Utata wa picha za anga na kutoonekana kwa nyota

Utata wa picha za anga na kutoonekana kwa nyota

Kuna kitu kinaitwa exposure, nyota zinaoenekana sana kwenye space ila camera inapopiga kitu chenye ku-reflect mwanga inafanya exposure area kuwa ndogo na ule unaoreflect unafanya mwanga wa nyota kuwa dim, kwa mfano chukulia unaangalia mwezi ukiwa mkubwa na unatoa mwanga mwingi utagundua nyota chache zonazoonekana.
 
Unajua kwangu mimi hakuna watu waongo kama wazungu.Mimi tangu walipotuigizia suala la mtu kwenda mwezini,nikawa nimekata mzizi wa fitina ya kuwa KAMWE SITAAMINI HABARI ZA ANGA NA SAYARI.Kwahiyo kila ninapo ona habari hizi na mfano wake naona kama ni stori na masimulizi ya pauka pakawa...
 
Katika lile igizo lao la mtu kwenda mwezini,wapo waliohoji kwanii hazikuonekana nyota katika ile picha ya mtu akiwa mwezini.Kwa kujitutumua kwao wakasema huwezi kuziona nyota sababu mwezini hakuna hewa na mwezini si kama duniani,wakamithilisha na mfano wa sauti isivyoweza kutembea katika vacuum space yaani mwezini sababu hakuna hewa kumekuwa kama vacuum space.

Unajua watu hawa inabidi wafikie muda wakubali ukweli mama ya kuwa kuna vitu ambavyo viko ndani ya uwezo wetu na vile ambavyo viko nje ya uwezo wetu.Na visivyowezekana wakubali kwamba haviwezekani sio kutuletea mapicha ya ubunifu bunifu tu na uongo wa tabaka la chini.
 
lakini mkuu, wanasayansi wanasema nyota zinaonekana vizuri sana kwenye kwa sababu hakuna atmosphere na ndo maana zikatumwa space telescopes, sasa iweje unasema kwa sababu hakuna atmosphere ndio maana picha hazionyeshi nyota?, chukulia mfano wa hii picha
View attachment 477251
hili ni jibu toka kwa mwanaanga
Hivi kaka,unaweza kunithibitishia kwamba picha hiyo kweli imepigwa na hicho kifaa ?
 
Nyota zipo mbali sana,huwezi kuziona kama kuna mwanga
 
Hivi kaka,unaweza kunithibitishia kwamba picha hiyo kweli imepigwa na hicho kifaa ?
Huwa najiuliza huwa wanakuwa katika position gani kuweza kupiga hizo picha, eti wanapiga picha ulimwengu mzima sayari zote zinaonekana kweli?
 
Ukitazama vizuri 'background' ya picha nyingi ni nyeusi. Ingewezekanaje nyota ina/zinazong'aa zisionekane kwenye hilo kiza?
 
Huwa najiuliza huwa wanakuwa katika position gani kuweza kupiga hizo picha, eti wanapiga picha ulimwengu mzima sayari zote zinaonekana kweli?
Google hilo swali lako na utajibiwa vizuri zaidi na wataalam! It's fascinating indeed,
 
Akili ya mwanadamu babu kubwa walahi!
 
Hii picha ilipigwa na satellite inayozunguka mwezi, hapo jua lilikuwa kali sana mwezini hivyo mwanga ulikuwa mwingi. Kumbuka mwezini hakuna atmosphere wala mawingu. Kwa mwanga huo huwezi kuona nyota kirahisi. Ni kama hapa duniani, huwezi ona nyota mchana kirahisi.
Hjafafanua vizuri mkuu ongeza marifa na elimu uliopata ya geografia ili tufaidike tunasubiri
 
Nyota zipo mbali sana,huwezi kuziona kama kuna mwanga
Mkuu hapa umetuuza, wanasayansi wanasema zinaonekana nyingi na kwa wepesi ukiwa kwenye space sasa ww unatuambia umbali, unajio kuna radio telescope mwenyewe wanazodai unaweza kuona galaxy ya mbali zaidi.
 
Back
Top Bottom