Enzi ya USA ni kweli inaenda kupita kama taifa ambalo liliwekwa na God strategically kwa ajili ya kueneza injili ya Yesu Kristo pamoja na kuisupport Israel. Hii ni enzi ya mataifa na ipo ukingoni. USA haitajwi moja kwa moja kwenye biblia lakini Ulaya ipo kwa maana ya ufalme wa rumi ambao ulikufa na sasa umerudi kupitia jumuia ya ulaya. Mpinga kristo atatokea jumuia ya ulaya kwa maana ya lile andiko la pembe moja iliyochomoza katika zile 10. Ninavyoamini unyakuo upo karibu sana! lakini ni ngumu kusema timeline yake ila ni kweli dunia inaelekea pagumu sana kiuchumi na kuna uamsho mkubwa wa mwisho umeshaanza na utaendelea kwa kipindi fulan hivi ambapo watu wengi watampokea Yesu.Huyo mpinga kristo ataibuka siku chache baada ya unyakuo na kwa kuanzia ataonekana ndiye mkombozi wa ulimwengu kwa maana ya shida za kiuchumi, na hata mgogora wa israel na palestina atatoa suluhu ambapo atafanya mkataba na israel ambapo miaka mitatu ya mwanzo israel itaona kweli shida yake na palestina imeisha lakini miaka mitatu na nusu tu ikiisha israel wanageukwa na huyu jamaa na majeshi ya Libya, Ethiopia, Russia, Iran na mengine yataivamia Israel. Israel itakula kichapo kibaya sana, lakini inapofika miaka 7 ndipo sasa Yesu anarudi na kuiokoa Israel.
Mojawapo ya sababu ya USA kutokuwa nguvu tena baada ya unyakuo ni kuwa hakutakuwa tena na wale waombaji waliojitoa kwa dhati na ambao wamekuwa wakiomba toba kwa ajili ya taifa la USA lakini siyo hivyo tu hakutakuwa na waombaji wanaoombea mafanikio ya USA maana itakuwa wamenyakuliwa so lazima lifike mwisho na ndiyo maana hata Israel itabaki ukiwa maana watetezi wake kwa maana ya wanaoliombea mema kwa Mungu wengi sana watakuwa wamenyakuliwa.
Kwa wale tunaoamini katika kumkiri Yesu Kristo kuwa bwana na mwokozi wa maisha yetu ni wakati wa kuendelea kujitakasa kwa maana ikitokea ukaukosa unyakuo aisee kipigo cha Mungu katiko hiyo miaka 7 aisee acha tu ni dhiki kuu kweli kweli.