Utendaji wa wataalamu wetu wa afya hauridhishi

Pole sana mkuu lakini kwa tatizo la pumu mtoto akitumia nebuliser asubuhi kabla hajakwenda shuke na usiku kabla hajalala si rahisi kupata attacks. Si anazo zote mbili ya blue na brown?

Turudi kwenye mada ni kuwa hakuna medical negligence claims, bill ikiwafikia watawajibika.
 
Nilikuwa bado sijapewa wakati huo ila kwa sasa ninazo,alikuwa anawekewa ile ya hospitali,kimashine flani kinafunika pua halafu anawasha kinatumia umeme ndani yake kunakuwa kama kuna maji yanachemka...
 
Nilikuwa bado sijapewa wakati huo ila kwa sasa ninazo,alikuwa anawekewa ile ya hospitali,kimashine flani kinafunika pua halafu anawasha kinatumia umeme ndani yake kunakuwa kama kuna maji yanachemka...
Ile ya hospitali sasa ndiyo nebuliser, hii ya blue na brown ni pump.
 

Huduma mbovu ni tatizo la ofisi karibia zote za umma.

.................Bora hata ukutane na mhudumu wa kiume dada zetu wamekuwa wa moto.
 
Issue kubwa nlioona ni uhaba wa watumishi hasa hospitali zinazohudumia wananchi wanyonye kwa ngazi ya wilayaa

Sikubali kabisa swala la kupiga wajawazito lakini situation ndo zinazosababisha wanakutana na hayo

Namfano haii nmeona mwenyewe kutoka hospital moja apa nchini ya wilaya

Wadi ya wazazi ina

#Antenatal kuna wagonjwa wanaitaji huduma
#Post natal kuna wagonjwa wanaitaji huduma
#Post operative kuna wagonjwa wanaitaji huduma
#kangaroo mother care kuna wagonjwa wanaitaji huduma

#Kubwa kabisa kuna labor unit wanakojifungua
Wapo wanaitaji huduma ya haraka


IYO WARD NA SEHEMU ZOTE IZO NLIZOTAJA ZINA WAUGUZI WAWILI TU IMAGINE

na ikitokea emergence operation anatoka muuguzi mmoja kuenda kuchukua mtoto na kufanya neonatal resuscitation ikihitajika kwaiyo anabaki mmoja

Uyo mmoja ndo atasimamia kote kule alafu inatokea mama analeta masihara kwenye kujifungua apo hakuna cha ziada hata akila kofi au ahatarishe maisha yake na mtoto kitu ambacho ikitokea hakuna atakae mtetea uyo muuguzi zaidi ya kumbebesha mzigo

Ivo tusiwalaumu sana mana pamoja na kula makofi wengi wanarud nyumbani na tabasamu zito la kupata mtoto hai mwenye afya nzur


Niishie hapo leo kuna vingi watu hawajui kuhusu suala la kutoa huduma japo mapungufu yapo pia
 
Hii ni kutatarisha usalama wa wagonjwa nacwafanyakazi. Vyama vya wafanyakazi vinatakiwa kukemea mambo kama haya.
 
Sasa mkeo akizembea alafu asisukume mtoto akafa mnaanza tena kulaumu ma nurse....huko wanapojifungulia wajawazito ni sehemu ngumu sana kufanya kazi...humsukumi mtoto unategemea uchekewe,mtoto akifariki katika mazingira hayo lawama kwa madaktari
Mbona Private hawapigi watu na watoto wanazaliwa vizuri tu? Unapewa maneno mazuri ya kutiwa moyo pamoja na mbinu za kukusaidia usiishiwe nguvu hadi unajifungua salama.
 
