Jana usiku umeme uliisha kwenye mita yangu. Nikanunua shilingi elfu 9 kwa tigopesa, nashangaa muamala unasitishwa kila naponunua. (Ninatumia tarrif ya chini ile) umeme wa elfu 9 unanitosha kwa mwezi mzima.
Ikabidi nipige simu tigo, wakaniambia kuwa mita inadaiwa shilingi laki 1 deni ya kodi ya majengo kwa mwaka 2022/23, kwa hiyo ninunue umeme wa kuanzia Tshs. 100,000/= ndio itakubali.
Kwa kweli nimeshangaa na kusikitika sana. Nyumba ni andagraundi, imehesabika kuwa ni ghorofa, na muda wote nilikuwa nalipa elfu 1 kila naponunua umeme.
Sasa hii ya kufungia mita ili ninunue umeme wa laki kwa kweli ni uonevu, hapa ndio nimeelewa kwa nini wafanyabiashara wa Kariakoo waliandamana. Halafu mwaka 2022/23 unaisha mwezi huu, Juni 30, maana yake nitalipa laki na mwezi wa 7 watanifungia tena ili nilipe laki ya mwaka 2023/24..kisa vyumba viwili vya andagraundi.. TRA hapa mnazingua, mnachofanya ni wizi.