Utata wa mpaka wa ziwa Nyasa: Google map wako sahihi kwa 100%, serikali ya Tanzania msipotoshe na kutisha watu

Utata wa mpaka wa ziwa Nyasa: Google map wako sahihi kwa 100%, serikali ya Tanzania msipotoshe na kutisha watu

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
11,550
Reaction score
40,697
Serikali ya Tanzania imetoa tamko la marufuku ya kuzuia matumizi ya google map yenye kuonyesha mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye ziwa Nyasa ulipo kutumika kufundishia mashuleni. Kwenye ramani hiyo ya google inaonyesha mpaka wa kisheria uko pwani ya Ziwa Nyasa upande wa Tanzania na hapo hapo kuonyesha mpaka ambao Tanzania inadai ambao uko katikati ya Ziwa Nyasa. Kimsingi google map wako sahihi kwa 100%. Huo ndio ukweli ambao umekuwepo siku zote kabla hata ya kupata Uhuru na baada ya kupata uhuru.

Mpaka leo hii Tanzania tunadai kupata haki ya kumiliki karibu nusu ya Ziwa Nyasa lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa Malawi bado wana umiliki wa Ziwa Nyasa lote katika mpaka wake na Tanzania. Ni ukweli mchungu dhidi ya Tanzania na ukweli usio wa haki. Lakini ndio ukweli halisi. Tuna haki ya kudai ubadilishwe lakini hatuna haki ya kuupotosha.

Zama za kuwadanganya watu kielimu na kuwatisha wasijifunze kujua nini dunia inasema na kutambua (tofauti na vile walivyoaminishwa awali) kuhusu jeografia, historia na sayansi zimepitwa na wakati.
IMG-20241223-WA0006.jpg
 
Hili jambo litaleta shida huko mbeleni. JPM angekuwa mtu sahihi wa kulimaliza.
Mtu sahihi alikuwa Nyerere (kwa sababu alikuwa na ushawishi), na labda Kikwete (alikuwa ni mwanadiplomasia mzuri), tofauti na hapo tupate rais mwenye kujua sheria za kimataifa vizuri (hapa nadhani Lissu atatufaa zaidi). Magufuli angeishia kutumia nguvu (jeshi), Ziwa tungelipata lakini tungeshindwa kulitumia, lingeishia kuwa kambi ya wanajeshi wa majini.
 
Serikali ya Tanzania imetoa tamko la marufuku ya kuzuia matumizi ya google map yenye kuonyesha mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye ziwa Nyasa ulipo kutumika kufundishia mashuleni. Kwenye ramani hiyo ya google inaonyesha mpaka wa kisheria uko pwani ya Ziwa Nyasa upande wa Tanzania na hapo hapo kuonyesha mpaka ambao Tanzania inadai ambao uko katikati ya Ziwa Nyasa. Kimsingi google map wako sahihi kwa 100%. Huo ndio ukweli ambao umekuwepo siku zote kabla hata ya kupata Uhuru na baada ya kupata uhuru.

Mpaka leo hii Tanzania tunadai kupata haki ya kumiliki karibu nusu ya Ziwa Nyasa lakini hiyo haiondoi ukweli kuwa Malawi bado wana umiliki wa Ziwa Nyasa lote katika mpaka wake na Tanzania. Ni ukweli mchungu dhidi ya Tanzania na ukweli usio wa haki. Lakini ndio ukweli halisi. Tuna haki ya kudai ubadilishwe lakini hatuna haki ya kuupotosha.

Zama za kuwadanganya watu kielimu na kuwatisha wasijifunze kujua nini dunia inasema na kutambua (tofauti na vile walivyoaminishwa awali) kuhusu jeografia, historia na sayansi zimepitwa na wakati.
Umeshiba makande wewe. Kama kuna siku niliwahi kumuelewa Mzee Jakaya ni siku alipoelezea historia ya huu mgogoro. Lazima tuwafundishe watoto wetu, kwani sababu mzito za kihistoria na za kisasa zipo kwanini mpaka uwe katikati. Yaani Google map ikisema Mt.Kilimanjaro ipo Kenya na sisi tuufyate siyo?
 
Mitanzania mingine bwana....wewe unatumia kiakili chako kilichofungwa kudraw conclusion ya jambo kubwa kama hili halafu cha ajabu unajiona upo sahihi. Tuelimikeni tuacheni kujifanya wajuaji. Tuwe open minded....

Open a discussion and learn from others. Tufike Mahali tujue athari ya maandiko tunayoandika bila kufanya kautafiti.....ni kweli upo entitled na maoni yako lakini unatakiwa ku-declare haya ni maoni binafsi.
 
Weka hapa Source ya huo 'ukweli' wako.

Au unataka tukuamini wewe broo..!
Mipaka yote ya bara la Afrika iliwekwa na wakoloni, na hiyo ndio tuliweza kurithi baada ya uhuru na sheria za UN zinatamka wazi, mipaka ya kikoloni ya kisheria ndio mipaka rasmi baada ya uhuru. Mpaka wa kikoloni unatamka wazi kuwa Ziwa Nyasa lote ni mali ya Malawi japokuwa lilikuwa linapakana na nchi tatu (Malawi, Tanzania, Msumbiji), leo hii Msumbiji ana umiliki pia wa sehemu ya ziwa Nyasa baada ya kuridhiana na Malawi kumpa sehemu ya ardhi yake yenye milima ili yeye (Msumbiji) apate sehemu ya ziwa hivyo mpaka wa Malawi na Msumbiji ukabadilishwa kisheria. Tanzania tumekataa kuridhiana na Malawi ili nasi tupate sehemu ya ziwa kisheria.

Hoja ya Tanzania ni moja tu, mkataba wa kikoloni ulioipa Malawi umiliki wote wa Ziwa haukuwa wa haki, hivyo haupaswi kurithiwa, upigwe chini. Hayo sasa ndio mambo ya kisheria, siku moja tutajadili upya hapa JF japokuwa ilishajadiliwa sana humu.
 
Wote tuna haki kwa maana ziwa liko pande zote mbili
Ndugu umetaza ramani vizuri?
Ziwa linapakana na nchi tatu, sio nchi mbili. Kuna Malawi, Tanzania na Msumbiji.
Kwanini mpaka wa zamani ulionyesha Msumbiji hana umiliki wa ziwa lakini leo ana umiliki wa ziwa? Jibu ni kuwa ilibidi Msumbiji aombe umiliki wa ziwa kwa kumpa Malawi sehemu nyingine ya ardhi yake.
 
Mitanzania mingine bwana....wewe unatumia kiakili chako kilichofungwa kudraw conclusion ya jambo kubwa kama hili halafu cha ajabu unajiona upo sahihi. Tuelimikeni tuacheni kujifanya wajuaji. Tuwe open minded....

Open a discussion and learn from others. Tufike Mahali tujue athari ya maandiko tunayoandika bila kufanya kautafiti.....ni kweli upo entitled na maoni yako lakini unatakiwa ku-declare haya ni maoni binafsi.
Wewe uliyefanya utafiti njoo hapa na uchambuzi wako, hakuna aliyekukataza. Huna hoja basi ishia kusoma hoja za wengine.
 
Back
Top Bottom