Hii ni kutatarisha usalama wa wagonjwa nacwafanyakazi. Vyama vya wafanyakazi vinatakiwa kukemea mambo kama haya.
Hakuna anaependa kufanya ivo na bodi husika nadhani zinafanya kazi tatizo lipo kwenye uhalisia sio kulitizama kwenye maandishi
 
Heshima kwako muhenga wa JF
 
Hamna anayependa kufa, na kila mtu anajua ukishindwa kujifungua kinachofuata kama sio operation ni kifo. Na kupelekwa kwenye operation inategemea kama mtoto bado hajashuka chini na nyonga ikafunguka. Kila mtu anajua ukishindwa kujifungua ni either umpoteze mtoto, wewe mwenyewe ufe au wote. Sasa unafikiria kuna anayependa yamkute hayo? Unakuta mtu anajitahidi kadri ya uwezo wake lakini anashindwa hadi wengine wanazimiaga katika harakati za kujifungua.
 

Kuna mtu atakuambia wabunge ni watetezi wa uma, nchi hii vituko haviishi! Bado namtafuta sana aliyefanya maamuzi ya watumishi wa uma kulipwa hivi na wanasiasa kulipwa vile!
 
Nimeshangaa kuna afisa tabibu mtaani kwetu atafanya mtihani wa QT mwaka huu na kaajiriwa mwaka jana 2018 baada ya kumaliza chuo mwaka 2017, sasa sijui alijiunga chuo kwa vigezo gani maana kwa hesabu za haraka anatafuta cheti cha form 4

Huku mtaani watoto wanapigwa sindano na yeye ni majipu tu, Ukimu assess kwa changamoto kidogo tu au kuuliza ushauri ujue umetafuta ugomvi. Hawa ndo watoa huduma kwa jamii zetu unategemea nini!
 
Usione tu sekta ya afya bali hata ikulu inalo hitaji la kupanguliwa na hao waliopo wapelekwe tena darasani. Kama unaweza kukaa kimya kuhusu jambo la kukanusha tu nadhani hatujui tunalofanya au nafasi zetu hatuzijui
 
Kwa upande wangu kuna kada mbili imetokea tu huwa naona hawako friendly kabisa,ya kwanza ni Polisi na inayofuata ni Manesi hasa wakike.
 
Mbona Private hawapigi watu na watoto wanazaliwa vizuri tu? Unapewa maneno mazuri ya kutiwa moyo pamoja na mbinu za kukusaidia usiishiwe nguvu hadi unajifungua salama.
Huko private ratio ya wauguzi na wagonjwa iko vipi?
Unakuta wauguzi wawili wanamzalisha mgonjwa mmoja


Lakini huku serikali wauguzi wawili, wagonjwa 15 leba unaanzaje kuanza kubembeleza huku wengine nao wanasubiri kujifungua, wengine njia ya kawaida imeshindikana inabidi aandaliwe aende operation na wauguzi ni hao hao wawili
 
Tuishtaki wizara ya afya kwa kuhatarisha maisha ya raia. Upungufu wa wafanyakazi ni mkubwa mno. Licha ya upungufu wengi hawana nidhamu ya kazi.
 
Umemaliza kila kitu. Issue ya customer care Tanzania ni majanga. Tunahitaji kuweka somo hili mashuleni kufundisha customer care. Kwa kweli ni shida mno
Usilaumu sector ya afya tu customer care hapa Tz ni 0% neenda kila sector private na serikalini, unaweza ukafikiri kwamba wanalazimishwa kazi au hawalipwi mishahara kuna haja ya orientation seminar kwa watumishi wote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Taja hiyo wilaya aise. Huu ni unyama
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bongo kulalamika kwa vitu kama hivi hakusaidii sana. Solution ni moja tu: TAFUTA PESA.
Yaani tafuta pesa kiasi kwamba unachagua wewe utibiwe hospitali ipi, uonwe na daktari gani na upewe huduma na muuguzi gani.
Mimi hiyo solution (ya kutafuta pesa) ndo naifanyia kazi sasa hivi. Mwanzoni nilikua nalalama sana kama wewe mtoa mada, nilipogundua na differentiate constant, nika resort kwenye hiyo solution.Tatizo Watanzania wengi wetu wameshakubali "unyonge" na kazi ya mnyonge kubwa ni kulalama tu,na kuiomba msaada serikali.
Maana hizo hospitali za government kwanza ukianza kuelezwa matatizo yao,kama una roho nyepesi unaweza kuishia kutoa machozi.
Bottom Line:TAFUTA PESA
Alamsiki.
Sky Eclat
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…