SoC02 Utawala Bora katika Taifa

Stories of Change - 2022 Competition

KHALFAN CHETU

Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
10
Reaction score
10
Utawala ni Hali inayoakisi sifa nyingi zilizopo kwenye Matabaka Makuu Mawili ambayo yanaunganishwa na Tabaka liitwalo Mifumo/Mfumo. Sifa kama Utii,Uzalendo,Ukarimu,Ubunifu,Kujitoa,Misimamo Madhubuti,Utu,Kujituma,Ushirikiano na kadhalika. Hizo ni baadhi tu za Sifa zilizopo kwenye Tabaka la Watawala na Watawaliwa.

Kwa hivyo, Utawala unaelezeka katika Maeneo Makuu Matatu kwa Ujumla,Yaani ni WATAWALA,MIFUMO na WATAWALIWA. Ama kwa Lugha rahisi tunaweza kusema ni VIONGOZI,KATIBA na WANANCHI. Kimsingi,Mifumo ndiyo inayoweza kutumika kuwapata Watawala na Mifumo ndiyo kiunganishi pekee kati ya Watawala na Watawaliwa hii ni kwasababu palipo na Tabaka zaidi ya Moja huwa Hekima inahitaji Mifumo wezeshi itakayotengeneza Uwiano kati ya walio kwenye Tabaka la Juu na wa Tabaka la Chini Kimamlaka.

Ili Utawala uwe Bora au Dhaifu utategemeana na vile Mifumo itakavyokua. Ukitazama kwa Nchi kama Tanzania,Sababu kubwa ya Matatizo mengi mara zote ni Mifumo dhaifu ya Kiutawala ambayo inajumuisha Katiba,na Hali zinazoakisi Tafsiri Mbovu na Potofu kuhusu Demokrasia. Dhana ya Utawala Bora kwa Taifa lolote lile inataswira nyingi zinazokubalika ambazo hata kama Tanzania itazizingatia basi pia itakuwa Moja kati ya Nchi zenye Utawala Bora. Baadhi ya Taswira hizo ni kama ifuatavyo:-


(1)HAKI ZA BINADAMU NA MAADILI; Katika Mataifa mengi yanayowakutanisha Watu wenye Itikadi tofauti za Kiimani na Kimila ni Utawala Bora pekee ndio unaoweza kuisimamia Jamii yenye Watu wenye Mitazamo kinzani kuishi kwa Amani pasina kuhitilafiana, lakini pia Pasina Watu hao kuyakiuka Maadili ya Jamii kupita kiasi kwa kisingizio cha HAKI ZA BINADAMU. Yaani kipindi ambacho kila Mtu anapewa Uhuru wa mambo yake binafsi inapaswa kuhakikishwa hawavunji Sheria na kuingilia Itikadi,Mila au Imani za Watu wengine. Kwenye Hoja hii ni dhahiri Tanzania bado haikidhi vigezo vya kuwa Nchi yenye Utawala Bora kwasababu inashindwa kukabiliana na Maudhui mengi kwenye Nyimbo za Wasanii wa Ndani wanaovaa Nusu Uchi kwenye Nyimbo zao na Majukwaani.


(2) UHURU WA KUONGEA; Sifa moja wapo pia ya Utawala Bora katika Nchi yoyote ni kuuelewa Utofauti uliopo kati ya Uhuru Wa Mwananchi Wa Kukosoa au Kutoa Maoni dhidi ya Uhuru Wa Mwananchi Kukashifu Na Kutukana. Kimsingi, Serikali nyingi husema kuna UHURU WA KUONGEA kwenye Nchi zao lakini Raia wao hujikuta kwenye Matatizo baada ya kumaliza kuutumia Uhuru huo, na kwakua Utawala Bora ni ule unaojumuisha Wananchi,Katiba na Viongozi kuna Muda hata Wafuasi wa vyama vya Upinzani nao huvuka mipaka katika Maneno yao pasina kuupima Uzito wa Athari kwa Amani na Usalama wa Nchi wakiamini kuwa Wanautumia Uhuru wao wa kuongea.


(3)DEMOKRASIA NA UZALENDO; Mataifa mengi yenye Utawala Bora wenye Viwango toshelevu kwa Mahitaji ya Raia wake wanajua MAHALA sahihi katika HALI sahihi ambazo kwao huamua kuutumia UZALENDO kama Kiungo cha DEMOKRASIA pale inapoonekana kuwa Maamuzi au Mitazamo ya wengi haiwezi kufikia Mustakabali mwema wenye MATOKEO chanya kwa kila Upande na kwa Taifa. Mfano, Kupitia Demokrasia maamuzi ya Taifa kuingia kwenye VITA au kuzuia Uingizwaji wa BIDHAA zinazoshukiwa kuhatarisha Afya za Binadamu yanaweza yakakwama au yakachelewa kwa kutafuta Maridhiano ya kila Upande hata kama TAIFA lipo kwenye HALI ya hatari ilihali huwenda baadhi Wamepokea Hongo ili kuhujumu Maamuzi ya Kizalendo. Hivyo basi,Mataifa yote Makubwa Mifumo yao ya Kiutawala imeikutanisha Demokrasia na Uzalendo kama Ndugu ndio maana yanapokuja Maswala ya Maslahi ya ndani ya Taifa,kwa pamoja Wapinzani na Serikali huungana Chini ya Kimvuli cha Uzalendo. Ila kwa Taifa kama Tanzania bado Watu wanaamini sana katika Uvyama ndani ya kichaka cha Demokrasia hata kwenye mambo ya Kitaifa kwa kupinga Kila Kitu, hivyo ili kwetu Utawala Bora usiishie kuwa Kitendawili tunahitajika kuiunda DEMOKRASIA mpya ya Kitaifa yenye DIRA YA UZALENDO,kama ilivyo CHINA,URUSI,IRANI,MAREKANI na Mataifa mengine ambayo kwao TAIFA kwanza kisha Uvyama baadae. Hoja hii naipigilia Msumari kwa NUKUU ya JAMES MADISON(1789) Inayosema kuwa "...TAWALA ZA KIDEMEKRASIA DAIMA ZIMEKUA MBONI ZA VURUGU NA USHINDANI.. NA KWA UJUMLA KAMA AMBAVYO ZIMEKUA NA UMRI MFUPI KATIKA MAISHA YAO NDIVYO AMBAVYO ZIMEKUA KATILI KATIKA VIFO VYAO...".

