New Designer
JF-Expert Member
- Aug 8, 2025
- 551
- 879
Habari wakuu,
Nimekuwa nikifuatilia na kushiriki mijadala mbalimbali hapa JamiiForums, nikijaribu kutoa ushauri na mawazo ya kuboresha sekta ya teknolojia na maendeleo ya kidigitali. Katika muda huu, nimegundua jambo moja ambalo linaweza kuuwa kiwanda cha teknolojia nchini.
Kwa bahati mbaya, matukio yanayoendelea ya utekaji, vitisho, na uhalifu dhidi ya watu, yameanza kuvuruga kwa kiasi kikubwa imani ya wananchi na wadau katika mwelekeo wa kidigitali wa nchi yetu.
Wengine wamelengwa kwa sababu ya mawazo yao, wengine kwa sababu ya kazi zao katika vyombo vya habari au nafasi zao katika jamii. Haya yote yanazalisha hofu, ambayo inaua ubunifu, inazuia mjadala wa wazi, na inafanya vijana wengi wenye vipaji katika teknolojia kushindwa kujiamini kutumia majukwaa ya kidigitali kwa uhuru. Mfano kushauri, kuonesha ubunifu mpya, n.k
Sekta ya teknolojia haiwezi kukua kwenye mazingira ya hofu,
Mwekezaji, mbunifu au mtaalamu wa IT anahitaji uhakika wa usalama — sio tu wa data, bali wa maisha na uhuru wake wa kufikiri. Wakati wananchi wanapoteza imani na mfumo wa usalama, hata teknolojia bora zaidi haina nafasi ya kustawi kila kitu wanaona ni utekaji tu,
Matukio ya uhalifu pia yanaathiri taswira ya nchi kimataifa, jambo linaloweza kuwatisha wawekezaji wa sekta ya kidijitali na kupunguza.
Kiwanda cha kidigitali nchini kipo katika hatari kubwa sana hasa kipindi hiki.