Utengano na woga wa watanzania ndio nguvu ya Watawala kuendelea kuwa walivyo leo

Utengano na woga wa watanzania ndio nguvu ya Watawala kuendelea kuwa walivyo leo

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,455
Reaction score
5,134
Miaka kadhaa iliyopita nilisoma kitabu kimoja kilichokuwa na hadithi ya baba mwenye watoto 10, ambao kila mmoja alipoambiwa avunje fungu la vitiji 10 peke yake alishindwa ila pindi walipoambiwa wavivunje kwa pamoja vijiti hivyo 10 walivivunja kwa urahisi sana! NAAM Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.

Nimekumbuka kitabu hicho baada ya kujiona jamii yangu ya kitanzania nikiwemo na mimi mwenyewe jinsi tulivyo, hatuna Umoja hata pale unapohitajika umoja kuweza kuvunja vijiti ambavyo mtu mmoja pekee hawezi bali linahitajika kundi la Watanzania wote kuweza kuvunja vijiti hivyo ili tuweze kujikwamua kwenye mkwamo tuliomo.

Tunajikuta hatuna tofauti na wale panya walioitisha kikao kwenye kitabu kimoja cha zamani wakati wakitaka kumuwekea ishara paka ili akija wajue waweze kukimbia wasiliwe. Wakakaa kujadili Ni nani atamfunga paka kengele, akajitokeza panya madoa kuwa Jasiri ambaye alionyesha uthubutu wa kumsogelea Paka ila kwa bahati mbaya Panya wale wengine walikuwa na tabia kama za Watanzania wa juzi, jana na sisi wa leo, wakamkimbia mwenzao akaliwa!!!! Badala wangeungana kumsaidia kufikia lengo lao ila hofu na utengano wao vimewaponza mpaka leo wanaliwa na paka bila kupata suluhisho sababu ya uoga na kukosa umoja!

Je, Watanzania tutaendelea kuwa na utengano na woga mpaka lini? Tutanedelea kuwakimbia wanaojaribu kumfunga paka kengele mpaka lini? Au nasi tuendelee kuliwa na paka mpaka daima milele kwa kushindwa kuwa wamoja?

Siyo ajabu kwa watanzania kuwakimbia wanaojaribu kuonesha ari ya kuhitaji mabadiliko ya mifumo kandamizi kwa ajili ya Watanzania wanapojikuta wameingia kwenye mikono ya wenye mamlaka badala ya kusimama nao sisi tunaingia kwenye mashimo kama wale panya walivyomkimbia panya madoa.

Tukiwa wamoja na kuondoa hofu tutaweza kuwawajibisha watawala walioweka mifumo mibovu ya uchaguzi ili wao washinde, wanaoiba pesa za umma ili wao waishi kwa neema na nk
 
Tatizo la nchi hii, Ndugai ni mmoja tu, wangekua watano kingeeleweka tu,
Miujiza ya nchi yetu; Mbunge anasimama anampangia rais wake kwamba amchague majaliwa tena kuwa pm, that means matokeo ya uchaguzi tayali na rais amekwishashinda, majaliwa amekwishashinda na kama ndio hivyo basi uchaguzi wa nini kama sio matumizi mabaya ya pesa za umma?
 
Back
Top Bottom