(4)WATU NA UCHUMI; Kokote kule Ulimwenguni, Nchi yenye Utawala Bora huhakikisha kuwa Uchumi ni Watu. Hapa nikiwa Namaanisha kuwa RAIA WAZAWA na si MTU yeyote. Mataifa mengi yanayotazamwa kama Mifano ya Utawala Bora yamehakikisha kuwa Uchumi wao unajengwa na WAWEKEZAJI WA NDANI zaidi kuliko wale wa NJE na hiyo ni katika kuhakikisha Mataifa yao yanajitosheleza kwa kiwango Stahiki kwa kuwapa FURSA na VIPAUMBELE zaidi RAIA wao kwa kuwatengenezea Mazingira Rafiki Wajasiriamali Wadogo na Wakubwa.
Taifa kama Tanzania pia linaweza kunasibishwa kama Miongoni mwa Mataifa yenye UTAWALA BORA endapo itajidhatiti katika kujenga na kuuinua UCHUMI WA TAIFA kupitia Watu wake wa ndani kwa kuwatengenezea Mazingira na Mifumo rafiki itakayowawezesha Wajasiriamali wa aina zote kuuendesha Uchumi wa Taifa lao pasina kuwategemea Wawekezaji wa Kigeni Moja Kwa Moja.


(5)UWAJIBIKAJI,NIDHAMU NA KUJITOA; Miongoni mwa Sifa za Utawala Bora ni Uwajibikaji wa Watumishi na Viongozi,Nidhamu pamoja na Kujitoa. Nchi nyingi ikiwemo Tanzania Watumishi wakubwa katika Serikali na Uongozi,hawana Tabia za Uwajibikaji isipokua kujionyesha kwa Wakubwa wao na kwa Wananchi. Viongozi na Watumishi wengi wa Serikali wamekosa Nidhamu kiasi kwamba kwao hawaoni HATARI iliyopo katika kutoa Maneno ya kuwakashifu hata waliokufa pasina kutazama ni kwa kiwango gani wanaibua HISIA Hasi na Maumivu kwa Raia na Ndugu wa Hao wanaokejeliwa. Lakini pia siku hizi tumekosa Viongozi ambao kwao ni HERI waumie au hata kupoteza MAISHA katika kulilinda TAIFA,WATU na RASILIMALI.

Mara zote UFUNUO hauji kwa vilivyowazi,bali kwa vilivyofunikwa. Na kila kilichofunikwa kina HILA ya Upumbavu na Upofu wa vilivyo Nje. Kama ambavyo UTAWALA BORA ni Ndoto ya kila RAIA katika Taifa,Ndivyo kila MTU anavyohitajika kuufumbua Mdomo wake ama Kurasa zake ili kuongea au kuviandika vitakavyofunua MACHO ya wenzetu waliolala ili kuwajuza na kukumbushana juu ya Safari tuliyonayo kama Taifa kwasababu hata Viongozi wa LEO ndio walewale WATU ambao walikua miongoni mwetu Miaka ya Nyuma.


 
Upvote 4
Shukrani sana..
Kwangu UZALENDO naufananisha na MTI wa Matunda unaohitaji MAJI,RUTUBA na MWANGA ili Unawiri.. Nikimaanisha kwamba UZALENDO una NGUZO zake kuu TATU kwa namna ninavyoutazama,Nazo ni:- WATU,SERIKALI na MAZINGIRA MAZURI. Kama ambavyo MMEA hunyauka ukikosa KIMOJA kati ya RUTUBA,MWANGA au MAJI ndivyo hata UZALENDO hupotea pasipo na MAZINGIRA MAZURI kwenye JAMII kama AJIRA,USALAMA na Kadhalika ambavyo Vinategemewa kutoka kwa VIONGOZI.. Lakini pia WATU wenye IMANI,NIDHAMU na UTII. kisha SERIKALI ambayo licha ya WATU wake kuishi katika MIFUMO YA IMANI,NIDHAMU na UTII.. yenyewe inapaswa kuendesha TAIFA kwa Maslahi ya Wote na si kwa Maslahi yao Binafsi lakini pia Waonyeshe HALI ya Uchungu na Taifa lao na si vinginevyo. HUO NI UZALENDO TOSHA, KINYUME NA HIVYO NI KUJARIBU KUJIINUA KWA KUJIDONDOSHA.
 
Kaka Khalifa

Nimekupigia Kura Naomba na Mimi unipigie Kura kupitia SoC 2022 - Tufuge nyuki kwa maendeleo endelevu na tuwalinde kwa wivu mkubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…