BUSARA ZANGU
JF-Expert Member
- May 5, 2013
- 779
- 1,269
Heshima kwenu wakuu
Leo ni siku nyingine, na mada nyingine mezani. Katika Maisha yetu naamini tumewahi kukaa na wazee ama watu waliotuzidi umri ambao wametusimulia mengi yaliyotokea kwenye maisha yao. Mengine mazuri, mengine hawataki hata kuyakumbuka.
Naamini ipo siku tutakuwa watu wazima ama wazee Mungu akitujalia uzima. Je tunataka tuwasimulie nini watoto ama wajukuu zetu? Kuna mzee mmoja aliwahi kunisimulia jinsi alivyokataa kiwanja/eneo sinza miaka ya 1980 akidai ni porini,wakati huo anadai mpaka sungura walikuwepo maeneo ya sinza. Je wewe sinza yako ya leo ni ipi? Chaka gani ambalo unalidharau na hutaki eneo hata bure? Ndugu, ardhi inapanda thamani kila leo. Tengeneza stori nzuri kwa wajukuu zako.
Mimi nataka niwasimulie jinsi nilivyoanguka mara 20 kwenye biashara zangu tofauti kabla sijasimama na kuanza ku make katika biashara zangu. Sitaki kusimulia wajukuu zangu jinsi nilivyoanguka kwenye biashara nikaona bora niajiriwe.
Utawasimulia nini wajukuu watakapokuuliza mbona wewe huna hela kama yule rafiki yako tajiri ambaye kila siku unawaambia wajukuu zako kwamba mlisoma naye. Je utawaambia Mungu ndio amempa yeye na amekunyima wewe? Je utamwambia huna bahati?
Je utawasimulia jinsi ulivyokuwa unazichanga na kujenga mpaka ukajenga nyumba ya 1,2......8....ama utawasimulia jinsi kiinua mgongo kiivyosaidia kumaliza nyumba yako kwa tabu?
Je utawasimulia jinsi ulivyokuwa cha pombe, mpenda mademu na namna ulivyowala.
Tafuta stori nzuri kaka. Tafuta stori nzuri dada ya kusimulia wajukuu/watoto wako. Andaa maisha yako sasa hivi ili uwe na stori tamu kuhusu maisha yako na uache legacy nzuri (sijui Kiswahili chake).