Utatu wa G Records: Kazi za Roy Bukuku, G2 na KGT katika studio ya G Records

Utatu wa G Records: Kazi za Roy Bukuku, G2 na KGT katika studio ya G Records

Bizzman_ ametoroshwa nae alikua producer soundcraftars.......
Bizzman nasikia alikuwa mkali wa kuarrrange strings alikuwa naitwa studio hata na akina majani kutupia strings kwenye mangoma.
Nimemkumbuka pia producer complex RIP na ngoma za AY za mwanzo kama raha tu na changa la macho.
 
Bizzman nasikia alikuwa mkali wa kuarrrange strings alikuwa naitwa studio hata na akina majani kutupia strings kwenye mangoma.
Nimemkumbuka pia producer complex RIP na ngoma za AY za mwanzo kama raha tu na changa la macho.
Siku zinaenda aiseee....
 
Siku zinaenda aiseee....
Sana mkuu. Hivi Snalee yukl wapi. Hivi ile ngoma ya Snalee na Blu aliitengeneza Roy? Lile chupa la Adam Juma niliona ni level za mbele maana watu wote snalee na blu
 
Roy alikuwa noma sana huyu jamaa umemaliza yote.
Hivi KGT bado anafanya production? Maana jamaa kagonga ngoma kibao kubwa lakini hata sura yake siijui.
Na si kuna kipindi roy alijiondoa akaanzisha studio yake ya G2?
Nasikia sina hakika utanisahihisha, akina bob manecky wamepita mikononi mwa roy. Maana ukisikiliza ngoma kama neira, asia na ngoma za mwanzo za manecky kama vile alikuwa anapita kwenye midundo ya roy na mabass kama yote.
LGT huyu hapa, msikilize. Jamaa anavyoongea na kujibu maswali tu inaonyesha yupo smart and well composed
 
Sana mkuu. Hivi Snalee yukl wapi. Hivi ile ngoma ya Snalee na Blu aliitengeneza Roy? Lile chupa la Adam Juma niliona ni level za mbele maana watu wote snalee na blu
Dah hii ngoma ilikua balaa
 
Afu KGT beat zake nyingi zilikuwa zinafanana alikua anajisample mwenyewe
 
UTATU WA G RECORDS

DJ Gulu Ramadhan Nnanji " G LOVER" alifungua studio yake, G RECORDS na kumpatia mikoba yote ya production, Roy Bukuku.

Kazi nyingi zilipikwa pale huku utambulisho wa kazi alizozitengeneza Roy ukiwa ni uzito wa midundo yake.

Mara kukawa na G2 (G mbili au G Square), kisha akaibuka KGT na baadaye, Roy akafariki na kubadili taswira nzima ya G RECORDS.

Nazileta kazi 20 zilizopikwa na "wamba" hawa wawili kutoka nyumba kubwa, G RECORDS
NGOMA KUMI ZA ROY
1. HAWAPENDI - JOH MAKINI
2. ICE CREAM- NOORAH FT SUMA LEE
3. USIKU HUU - DAZ BABA FT BLUE
4. CHUNGWA - SUMA LEE
5. MAPOZI - MR BLUE
6. SAFARI NI NDEFU - BWANA MISOSI FT SUMA LEE
7. USITOE - BIG MAN IZ FT ENIKAH
8. NIMEKUBAMBA - ENIKAH
9. SIAMINI - MATONYA
10. DAKIKA MOJA - NGWEA FT NOORAH
NGOMA KUMI ZA KGT
1. NIACHE NITEMBEE - BABY J FT CHID BENZ
2. HASIRA ZA NINI - CHID BENZ FT ALI KIBA
3. CINDERELLA - ALI KIBA
4. NI SOO - PASHA
5. NIDANGANYE - SHETTA FT DIAMOND
6. MAPENZI MATAMU - HAKEEM 5
7. MOYO - ABBY SKILLS FT KIBA
8. I'M IN LOVE - ALI COM FT KGT
9. ABIRIA CHUNGA MZIGO WAKO - MATONYA FT BLUE
10. ANASOMA - PICO FT FA

Roy ndiye aliyemtoa Blue. Baada ya kifo chake, Blue alipata shida sana maana alikiri kuwa Roy alimuwezea sana na baada ya kutuliza akili sana, akaona akomae na Man Walter, Sei na Dunga kwa kiasi kikubwa.
Roy alifanya kazi nyingi za Suma Lee, Abby Skills, na Mr Blue.

20% anasimulia kuwa kipindi analibishia hodi game hili aliibuka kwa Roy mpaka akachoka.

Siku moja Blue akagonga na kuwaacha akina 20 wakiwa WAMEKAA benchi. Roy akiwa ndani akauliza, nani anagonga, Blue akajibu, "Blue hapa" Roy akamwambia apite.

Siku ya pili, 20 akaona usintanie, akagonga na Roy alipouliza nani?? 20 akajibu "Blue hapa" Roy akaruhusu aingie, wakatoana nishai huko ndani.
Baada ya Wameiba pombe na Vijimambo kufanya vizuri, Roy akamchek Noorah na kumwambia kama ana ngoma nyingine aibuke watoe kitu, Noorah akafunua daftari lake la mistari na kwenda na vocals zote mpaka chorus lakini Roy akaivua Ile chorus na kumpa msanii wake afanye maunyama, ndiyo namwongelea Ismail "Suma Lee"

Roy aliacha pigo kubwa kwa WAPENDA MUZIKI lakini pia kwa mdogo wake wa damu aliyefanya naye kazi nyingi aitwaye ENIKAH.

Gulu aliwahi kulalamikiwa kuwa aliwapendelea Wazanzibar wenzake na wasanii wake wengi walidaiwa kuwa waislam, akawapa jibu jepesi tu kuwa mbona producer wake mkuu Roy alikuwa Mkristo.

KGT yeye aliendelea na Abby Skills, na Ali Kiba lakini akatuibulia Pasha na kufanya kazi nyingi na Picco Kikongwe.

Msanii gani mwingine au ngoma gani nyingine zilipikwa G2 na zimesahaulika?

Una kumbukumbu gani nyingine kuhusu G RECORDS?
LUAH
110523.
View attachment 2618590View attachment 2618591
View attachment 2618592


ICE CREAM--NOORAH

You're the kid that came to rap, right?
(Yeah, toka Shy-Town)
Uh huh
The one and only
Ni Noorah A.K.A. BabaStylz (Babastylz)
Oh, yeah nipo na Suma Lee
Muite Roy ndani ya G-Recordz
Chemba Squad
Ebwana Ibra eh!
Yeah, utaipenda hii

Akatizapo kila street midume yenyewe zapwita
Akikuta kijicho ni kama anakuita
Ooh anawachengua matoz, mtoto anayajua mapozz

Daah hii ilikuwa moja ya ngoma kali sana kutoka kwa Noorah ft Sumalee, beatz ikisukwa na Roy from G Records

Video kali enzi hizo chini ya Director Adam Juma from Visual Lab

RIP Roy, kazi zako tutazikumbuka sana sana
 
Back
Top Bottom