Habari Wana JF
Tujifunze utengenezaji wa vyungu vya maua.
MALIGHAFI
1.MCHANGA
2.CEMENT
3.MWIKO WA KUJENGEA
4.UMBO
5.RANGI
6.VANISH (MAHOGAN)
JINSI YA KUTENGENEZA
Changanya MCHANGA 3 + CEMENT 2 weka maji uwe mchanganyiko kama wakupigia plasta.
Tandika Salfeti chini, chota mchanganyiko wako utengeneze chapati ya sentimita 3. Kisha toboa katikati ya hiyo chapati na ujazie udongo mkavu.
Jaza mchanga ndani ya umbo kisha weka umbo juu ya chapati. Anza kuchapia iache ikauke. Ikikauka mimina mchanga toa kiroba.
Chukua rangi nyekundu changanya na cement kisha paka chungu chako vizuri kwa uwiano, ikikauka paka vanish.
TAYARI KWA KUUZA
MAMBO YA KUZINGATIA
-Vanish zipo nyingi ulizia aina ya MAHOGAN
-UMBO- chukua kiroba kama cha unga nenda kwa fundi cherehani apitishie uzi pembeni na pembeni akitengeneza umbo la chungu unachotaka. Baada ya hapo jaza mchanga.
-Biashara hii haihitaji mtaji mkubwa wala fremu. Ni fursa nzuri...
Asante...
-Queen Chagga