho, na Ina madhara makubwa sanaNi suluhisho.
Maana yake atakaeibuka mshindi ndo atalimiliki ziwa 100% kuliko hii Kila mtu anasema yake
Huna akili mkuu. Toka lini water bodies ikawa ya upande mmoja yote..? Wewe mmalawi dawa tukujue na tukupeleke mahakamani.Serikali ya Tanzania imetoa tamko la marufuku ya kuzuia matumizi ya google map yenye kuonyesha mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye ziwa Nyasa ulipo kutumika kufundishia mashuleni. Kwenye ramani hiyo ya google inaonyesha mpaka wa kisheria uko pwani ya Ziwa Nyasa upande wa Tanzania na hapo hapo kuonyesha mpaka ambao Tanzania inadai ambao uko katikati ya Ziwa Nyasa. Kimsingi google map wako sahihi kwa 100%. Huo ndio ukweli ambao umekuwepo siku zote kabla hata ya kupata Uhuru na baada ya kupata uhuru.
Mpaka leo hii Tanzania tunadai kupata haki ya kumiliki karibu nusu ya Ziwa Nyasa lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa Malawi bado wana umiliki wa Ziwa Nyasa lote katika mpaka wake na Tanzania. Ni ukweli mchungu dhidi ya Tanzania na ukweli usio wa haki. Lakini ndio ukweli halisi. Tuna haki ya kudai ubadilishwe lakini hatuna haki ya kuupotosha.
Zama za kuwadanganya watu kielimu na kuwatisha wasijifunze kujua nini dunia inasema na kutambua (tofauti na vile walivyoaminishwa awali) kuhusu jeografia, historia na sayansi zimepitwa na wakati.
Hapo sikuungi mkono kipindi kile tunataka kupigana watu tulikuwa tunajamba jamba unadhani tulikomalia kisicho halali we we inatakiwa mamlaka ikuchunguzeSerikali ya Tanzania imetoa tamko la marufuku ya kuzuia matumizi ya google map yenye kuonyesha mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye ziwa Nyasa ulipo kutumika kufundishia mashuleni. Kwenye ramani hiyo ya google inaonyesha mpaka wa kisheria uko pwani ya Ziwa Nyasa upande wa Tanzania na hapo hapo kuonyesha mpaka ambao Tanzania inadai ambao uko katikati ya Ziwa Nyasa. Kimsingi google map wako sahihi kwa 100%. Huo ndio ukweli ambao umekuwepo siku zote kabla hata ya kupata Uhuru na baada ya kupata uhuru.
Mpaka leo hii Tanzania tunadai kupata haki ya kumiliki karibu nusu ya Ziwa Nyasa lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa Malawi bado wana umiliki wa Ziwa Nyasa lote katika mpaka wake na Tanzania. Ni ukweli mchungu dhidi ya Tanzania na ukweli usio wa haki. Lakini ndio ukweli halisi. Tuna haki ya kudai ubadilishwe lakini hatuna haki ya kuupotosha.
Zama za kuwadanganya watu kielimu na kuwatisha wasijifunze kujua nini dunia inasema na kutambua (tofauti na vile walivyoaminishwa awali) kuhusu jeografia, historia na sayansi zimepitwa na wakati.