kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Maisha yamepanda, maisha ni magumu na hali ni mbaya sana kwa watawala katika kipindi hiki. Ni vigumu kuwashawishi wapigakura kuwa hali hii nguvu ni kwasababu ya vita ya Ukraine na Russia na sio uzembe na ufujaji wa viongozi wao. Kilichomwangusha Raila kwenye sanduku la kura ni kuungwa mkono na Raais kenyatta kwenye kampeni zake. Nchi yoyote duniani itakayofanya uchaguzi wake kwenye kipindi nchi lazima watawala watashindwa tu, bila kujali nchi hiyo iko bara gani.
Hata hivyo, ni vigumu sana wale watakaoshinda kwenye chaguzi kipindi hiki kupata uungwaji mkono kikamilifu na mataifa ya Magharibi ikiwemo marekani, maana kupata ushindi kwenye kipindi hiki ni sawa na kuunga mkono Russia. kama ukimsikiliza vizuri William Ruto sera zake ni kama vile za kijamaajamaa za kila kitu bure.
Nchi za magharibi haziamini kwenye kutoa huduma bure kwa wananchi kama matibabu na elimu ya juu maana hii itapunguza idadi ya cheap labour kwenye mashamba, viwanda na biashara zao.
Wanaamini kuwa kama mtu atakuwa na uhakika wa kutibiwa bure na kuwa na elimu kubwa atakuwa na uwezo mkubwa wa kuchagua kazi na kujadili malipo. Sina uhakika kama Ruto atapewa Urais pale kenya kwenye miradi mingi ya Magharibi.
Ili watawala waeleweke kwa wananchi ni kuacha kupata faida za kiuchumi kwenye kipindi hiki. Yaani watangaze hatua kama kufuta posho za wabunge kwa muda, kusimamisha nafasi za ubunge wa viti maalum, kusimamisha tozo za miamala, serikali kupiga marufuku matumizi ya magari makubwa kwa watumishi na viongozi wote, kutangaza kusitisha safari za nje ya nchi ili kubana matumizi, nk. hatua kama hizo ndizo zinazoweza kuwapa imani wananchi kwamba kweli hali hii ngumu iko nje ya uwezo wa serikali yao, vinginevyo hawawezi ku associate kati ya vita ya ukraine na hali nguvu kwao tu.