Utavumiliaje penzi hili?


Piga sala sana kaka! Hicho kimeo kaka! Ukishamaliza sala fwata huu msemo.....HOME IS WHERE YOUR HEART IS!
 

Hii ni moja za kesi ngumu kidogo katika mahusiano ila binafsi nafikiri jaribu kuzungumza na wasimamizi wenu wa harusi kwani inapoelekea sasa utahatarisha ndoa yako na zaidi ya yote watoto, matron anaweza kukusaidia kukzungumza nae kama ni mtu mwelewa na yeye, ila nisingekushauri utoke nje ya ndoa kwani sio tiba jaribu kutibu matatizo ya ndoa yako mapema kabla mambo hayajawa mabaya zaidi.
 
Umezunguka sana kwenye post yako nimekusoma kisaikolojia umempenda sana huyo malaya wa nje ila wife iz ze best kuliko huyo malaya kaa chini umiza kichwa mkeo atabadilika.
 
Pole sn,kwa vile mkeo anamisimamo ya kidin nakushauri ongea na watumishi wa mungu wanaohusika na kutoa mafundisho na ushauri wa ndoa kanisan kwao hasa wanawake waeleze matatizo ya mkeo wao wataongea naye kutumia maandiko ya biblia watamfundisha mbinu namajukumu yake yote ya kumridhisha mume kunako 6 kwa 6,mapoja na majukumu ya nyumban ikiwamo usafi hakika ataelewa na utashangaa namna atakavyobadilika,

Wakati anahudhuria mafunzo hayo hakikisha unampa sapoti yote ikiwezekana nawe uhudhurie ili nawe ujieleze vile unavyotaka awe na ahakikishiwe mbele yako kuwa maandiko hayapingani na kuridhishana kimapnz kwa wanando.

Naamin malezi na mazingira aliyokulia ndio yamemfanya awe hivyo,na nashindwa pia kuelewa ilikuwaje huko kwao wamwache binti yao aolewe bila hata kupata mafunzo hata yale ya kawaida tu kuhusu maisha ya ndoa mpaka usafi tu unamshinda!!
Kila laheri naamini km mtashirikiana kwa pamoja huyo atakuja kuwa fundi mpaka utamsahau huyo kimda wako.
 
khaaa... Best shughuli nzito hapo mh! Kaz unayo
 
Wanaume wa siku hzi na nyie mmezidi...eti kuna mwanamke wa kuoa na wa kuzugia (yani wa starehe), sasa wewe ulitaka wa kuoa, mara nyingi hao mnaowaita wa kuoa ndo walivo (yani wale wa me nasoma kaseti langu ukimaliza funika)!Wanawake na nyie ndoa mnazitaka kumbe shuhuli hamuiwezi, wanaume wenu wakipita kona wakikutana na sie ma-single.......shuhuli inakuwa pevu hata kurudi makwao inakuwa tabu......! Hapo pagumu kaka, huo wako mzigo ubebe tu ndugu! kuutua ni hadi kifo kiwatenganishe.......au mwisho wa dunia......
 
he, pole sana ,lakin huna makosa jukumu analo huyo wife wako yeye ndio chanzo , sasa apo wataalamu wakupe ushauri ,bcz love without hapiness is useless, hapo kwa mwanamme yeyote hachukui tafran hiyo ,, sijui uyo dada dini gani ilo mwambia kua asimfurahishe mume wake, balaa duniani m,mungu atustiri tusiwe miongoni mwa kama yeye ameen
 
mmh pole sana mkuu.
fanya yoote usimsahau mkeo kbs, we endelea 2 kumfundisha mdogo mdogo ivyo ivyo atacopy tu jaman. huyo wa nje usimtilie maanan kbs, ikiwezekana piga chini mpe 2 somo mkeo tena la kiu2 uzima nina iman atakuelewa.
 
Umesema wote mlikuwa bikira tofauti yenu ni wewe kuwa ulipata kabati ka kuingia mjini kabla yake. Nina imani kabla ya kufunga ndoa wote mlifundwa ni jinsi gani ya kuishi mkiwa kama mme na mke, ndoa yenu kama ilikuwa ya kiislam, kristo, serikali, au kipani lazima mlipata. Sasa rejea kwa somo yake au shangazi yake nenda kamweleze jinsi gani ndoa yako imegeuka shubiri tofauti na asali uliyotaraji toka kwa mkeo huyo ambaye ameshindwa kufuata kile unachopenda.
Kuhusu huyo rafiki ulie mpata nashauri jaribu kuanza kukata kamba taratibu ingawa najua itakuwa ngumu kumeza hii, ili ulee mkeo na mtoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…