Sami Omary Khamis
Member
- Sep 8, 2020
- 67
- 133
Na Bwanku M Bwanku
Fursa za ajira ni eneo muhimu sana katika kukuza maendeleo ya kiuchumi na kijamii ambapo jamii hususan vijana hupewa nafasi ya kuchangia utaalam wao katika kufanya kazi ili kuchangia kukuza maendeleo ya Taifa. Serikali iliyoundwa na CCM katika miaka mitano iliyopita iliweka nguvu kubwa sana kwenye sekta ya ajira ikiwa ni pamoja na kutoa nafasi nyingi sana za ajira, kuongeza ujuzi kwa vijana, kulinda ajira za wazawa na kutekeleza mipango na mikakati mikubwa ya kuongeza ajira nchini.
Kwa kazi kubwa iliyofanyika, Sura ya pili ya Ilani ya CCM, kipengele cha 31 ukurasa wa 26-29 umeeleza kwa kina mafanikio makubwa yaliyopatikana kutoka mwaka 2015-20 kwenye utoaji wa ajira nchini ikiwemo:-
(a) Kuongezeka kwa ajira kutokana na kukua kwa uchumi katika sekta mbalimbali za uzalishaji na utoaji huduma ambapo takribani fursa za ajira 6,032,299 zimezalishwa katika sekta rasmi na zisizo rasmi. Kati ya hizo, ajira 1,975,723 zimezalishwa kwenye sekta rasmi ya umma na binafsi na ajira 4,056,576 kwenye sekta isiyo rasmi.
(b) Mikopo ya masharti nafuu yenye thamani ya shilingi bilioni 17.9 imetolewa kwa vikundi vya vijana 535 vyenye wanachama 3,745 ili kuwawezesha vijana hao kupata mitaji ya kuanzisha biashara.
(c) Mfuko wa Maendeleo ya Vijana unaochangia asilimia nne ya mapato ya ndani ya mamlaka za serikali za mitaa umetoa shilingi bilioni 14.7 kwa vikundi vya vijana 2,026 vyenye wanachama 20,260.
(d) Vijana 67,243 wamepatiwa mafunzo katika maeneo ya kukuza ujuzi na stadi za kazi katika ujenzi, kurasimisha ujuzi uliopatikana kwa mfumo usio rasmi, ujasiriamali na kurasimisha biashara.
(e) Wahitimu 5,975 wamepatiwa mafunzo kwa vitendo mahali pa kazi katika fani walizosomea na vijana 1,827 wamepata ajira kutokana na uzoefu walioupata.
(f) Halmashauri za wilaya 111 zimetenga maeneo yenye ukubwa wa ekari 217.8 na kuwezesha vijana kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo, ufugaji, biashara na viwanda.
(g) Makampuni 217 ya vijana yameanzishwa ambapo kati yake makampuni 76 yamethibitiwa na kupewa kibali cha kuomba zabuni za Serikali.
(h) Kupitia programu ya stadi za maisha kwa vijana walio nje ya shule ambapo wawezeshaji wa kitaifa 78 wameandaliwa na kutoa elimu hiyo kwa vijana 12,500 kwa njia ya Elimu Rika.
Zaidi Sura hiyohiyo ya pili ya Ilani ya CCM kwenye kipengele cha 31 kimeonyesha mafanikio makubwa ya utoaji wa fursa za ajira kwa miaka mitano iliyopita kutokana na utekelezaji mkubwa wa miradi ya kimkakati kama ifuatavyo:-
(a) Mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge hadi 2020 ulikuwa umetoa ajira 14,139.
(b) Mradi wa Ubungo Interchange hadi mwaka 2019 ulikuwa umetoa ajira 502.
(c) Upanuzi wa Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere kwa Kujenga Terminal III ambao ulitoa ajira 1,056.
(d) Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere ambao hadi mwaka 2020 ulikuwa umetoa jumla ya ajira 3,412
Nani kama CCM? Twende tukafanye maamuzi yetu Oktoba 28.
TUMETEKELEZA KWA KISHINDO, TUNASONGA MBELE PAMOJA.