Janeth Thomson Mwambije
Member
- Apr 11, 2024
- 24
- 55
Nilifanikiwa Kutembelea Ofisi Ya Kata Ya Kivule, Iliyopo Wilaya Ya Ilala, Mkoa wa Dar Es Salaam, Ili Kuweza Kupitia Taarifa Ya Utekelezaji wa Ilani Ya Chama Cha Mapinduzi Kwenye Kata Ya Kivule Iliyotekelezwa Kwa Muda Wa Juni - Disemba 2024, Kwa Mapato Ya Ndani - Halmashauri Ya Jiji La Dar Es Salaam
Miongoni Mwa Utekelezaji wa Ilani Ya Chama Cha Mapinduzi Kwenye Kata Hii Ni Pamoja Na;
- Ukarabati wa Madarasa Kumi na Mbili (12) Katika Shule Ya Sekondari, Misitu Iliyogharimu - 174,600,000/=Tshs
- Ununuzi wa Madawati na Meza, Mia Hamsini, Katika Shule Ya Sekondari Misitu, Iliyogharimu - 12,000,000/=Tshs
- Ujenzi wa Choo Chenye Matundu Ishirini, Katika Shule Ya Juu Ya Upili (Advance), Inayotegemewa Kuanza Hivi Karibuni - Kivule, Iliyogharimu - 46,000,000/=Tshs
Pamoja na Ununuzi wa Viti na Meza Mia Tatu Sitini (360), Iliyogharimu - 28,800,000/=Tshs
- Umalizaji wa Ofisi Ya Walimu Katika Shule Ya Sekondari Abuuy Jumaa, Ambayo Mpaka Sasa Imeshapokelewa - 50,000,000/=Tshs Kwenye Akaunti Ya Shule Ya Sekondari Abuuy Jumaa, Na Taratibu za Ujenzi Zinaendelea
- Ujenzi wa Choo cha Matundu Kumi (10) Katika Shule Ya Msingi Misitu, Iliyogharimu - 20,000,000/=Tshs
- Ujenzi wa Choo cha Matundu Kumi (10) Katika Shule Ya Msingi Serengeti, Iliyogharimu - 20,000,000/=Tshs
- Ununuzi Ya Madawati Mia Mbili Hamsini (250) Katika Shule Ya Msingi Serengeti, Iliyogharimu - 20,000,000/=Tshs
- Ununuzi Ya Madawati Mia Mbili Hamsini (250) Katika Shule Ya Msingi Kivule Annex, Iliyogharimu - 20,000,000/=Tshs
- Ununuzi wa Madawati Mia Tatu (300) Katika Shule Ya Msingi Kivule, Iliyogharimu - 24,000,000/=Tshs
- Ununuzi wa Madawati Mia Mbili Hamsini (250) Katika Shule Ya Msingi Bombambili, Iliyogharimu - 20,000,000/=Tshs
- Ujenzi wa Kituo cha Polisi, Ambacho Mpaka Sasa Kimepauliwa, Na Mpaka Sasa Kimegharimu - 80,000,000/=Tshs
- Utengenezaji wa Bicon Elfu Ishirini na Nne (24,000), Kwa Ajili Ya Urasimishaji Makazi, Iliyotegemea Fedha Kutoka Serikali Kuu - 120,000,000/=Tshs
- Ujenzi wa Daraja Kwa Msumi (Bombambili) Na Ujenzi wa Barabara Ya Changarawe Ya Kilomita Moja Nukta Tano (1.5), Iliyogharimu - 957,060,400/=Tshs
- Ukarabati wa Barabara Ya Kivule Makonde (Mnarani) Ya Kilomita Tatu (3Km), Iliyogharimu - 44,950,000/=Tshs
- Ukarabati wa Barabara - Kutoka Kivule Fremu Kumi Kwenda Kivule Makutano Ya Kwenda Hospitali Ya Wilaya, Kilomita Mbili Nukta Tano (2.5Km), Iliyogharimu - 24,600,000/=Tshs
- Ukarabati wa Barabara Kuelekea Hospitali Ya Wilaya Kivule, Kilomita Moja (1Km) - 46,286,800/=Tshs
- Ukarabati Wa Barabara Ya Kivule - Mzunguko Kwa Mbondole (Midomo Miwili, Mitaro, Kifusi, Kingo za Mawe, Na Ujenzi wa Karavati Mwanzo Mwema), Iliyogharimu - 44,700,000/=Tshs
- Ujenzi wa Barabara Kutoka Kwa Diwani Kwenda Bombambili Kwa Osama, Kumwaga Vifusi na Kukwangua - 52,000,000/=Tshs
- Hakuna Wanafunzi Wanaokaa Chini
- Ushindi wa Chama Cha Mapinduzi Kwa Wagombea Wote wa Nafasi Ya Mtaa Kuanzia Wenyeviti, Wajumbe na Viti Maalumu wa Chama Cha Mapinduzi, Kwenye Mitaa Yote Minne Ya Kata Ya Kivule (Kerezange, Kivule, Bombambili na Magole)
Kazi Zinazotarajiwa Kuanza Kutekelezwa Ndani Ya Mwaka 2025 Kwenye Kata Hii Ya Kivule, Ni Pamoja Na;
- Ujenzi wa Shule Ya Msingi Ya Mchepuo wa Kuiingereza, Ambayo Mpaka Sasa Imeshaingizwa 450,000,000/=Tshs Kwenye Akaunti Ya Shule Ya Msingi Kivule
- Ujenzi wa Barabara ya Kivule Kwenda Msongola, Ya Kiwango cha Lami
- Umaliziaji wa Majengo Mbalimbali Ya Hospitali Ya Wilaya - Kivule
- Umaliziaji wa Kituo cha Polisi
- Ujenzi wa Chuo Cha Uuguzi na Mabweni ya Wanachuo Kwa Wanafunzi wa Kike na Kiume
- Ujenzi wa Masoko Mawili Ya Kivule Stendi na Kerezange, Ambayo Yanategemewa Kuwa Chini Ya Dar es salaam Metropolitan Development Project (DMDP)
- Ufidiaji wa Eneo la Ujenzi wa Shule ya Msingi - Magole A
- Ujenzi wa Shule Ya Msingi Ya Magole, Mpya
- Ujenzi wa Barabara Kutoka Makonde Kwenda Magole A
Nawapongeza Sana Wananchi wa Kata Ya Kivule, Kwani Mafanikio Hayo Ni Mchango wa Kodi Zao, Naipongeza Serikali Ya Jamuhuri Ya Muungano wa Tanzania, Chini Ya Daktari Samia Suluhu Hassan...Naupongeza Uongozi wa Halmashauri ya Jiji La Dar Es Salaam - Wilaya Ya Ilala... Naipongeza Ofisi Ya Mbunge wa Jimbo La Ukonga, Mhe. Jerry Silaa, Naupongeza Uongozi Mzima wa Kata Ya Kivule, Chini Ya Mheshimiwa Diwani. Nyansika Getama, Pamoja Na Wanachama Wote wa Chama Cha Mapinduzi
Hakika Faida Ya Konekshen Imeonekana ... CCM IPO KAZINI.... 🇹🇿
Naomba Kuwasilisha ✍️
Wenu Katika Ujenzi wa Taifa,
Janeth Thomson Mwambije
Mjumbe wa Mkutano Mkuu Mkoa - Wilaya Ya Ilala - UVCCM - DSM 🔰
#CommittingToSa💯
#KAZI IENDELEE 🇹🇿