Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Awamu iliyopita ilikuwa ngumu kiutawala na ilihitaji ujasiri kusimama na kubaki kwenye nafasi ya juu ya uteuzi. Dr. Anna Makakala Ni mmoja wa wanawake waliovumilia nakupambana kwa miaka mitano ya awamu hiyo bila kutumbuliwa.
Kila ukiangalia picha za awamo ya tano utabaini alipokuwa Rais na huyu mama na wakuu wengine wa vyombo vya ulinzi walikuwa naye. Maana yake aliweza kusafiri mchana na usiku kutetea kibarua chake. Hongera sana.
Sasa hivi ni muda wa Rais wa awamu ya sita kutebgeneza safu yake. Naamini yupo mbioni kuteua wakuu wa vyombo kwani waliopo sura zinasadifu kwamba wapo ukingoni. Lakini pia Ni haki yake kina na damu mpya kiutawala nakuruhusu mawazo mapya.
Dkt. Makakala anaweza akabaki au asibaki kwenye nafasi yake ila tuna budi kumpongeza kwa kazi aliyofanya. Nikipitia mitandaoni naona ni kipindi chake ndicho huduma za Uhamiaji ziliimarika namalalamiko yakapungua sana. Yeye Kama mwanamke mwenzetu kwa kweli amewafumbua macho wanaume kwamba wanawake wanaweza bila hata kuwezeahwa.
Tuliaminiwa kwenye sekta nyingine ila kwenye vyombo vya ulinzi ilikuwa bado, Sasa naamini Makakala ametupa mwanga na kutujengea imani kwamba tunaweza bila kuwezeahwa.
Nimwombe Mhe. Rais atusaidie kupata wanawake katika nafasi za juu za vyombo vyetu nikimwakikishia Kama Makakala aliweza katika mazingira ya hakuna kulala Basi watakaoteuliwa Sasa watafanya zaidi.
Tunapenda kuona luten General au meja general au hata CDF akiwa mwanamama.
IGP au Makamishna wa polisi Magereza na zimamoto tuwaone wanawake kwani naamini Wana sifa na maarifa yakuongoza vyombo hivi.
Dkt. Makakala umetuheshimisha, wanawake wengine mtakaopewa nafasi nilizoomba hapa msituangushe, kasimamieni kazi bila kutanguliza tamaa Wala kuonea watu.
Wanawake wanaweza bila hata kuwezeahwa.