UTAWALA BORA
Utawala Ni mamlaka aliyonayo mtu wa uteule aliyeteuliwa au kuchaguliwa na watu ili aweze kuwa muwakilishi na kiongozi wao katika kushughulikia masuala mbalimbali ya kijamii katika kitengo husika alichopewa inaweza kuwa ni Rais, Waziri Mkuu au Mbunge .
Nini utawala Bora?
Utawala Bora ni Hali ya mtawala au kiongozi kusimamia na kuongoza kwa niaba ya wananchi waliopo chini yake kwa mafanikio makubwa yanayopimwa na utendaji kazi wake.
Utawala Bora hupimwa na Mambo mbalimbali ikiwemo Imani ya wanaoongozwa, msimamo chanya, uwajibikaji katika sekta husika, chachu ya maendeleo kisiasa, kiuchumi,kiutamaduni, kijamii na kimazingira, mfano wa utawala Bora wa Raisi Samia Suluhu Hassan unaweza kupimwa kulingana na jinsi anavyoliongoza taifa la Tanzania akihakikisha Mambo yote yanayohusu maendeleo ya taifa katika sekta zote.
Pia, Utawala Bora huwa na faida nyingi ndani na nje ya nchi husika kwa ngazi ya mbunge utawala utaonekana Bora Kama atakuwa Ni muwajibikaji katika Jimbo lake akisimamia ipasavyo miradi mbalimbali ya kijamii katika KULETA mabadiliko chanya Kama vile kuhakikisha wanajamii wananufaika kiafya, kiuchumi na kijamii kutoa huduma za elimu kwa kujenga madarasa, umeme kwa kuhamasisha uwekaji wa nguzo za umeme na vyanzo mbalimbali vya nishati pia huduma nzuri za mawasiliano, uchukuzi, biashara na kilimo Bora.
Ikiwa ni Rais au Waziri Mkuu Basi ataitwa mtawala Bora Kama nchi itakuwa inaendeshwa kwa mujibu wa Sheria za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kukubaliwa na wananchi, kuwa msaada kwa wale WENYE uhitaji na kupewa Majina Kama "Mtetezi wa wanyonge".
Utawala Bora utakuwa na faida nyingi ndani ya nchi kama wananchi watakuwa Ni wenye furaha na kuridhishwa na mwenendo wa watawala wao ikiwa ni pamoja na:
• Uhusiano Bora wa Kimataifa, nchi yoyote ili iwe na utawala Bora lazima iwe na uhusiano mzuri kimataifa na mataifa yaliyoendelea na yanayoendelea, kwa sababu utawala Bora ndiyo utakaobainisha matunda ya huo uhusika wa nchi kimataifa Kama vile kutoa misaada ya kifedha na misaada mingine ya kijamii katika sekta za Afya,elimu,maji na nishati.
Kinyume chake utawala ukiwa mbovu Basi matokeo yake ni kuleta athari hasi Katika jamii na nchi kwa ujumla, kwani mataifa mengi yaliyoendelea yamekuwa yakitumia udhaifu wa baadhi ya viongozi wa mataifa yanayoendelea kama mataifa ya Malawi, Tanzania, Uganda,sudani kusini na kadhalika matokeo yake ni kuanguka kiuchumi na kupelekea matatizo Kama umasikini na magonjwa pia kuingia kwa vitu hatarishi nchini. Si hivyo tu Bali pia unyonyaji wa maliasili Kama madini kwaajili ya manufaa yao.
Lakini pia Utawala Bora ni nyenzo kubwa na muhimu ya kuifanya nchi au dola kuwa imara kwani hutambulika kutokana na namna viongozi wanavyoendesha nchi wakishirikiana na ulinzi au jeshi la kujenga taifa kuhakikisha usalama unakuwa mzuri utakaokuwa na tija kuleta amani, upendo, mshikamano, hekima, umoja na Uhuru wa raia katika maisha yao ya kila siku ya kibinafsi na ya kijamii.
Changamoto za utawala Bora, utawala Bora huweza kukwamishwa na baadhi ya vikwazo na kuifanya nchi itetereke Kama vile, fedha, amani kutoweka, migogoro ya kisiasa, Vita vya wenyewe kwa wenyewe, uhusiano mbovu baina ya mihimili ya serikali, kutokuwa na Uhuru wa raia na viongozi wao.
HITIMISHO; Utawala Bora ni nyenzo kubwa na muhimu Sana katika kuhamasisha maendeleo ya taifa kwani wawakilishi hawa wa wananchi wakiwa vizuri na misimamo yao ikawa imara dhidi ya maadui Basi hakika Mambo yataenda ipasavyo kwa uwezo wake Mungu, pia viongozi wanatakiwa kuwa na utegemezi mkubwa wa Mungu ili kuliweka taifa katika mikono salama ya Mungu dhidi ya maadui wa taifa letu, pia kuwa na Sera Bora za kuhamasisha maendeleo Kama Ile ya Hayati Dk. John Joseph Magufuli ya "Hapa Kazi Tu".

Upvote
1