Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Mradi wa Uzalishaji wa Sukari Mbigiri ambao unamilikiwa na kampuni tanzu ya Mkulazi uliyopo Wilayani Kilosa, Mkoani Morogoro una lengo la kuzalisha sukari tani 50,000 kwa mwaka. CAG alibaini mapungufu katika utekelezaji wa mradi huu kama ifuatavyo;
a). Kampuni ya Mkulazi kushindwa kusimika mtambo wa kuchakata sukari kwa wakati. Hii ni kinyume na mkataba wa mwaka 2018 uliosainiwa kati ya kampuni ya Mkulazi, Benki ya Azania na Chama cha Ushirika cha Kati cha Magole uliokuwa na lengo la kukuza mnyororo wa thamani wa sukari kwa kuanzisha mahusiano baina ya wakulima, benki na kampuni.
Kulingana na mkataba, kampuni ya Mkulazi ilitakiwa kusimika mtambo wa kuchakata sukari ili benki iweze kutoa mkopo kwa wakulima. Hadi mwezi Disemba 2020, kampuni ya Mkulazi ilikuwa haijasimika mtambo huo wakati wakulima walikuwa wameshaanza kulima miwa na imeshakomaa kwa matumizi ya utengenezaji wa sukari.
b) Kampuni ya Mkulazi haikuweza kusimamia utendaji wa wakulima wanaouzunguka mradi kwa kuwapatia ushauri wa kiutaalamu ili kuhakikisha uwepo wa miwa ya kutosha na yenye ubora kwa ajili ya kiwanda. Hii ni kinyume na Sera ya kilimo ya mwaka 2013 inayotaka kila unapofanyika uwekezaji mkubwa wa Kilimo kuhakikisha kwamba unawanufaisha wananchi wa eneo linalozunguka uwekezaji huo.
Ripoti ya Uwajibikaji 2021.