Utekwaji wa mabasi ya abiria: Imewahi kukukuta hii?

Utekwaji wa mabasi ya abiria: Imewahi kukukuta hii?

Duuu, wewe utakuwa mzee mwenzangu,make kwa kipindi hicho cha utekaji Karagwe hapo unaongelea miaka 93's to 98's enzi za Wakimbizi na kabla ya wakimbizi tokea Rwanda na Burundi.
Kipindi hicho Kimisi inatisha,Uzuri wa Kondoo inatisha,Kwenda Bushangaro njia ni hatari,Mlima Rwabunuka ni pata shika.
Majambazi maarufu kipindi hicho kulikuwa na Mwaarabu mmoja matata anaitwa SIRAJ,kwake Omurushaka,alifia jela la Kitengule baada ya kukamatwa kwenye sekeseke la kuua wazungu Kimisi,
Kulikuwa na majambazi wengi maarufu ambao sasa ni matajiri wakubwa waliohamia maeneo ya Mwanza,Kahama na kadhalika,siwezi kuwasemea hapa kwani baada ya wengi kutoka jela waliokoka na kuendelea na maisha mengine mikoa mingine.
Kuna lijamaa lingine lilikuwa linamiliki costa za kutoka Karagwe to Bukoba enzi hizo zenye jina la kuanza ZFNN[emoji23][emoji23],HATARI sana.Enzi hizo tupo Sekondari but jioni unaogopa kutembea usiku kwa kumuogopa SIRAJ.
WEWE mtoa mada utakuwa ulisoma Karagwe Secondary (KARASECO)Make ndo ilikuwa shule bora kwa Karagwe ya KKKT enzi hizo,ikifuatiwa na Kaisho Sec na shule bora ya Serikali ilikuwa Bugene Day Sec School.

Sent from my SM-G531H using JamiiForums mobile app
Nilisoma shule moja la kibabe sana linaitwa St. Bernard [emoji23] iko imepakana na seminary ya kido halafu advance nikasoma shule tena ya kibabe bugene day my brother alikuwa kaisho enzi za magabilo wanafunzi waligoma wakachoma moto shule [emoji23][emoji23][emoji23][emoji1373]
 
Back
Top Bottom