Utawala wa Rais Samia ni kama tuko fungate (Honeymoon); inabidi tuwe na Katiba Mpya ili ndoa iwe salama kwa wote

Utawala wa Rais Samia ni kama tuko fungate (Honeymoon); inabidi tuwe na Katiba Mpya ili ndoa iwe salama kwa wote

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Utawala uliobora ni ule utawala wa makubaliano baina ya mwanaichi na mamlaka

Suala la katiba mpya nalifananisha na ujio wa chupi za watoto maarufu pampas!

Zilipo ingia kwa Mara ya kwanza Tanzania baadhi ya watu walizipinga sana, wengine walidai zinaleta uhanisi kwa watoto, wengine walisema hazina maana! Yote hayo yalitamkwa kwasababu Africa hatupendi ustaarabu!

Katiba ni jambo la kistaarabu, katiba inaondoa ukinyaa, katiba ni mwongozo!

Katiba ya sasa haitoi taswira ya usawa katika kugawana keki ya taifa!

Kwa mfano!
  1. Kwa sasa kiongozi yoyote akifanya ufisadi, katiba haina adhabu kali kwa kiongozi huyu zaidi ya kumtangaza kwenye vyombo vya habari kuwa ni fisadi
  2. Katiba ya sasa inampa mamlaka hata RPC au polisi yoyote kumbakikia kesi au tuhuma mbaya mtuhumiwa ambaye hana hatia, na haiwawajibishi kwa makosa hayo hata pale mahakama inapobaini kuna undanganyifu. Hivyo udhalilishaji nakuchafuliwa jina kwa watu wasiyo waharifu bila katiba mpya kutaendelea tu maana polisi hawawajibishwi kwa uongo, ebu tafakari mtu anasota rumande yenye mateso kwa miaka miwili familia yake wanataabika kiasi gani kwa kesi za uongo?
  3. Ebu fikilia taifa linapata hasara kiasi gani kwa maamuzi mabovu?
  4. Huwezi kukwepa katiba mpya kama kweli unamalengo ya kuinyoosha inchi, katiba ni kila kitu na kila mahali!
Katiba ni mwongozo usiyohitaji kuwa na mtu mmoja! Mtu huishi na kufa lakini katiba haifi!

Ikumbukwe hata China walivyotunga sheria Kali ndipo na uchumi wao ulipaa!

Kwanini Tanzania tunaogopa katiba mpya? Kama kuandaa katiba mpya ni gharama kwanini tusichangie au kukopa kwa ajili ya katiba?

Kama ujenzi wa madaraja tunakopa fedha nyingi, hatushindwi kugharamia pia ujenzi wa katiba mpya!

Utawala wa Rais samia kaanza vizuri, lakini tusisahau huu ni utawala wa honeymoon! Bila katiba bora huko kwenye ndoa ugomvi hautaisha
 
Katiba katiba haikwepeki, mwendazake kashatuonesha namna katiba yetu ilivyo mbovu, kuna siku kwa katiba hii tunaweza pata mtu zaid ya mwendazake tukaamuriwa kutokauchi nyumbani hakika mm kwa moyowangu wote nipo tiyar kwa lolote katiba ipatikane tumechoka.
 
Hakika, mambo ya kuambizana kuna mtu anainyoosha inchi siyo
 
Hapo namba 2 sijaelewa Mkuu, ni kivipi Katiba ya sasa inamruhusu RPC au polisi mwingine yoyote kumbambikizia raia kesi?
 
Hapo namba 2 sijaelewa Mkuu, ni kivipi Katiba ya sasa inamruhusu RPC au polisi mwingine yoyote kumbambikizia raia kesi?
Kwasababu RPC anaweza kuita waandishi wa habari kumtangaza mtuhumiwa kuwa ni muovu, jambaz au hata kumuita muuza madawa bila kutiwa hatiani!

Mambo kama hayo yenywe kutweza, kuchafua au kuuwa biashara na utu yanafanyika!

Na hao ma RPC hawawajishwi kwa makosa hayo hata pale mahakama ikibaini udanganyifu kwa mtuhumiwa.
 
Wanaotaka katiba mpya ni Chadema sio wananchi wananchi tunataka Kazi iendelee.
 
Kwasababu RPC anaweza kuita waandishi wa habari kumtangaza mtuhumiwa kuwa ni muovu, jambaz au hata kumuita muuza madawa bila kutiwa hatiani!
Mambo kama hayo yenywe kutweza, kuchafua au kuuwa biashara na utu yanafanyika!
Na hao ma RPC hawawajishwi kwa makosa hayo hata pale mahakama ikibaini udanganyifu kwa mtuhumiwa
Mkuu naomba nikueleweshe jambo. Katiba ya nchi ni Sheria mama na ndiyo maana haina Chapter. Ila Sheria nyingine zote za Tanzania zina 'Chapter' kuanzia 'Chapter 1' na kuendelea. Siyo kila kitu kimo kwenye Katiba, vingine Katiba inaelekeza vikasomwe kwenye Sheria nyingine kama vile Police General Orders (kwa kada ya askari polisi).

Hakuna mahali Katiba imeruhusu unayoyasema either expressly or impliedly. Hayo ni makosa ya askari yeye binafsi na madhaifu yake kiutendaji kwa kufanya kazi bila kuzingatia weledi. Hata hivyo, jeshi la polisi lina Sheria zake kama vile Police General Orders n.k ambazo zinawaongoza.
 
Mkuu naomba nikueleweshe jambo. Katiba ya nchi ni Sheria mama na ndiyo maana ni 'Chapter 1' ya Sheria zote za Tanzania, Sheria nyingine zinafuatia kwa kupewa 'Chapter 2' na kuendelea. Siyo kila kitu kimo kwenye Katiba, vingine Katiba inaelekeza vikasomwe kwenye Sheria nyingine kama vile Police General Orders (kwa kada ya askari polisi).

Hakuna mahali Katiba imeruhusu unayoyasema either expressly or impliedly. Hayo ni makosa ya askari yeye binafsi na madhaifu yake kiutendaji kwa kufanya kazi bila kuzingatia weledi. Hata hivyo, jeshi la polisi lina Sheria zake kama vile Police General Orders n.k ambazo zinawaongoza.
Huwezi kuniambiwa hao ma RPC ote tunaowaona kwenye maTV kila siku wakitangaza watuhumiwa wawe hawajui P.G.O inasemaje!
Nachojua hakuna sheria ya kiwabana ndiyo maana hata wakibambika haiwaumizi!
 
Huwezi kuniambiwa hao ma RPC ote tunaowaona kwenye maTV kila siku wakitangaza watuhumiwa wawe hawajui P.G.O inasemaje!
Nachojua hakuna sheria ya kiwabana ndiyo maana hata wakibambika haiwaumizi!
Siyo wote mkuu. Na kwa kumbukumbu zangu ni kwamba IGP alishapiga marufuku kutangaza wahalifu kwenye media na alimpiga hilo biti Muroto wa Dodoma.
 
Back
Top Bottom