Utekaji unavyofanyika hatua kwa hatua


Ila pia kuna watu wana akili zao hawataki wajinga watuletee tabu halafu nchi iharibike. Wanasema ukweli. Ingawa ukweli mpaka ueleweke inachukua muda mara nyingine.

Naamini tunaanza kujivua gamba. Tutaanza kuchagua viongozi kwa kuangalia uwezo wao na sio sura zao. Sura zimetudanganya.
Tunahangaika maana tumekwama. majuto mjukuuu
 
Actualy hawaruhudisiwi wakiwa bado ni active members of the army, wakishatoka huko wanaruhusiwa. Mpaka kugombea

Ni sheria na zipo wazi
 
Umemaliza kila kitu.

Hivyo ndivyo ilivyo.
Bandiko lako hili ni darasa huru, kila mtu anapaswa kulielewa somo hili, ingawaje najua kwamba "wale jamaa' huko waliko watakuwa wanakukata jicho baya sana kwa sababu hili bandiko lako ni Kama vile 'umeuza ramani yao ya Vita kwa maadui zao.'
 
Hakika Mungu atawaangamiza....
 
Andiko la mtoa mada linajieleza, anguko likikaribia, uovu ukifikia mwisho, basi dalili zake ndo hizo.....
 
Sehemu ya pili na ya mwisho
Zimwi likujualo halikuli likakwisha (likakumaliza)
Tawala nyingi dhalimu huanza vema kabisa lakini kadiri zinavyozidi kukaa madarakani hunogewa na kuanza kuharibu
Sasa badala ya kujisahihisha wanapokosea wao huanza kushughulika na wanao wakosoa.. Mwanzoni hutumia sheria kwa majibu wa katiba lakini baadae hutunga sheria kandamizi ili kuwalinda na mwishowe huanza kuteka na kupoteza wakosoaji wake
Japo ni mabaya sana haya lakini kidogo hao dhalimu huwa na woga pia.. Wanafanya kwa tuo
Shida inakuja pale ambapo wakiwa madarakani wakapata marafiki wabaya wenye nia ovu
Hawa huja kwa mlango wa Urafiki na kukusaidia hapa na pale.. Sasa ukikubali tu kumkaribisha umekwisha
Kwa ghiliba na utapeli atachukua kila anachoona kinamfaa kwenye kaya yako na kwakuwa atakuwa amekufunga mdomo na mikono kwa gia ya urafiki na misaada anayokupatia unakuwa huna jinsi bali kumsikiliza yeye tuu. Mwishowe unakuwa mateka wake
Kuna Wakati kuna tawala zinasoma alama za nyakati na kuamua kutaka kuondoka lakini zinashindwa kutokana na kuwa mateka wa marafiki Wwabaya
Hawa wanatambua fila ukiondoka wewe nao wamekwisha, sasa wanaweza kukusaidia kubaki madarakani hata kwa mtutu wa bunduki na kufadhili makundi ya kuteka na kuua kila anayeonekana ni tishio kwako
Kibaya zaidi ni kwamba wao hawaonekani wamejificha nyuma yako.. Kwahiyo ubaya wote utakujia wewe! Lakini kufikia hapo huna namna maana umeshatekwa .. Meno NINGEJUA huja mwishoni na majuto mengi
Mungu baba IbarikiTanganyika na watu wake wote... Wema na wabaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…