Sisi na vyama vyote tusimfuate Msajili ambaye amepitiliza katika uoga wake wa nguvu ya CHADEMA na ACT. Jambo liko wazi. Sheria ilitungwa ili iratibu Muungano wa vyama, siyo kuzuia bali kuratibu. Muungano ni kitu kikubwa kwa sababu ama uhai wote au sehemu ya uhai wa mwanzo wa vyama vinavyoungana huondolewa, na uhai mpya hutengenezwa. Huo unahitaji kuelezewa haki na wajibu wake. Ndiyo sababu unahitaji sheria (regulation). Ushirikiano ni jambo tofauti, rahisi na la kila siku.
Halitengenezi uhai mpya au kuondoa wa zamani kwa namna yoyote. Hufanyika muda wote kwa hiari na namna mbalimbali. Hauhitaji makubaliano ya kimaandishi. Hauzuiliki wala kushitakika. Kuutungia sheria ni kichekesho. Wote tumekuwa tukijua kuwa, kwa vile vyama HAVIKUUNGANA katika muda wa kisheria, VITASHIRIKIANA tu vikipenda.
Ndivyo wanavyofanya. TLP na CCM walikuwa sahihi na Msajili alijua hivyo, ndiyo sababu alinyamaza. Ni ushabiki na uoga wake tu ndio uliomfanya kujaribu kukataza jambo hili - pale vyama asivyovitaka navyo vilipoonyesha ushirikiano. Tuendelee. Ushirikiano hoyee!