Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 593
- 1,376
"Mbona Polisi mnawaonea sana watu maskini, mtu ametekwa miaka mitatu iliyopita, eneo lake limechukuliwa na mtuhumiwa mnayemjua na kujengwa kiwanda lakini hamchukui hatua yoyote".
"Basi kama mnashindwa kumtafuta mtu aliyetekwa, mmeshindwa hata kutenda haki kwa kumrudishia eneo lake ambalo Takukuru imethibitisha kwamba wanalimiki kihalali mjane wake? Hapana msifanye hivyo"!
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amethibitisha kuitambua kesi hiyo na kubainisha kuwa Jalada la Kesi hiyo iliyofunguliwa miezi mitatu iliyopita lipo kwa Mwedesha Mashitaka Mkuu wa Serikali DPP.
Hoja hizo zimemfanya Katibu wa NEC Itikadi Uenezi na Mafunzo CCM Paul Makonda kushikwa na simanzi, kulia na kushindwa kuendelea kusikiliza kero za wananchi wa Tinde Mkoani Shinyanga.
Clouds TV