Utawasimulia Nini Wajukuu Zako?

BUSARA ZANGU

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2013
Posts
779
Reaction score
1,269
Heshima kwenu wakuu

Leo ni siku nyingine, na mada nyingine mezani. Katika Maisha yetu naamini tumewahi kukaa na wazee ama watu waliotuzidi umri ambao wametusimulia mengi yaliyotokea kwenye maisha yao. Mengine mazuri, mengine hawataki hata kuyakumbuka.

Naamini ipo siku tutakuwa watu wazima ama wazee Mungu akitujalia uzima. Je tunataka tuwasimulie nini watoto ama wajukuu zetu? Kuna mzee mmoja aliwahi kunisimulia jinsi alivyokataa kiwanja/eneo sinza miaka ya 1980 akidai ni porini,wakati huo anadai mpaka sungura walikuwepo maeneo ya sinza. Je wewe sinza yako ya leo ni ipi? Chaka gani ambalo unalidharau na hutaki eneo hata bure? Ndugu, ardhi inapanda thamani kila leo. Tengeneza stori nzuri kwa wajukuu zako.

Mimi nataka niwasimulie jinsi nilivyoanguka mara 20 kwenye biashara zangu tofauti kabla sijasimama na kuanza ku make katika biashara zangu. Sitaki kusimulia wajukuu zangu jinsi nilivyoanguka kwenye biashara nikaona bora niajiriwe.

Utawasimulia nini wajukuu watakapokuuliza mbona wewe huna hela kama yule rafiki yako tajiri ambaye kila siku unawaambia wajukuu zako kwamba mlisoma naye. Je utawaambia Mungu ndio amempa yeye na amekunyima wewe? Je utamwambia huna bahati?

Je utawasimulia jinsi ulivyokuwa unazichanga na kujenga mpaka ukajenga nyumba ya 1,2......8....ama utawasimulia jinsi kiinua mgongo kiivyosaidia kumaliza nyumba yako kwa tabu?

Je utawasimulia jinsi ulivyokuwa cha pombe, mpenda mademu na namna ulivyowala.

Tafuta stori nzuri kaka. Tafuta stori nzuri dada ya kusimulia wajukuu/watoto wako. Andaa maisha yako sasa hivi ili uwe na stori tamu kuhusu maisha yako na uache legacy nzuri (sijui Kiswahili chake).
 
Nitawasimulia safari yangu ya elimu.. Tokea mwanafunzi mbovu wa hesabu mpaka kuwa namba moja wa darasa mpaka kuwa injinia...

Pili nitawasimulia kwamba tuliwahi kuwa na rais ambaye (hapa naomba nisimalizie...)
 
Good Thinking Comrade.

Mada kama hii Jamii Forums, si mada pendwa. Tu wepesi mno wa kuchangia mada pendwa ambazo utamu wake huwa ni wa kitambo kidogo tu. Ngoja nidodose kidogo...

Today is your future. Maandalizi bora ya sasa ni mavuno bora ya uzeeni. Pia ya kusimulia uzeeni hupandwa leo. Iwe bora au duni, nzuri au mbaya.

Tuandae material things vya msingi, Asset za maana na kadhalika. Mjukuu akikuta viwanja, apartment za maana, maktaba iliyosheheni vitabu, ghala za kuhifadhia nafaka....itafana mno. Si akute Library za CD's za bongo movie, sub woofer za kila aina na orodha inaendelea..

Akute Autobiography yako, iso na ujanja ujanja ndani. Aisome na kuing'amua. Asikute vyeti feki. Akute tuzo mbalimbali za kijamii na kielimu na mengine mengi ya dizaini hii.

May almighty God strengthens all of us.

Asalaam.
 
Well said. I can't ask more contribution from you.
 
Legacy...ni urithi...vyema ila ungeanza kutupatia story yako ingemake cense sana
Mkuu, kwa sasa nipo stage ya za kutengeneza hiyo legacy. Bado ni mapema, ila nimeanza. Kusimulia sasa ni sawa na kushangilia ujauzito kabla mtoto hajazaliwa. But somethings interesting is going on. Let us all be blessed.
 
Enzi zangu sketi ilikuwa hainipiti
Huu ndio ukweli au maana ya kuishi ktk dunia hii ya Mungu,ila tegemea michango michache sana na haswa kwa vijana wetu waishi kwa kutegemea zali la "MENTALI"Tena wasio na msamiati wa SUBIRA ktk ufahamu wao!Ila tuschoke kukumbushana haya pale tupatapo fursa na nafasi ili pia iwe sehemu mojawapo ya simulizi kwa watoto au wajukuu wetu!
Naamini pia wazo hadimu kama hili ni fundisho tosha kuwa humu ndani kuna watu wa tabaka na daraja mbali mbali walio na makusudi ya kushirikishana mambo ya msingi yaliokosekana sehemu zingine!Mawazo kama haya yanafanya Mtandao huu uheshimiwe na wale wanao tumia muda mwingi kushughulika na mambo yasiyo na cha kujivunia sasa na hata baadae!
Hongera sana mkuu!!!!!!!!!!!
 
Passport yangu ina mihuri ya kutosha ni simulizi tosha wakibisha tu nawatolea kabatini maana wajukuu wa siku hz wabishi kama nn
 
Mungu anisaidie niweze kutumia mda Wang vizur kila siku nizidi kuwa bora zaidi ya jana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…