Utawala wa Kijeshi Niger: Mkituma Jeshi tutamuua Rais Bazoum

Mara nyingi ukivamia nchi kama hivyo inatakiwa upate sana sapoti ya wananchi ila nje ya hapo hayo mavamizi wanaenda kugeuzwa mishkaki yenye ndimu nyingi mbaya sana wananchi wakiunga mkono hawatapata msaada wa maana hapo
Hilo ni hakika.Kenya walitamani kuikalia Somalia kikoloni kwa kutekeleza matakwa ya West.Mpaka leo hawajaweza.
 
Kwa mujibu wa ECOWAS hiyo si shida kwao alimuradi wanatekeleza katiba yao ambayo Niger walisaini na umoja huo
 
Kwa mujibu wa ECOWAS hiyo si shida kwao alimuradi wanatekeleza katiba yao ambayo Niger walisaini na umoja huo
Hawaoni shida kuuliwa Bazoum.Kama akiuliwa itabidi wasimamie uchaguzi kumpata raisi mpya.Hiyo ndio itakuwa nini sasa ?
 
Mara nyingi ukivamia nchi kama hivyo inatakiwa upate sana sapoti ya wananchi ila nje ya hapo hayo mavamizi wanaenda kugeuzwa mishkaki yenye ndimu nyingi mbaya sana wananchi wakiunga mkono hawatapata msaada wa maana hapo
Wananchi WENGI Wana Chuki kubwa sana Kwa watawala wao na uhuni wao.

Historia ina tabia ya kujirudia.

Karne ya Kumi na tisa Babu zetu waliuza nchi zetu kwa Wageni wakiamini Wageni watawaletea maisha mazuri.
Karne mbili Karne moja mbele Babu zetu wakawakimbiza Wageni ambao waligeuka kuwa Wezi na wanyonyaji. Historia ikaandikwa.

Karne moja Mbele viongozi WETU wanauza Tena nchi Kwa Wageni Tena. Historia imejirudia.
Kuna wanaopinga sana uuzwaji Wa nchi zetu Kwa Wageni kama walivyopinga Babu zetu wakati Wa mkoloni
Historia imejirudia.

Dunia inakimbia Kasi na miaka inakimbia kulingana na Teknolojia. Miaka michache historia itajirudia .Watatokea wajukuu Wa Wapigania uhuru waliomwaga damu zao na kuzipigania Tena nchi Zao Kwa Nguvu kubwa .
Damu ya Babu zao Zinalilia ardhi yao.
Historia itaandikwa upya.
 
Hao wanatafuta tu huruma. Hivi wanaikumbuka kweli operation Entebe. Idd Amini angekuwa hai angewakataza kauli zao. Ecowas wakishindwa kum rescue basi waombe Israel ikafany mambo yake kule. Hata km wamefunga anga wanaume wataingia tena bila hata upinzani wa kuandikwa magazeti na watamtoa na kuondoka naye safely. Wanajizima data wakati wakijua majeshi ya USA na Ufaransa yapo hapo kitambo na wanamuunga mkono rais aliyepinduliwa na yanajua Hadi huyo aliyetwaa madaraka anapojisaidia haja kubwa.

Semea tu ni kwa vile ecowas ni toothless dog na ukiongeza na umaskini wa nchi zao inakuwa ni sawa na mtori usio na nyama.
 
Hawaoni shida kuuliwa Bazoum.Kama akiuliwa itabidi wasimamie uchaguzi kumpata raisi mpya.Hiyo ndio itakuwa nini sasa ?
Kwanini auliwe sasa? atapelekwa mtu The Heague nani kawatuma wapindue kwani hawakujua kama kuna ECOWAS
 
Tz misukule inalinda ugali wao.
Pamoja na kwamba baadhi ya mambo hayapendezi nchini, lakini kitu kinachoitwa mapinduzi ni cha hovyo sana. Hao Niger ni mapinduzi ya mara ya 3, 4. Je, kuna mabadiliko yoyote ya kiuchumi tofauti na uafrika wetu?
 
Kuna nchi ni ngumu sana kuziishi, Mali, Sierra Leon, Somali, Sudan, Liberia, Burkina Faso, yaani ni tatizo

Ukipata kazi huko ya kufanya ni bora mtu usiende tu, uteme hilo tonge.
 
Kuna nchi ni ngumu sana kuziishi, Mali, Sierra Leon, Somali, Sudan, Liberia, Burkina Faso, yaani ni tatizo

Ukipata kazi huko ya kufanya ni bora mtu usiende tu, uteme hilo tonge.
Shida umasikini wa fikra ,ubinafisi ,choyo na tamaa ni vitu vibaya vinavyo mtesa mwafrika,kiongozi wa kiafrika akishapata mali, familia na koo yake ikawa na uhakika wa kula na kufanya anasa anajiona kila kitu kaweza ,anasahau taifa lake na kuwa kibaraka wa nchi za magharibi

Waafrika wengi wanaishi maisha ya shida sana na bado wana shurutishwa kulipa kodi kandamizi na kodi zao zinatumika hovyo kushibisha matumbo ya viongozi na familia zao hadi koo,
Rasilimali za nchi zinatumika vibaya,wanaingia mikataba mibovu na ya hovyo na wanaendelea kujilimbikizia mali na kuweka hazina ya mali kwa vizazi vyao.

Laiti waafrika wangekuwa na vision kama ya Gaddafi tungekuwa mbali sana.

Wamagharibi hawajawahi kuwa watu wazuri kwetu,wapo kimasirahi sana na hawana mchezo na mtu anae cheza na tonge yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…