Utata wa vifo vya Tupac na B.I.G

Utata wa vifo vya Tupac na B.I.G

sosssy

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2017
Posts
668
Reaction score
537
Hii ni makala inayohusu malejendari wa muziki wa hiphop duniani ambao mpaka leo hii wanaheshimika na kuenziwa duniani kote na wapenzi wa muziki kutokana na kutendea haki tasnia ya muziki wa kufoka [kuchana]. Ukimuongelea TUPAC SHAKUR basi unaongelea kioo cha upande wa magharibi na ndo hivyo hivyo ukimuongelea B.I.G basi unaongelea kioo cha upande wa mashariki, hizi ni pande mbili walizotoka na kuziwakilisha hawa malejendari wa muziki.

Ndiyo kila mtu anajua kuwa wawili hawa walikuwa mahasimu sana na hata ilipokuja kufikwa kwa umauti wao hawa malejendari kulizuka mambo mengi kwa wengi kuamini kuwa uhasama wao ndo uliopelekea vifo vyao ila kuna mambo mengi yapo nyuma ya pazia tunatakiwa kuyajua kwa undani ikiwezekana.

Katika hii makala tutaangalia maisha yao wote wawili, utata wa vifo vyao [mauaji yao] ngazi kwa ngazi mpaka tuone mambo yanayofichwa kuhusu mauaji yao.

Tutaangalia nadharia tofauti tofauti kuhusu mauaji yao na kikubwa kilichonisukuma kuandaa makala hii ni uhusika wa taasisi za usalama MAREKANI yani naongelea FBI na CIA kuwa nyuma ya mauaji haya.

Wakati tutakapokuwa tumefikia kuona nadaharia ya FBI na CIA kuhusika na mauaji ya hawa wawili utagundua kitu na hii nadharia tutaiangalia kwa undani ili isionekane tunawasingizia.

Hapo ndipo utakapoamini kuwa CIA na FBI ni wauaji wa daraja la kwanza na ndo taasisi hatari sana inapofika kwenye suala la kuua kwa kuhakikisha wanapumbaza watu wasiwaone wao ni wahusika, kuna michezo michafu mingi imetendeka mpaka mauaji ya hawa malejendari yanawakuta. Nafikiri ni kusubiri tu makala ituchambulie kwa kina pamoaja na shahidi zake kuhusu utata wa mauaji ya hawa wazee wa kufoka.
IMG_5228.JPG
 
Mbona umetuacha chalinze sasa
 
PAC hajafa au hakufa siku ile why!!?
Ile siku anaenda kuperform club baada ya pambano la tyson kwanini alikataza dem wake na dada yake wasiende akakomaa kua wabaki hotelini??? Madaktari waliihakikishia familia kua lazima PAC atapona ukizingatia alishawahi kula shaba tano from close range na akapona... Why rim za gari iliyokua inafanyiwa investigation zilikua tofauti na gari ambalo alikua anaenda nalo club (bmw)? Why waandishi wa habari hawakuruhusiwa kwenda hospitali siku ya tukio? Why album yake ya mwisho ikitwa MAKAVELI (MAKAVELI ukiipangilia unapata neno "IM ALIVE") na sio TUPAC?
 
MAKAVELI THE DON KILUMINATI.
mashairi mengi ukiskiliza unaweza kupata uchizi.huyu jamaa ni aina ya watu wachache majiniaz wanaochezea akili zetu km za midoli
 
Back
Top Bottom