Utekelezaji wa Adhabu ya kifo Tanzania uwe kwa namna hii...

Utekelezaji wa Adhabu ya kifo Tanzania uwe kwa namna hii...

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
3,250
Reaction score
5,509
Tanzania ni moja ya nchi inayofuata misingi ya haki kwa watu wake na moja ya haki aliyonayo mtu ni HAKI YA KUISHI. Siku zote haki haiombwi ila inatekelezwa baada ya mtu kutimiza wajibu wake kwa sheria na katiba ya nchi husika.

Haki ya KUISHI ni hitaji la katiba lakini kuheshimu sheria na katiba ni wajibu wetu. Hapa ndio tunajiuliza swali la: Je, mtu aliyeasi katiba na kuvunja sheria kwa kiwango kikubwa bado anakuwa na haki ya KUISHI ?

Tukienda kiimani zaidi jibu ni ndiyo kwa sababu vitabu vya Imani vyote vinakata kuua na utekelezaji wa Adhabu ya kifo ni kuua lakini kiutawala ni hapana kwa sababu utawala unatakiwa kulindwa kwa jasho na damu na katika kuulinda huko utawala utekelezaji wa Adhabu ya kifo ni muhimu. Ninaposoma utawala kwa faida ya Uzi huu namaanisha Nchi.

Licha ya kiutawala adhabu ya kifo ni jibu la kusimamia kikamilifu sheria na katiba lakini bado watawala wana Imani na hapo ndio utekelezaji unakuwa ni mgumu.

Hapa ndio nimepata wazo la njia ya utekelezaji wa Adhabu hii.

Kwanza, katika nchi yetu anayesaini utekelezaji wa Adhabu ya kifo ni Rais wa nchi na hapo anasaiani baada ya mchakato mzima wa hukumu na rufaa kukamilika.

Kwa kuwa Rais ni binadamu na mwenye kufuata Imani utekelezaji wa Adhabu hii mara nyingine unaweza kuwa mgumu hivyo nashauri utekelezaji uwe kwa namna hii:

Baada ya hukumu na rufaa kumalizika na mtu kuhukumiwa adhabu hii, mahakama itengeneze mfumo maalumu ambao KAZI kuu ya mfumo humo ni kushirikisha Umma katika utekelezaji wa Adhabu hiyo

Kupitia mfumo huo , watu wanajisajili ambao wana miaka 18 na zaidi na hao watu waliojisajili ndio wanakuwa watekelezaji wa mfumo huo.

Baada ya mahakama kumhukumu mtu adhabu ya kifo ,mfumo unafunguliwa watu wanapiga kura ili anyongwe au asinyongwe na kama wengi wakisema anyongwe basi utekelezaji ufanyike. Kwa kifupi utekelezaji wake ufanye na watu PUBLIC EXECUTION POLL

Kwa kufanya hivi:

Itasaidia Rais kupunguziwa mzigo wa kufikiria kutekeleza adhabu hii.

Siku zote adhabu ya Umma ni adhabu ya haki hivyo hata wanaopanga kufanya uhalifu watakuwa wanahofia adhabu ya Umma.

Watu watakuwa wamepewa wajibu wa moja kwa moja kuulinda na kuhukumu pale sheria na katiba yao inapovunjwa

Watu watakuwa walinzi wa katiba yao.
 
Back
Top Bottom