UTENGENEZAJI WA MVINYO WA ROSELA
Mvinyo ni kinywaji kinachotengenezwa kutokana na juisi za matunda kama vile ndizi mbivu,machungwa,mapapai, mapera zabibu, malimao n.k, pia mvinyo unaweza kutengenezwa kwa kutumia juisi za matunda machanganyiko kama ndizi na karoti,zabibu na karoti na mchachungwa n.k
- MVINYO WA ROSELA
Mvinyo ni kinywaji kinachotengenezwa kutokana na juisi za matunda kama vile ndizi mbivu ,machunga ,mapapai,mapera ,zabibu,malimao n.k., pia mvinyo unaweza kutengenezwa kwa kutumia juisi za matunda mchanganyiko kama ndizi na karoti,zabibu na karoti na machungwa nk.
Ili kupata mvinyo ,kuna njia za kikemikali zinazoendelea wakati sukari na hamira vinapochanganyika vikasaidiwa na viambaupishi vingine vinavyotumika. viambaupishi vinavyotumika ni:
- VIFAA VITUMIKAVYO KATIKA KUZALISHA MVINYO
- Sufuria kubwa la kuchemshia juisi
- Chujio la plastiki au chuma cha pua
- Vyombo vya kuchachulia kama ndoo madumu nk.
- Mwiko wenye urefu wa kutosha
- Mirija ya kuchachulia
- Pima maji {hydrometer}
- Jagi la kuchukulia sampuli
- Chupa au kikombe cha kupimia majimaji chenye ujazo wa mililita 250 -500
- Kipimajoto
- Kipimatindikali
- Mizani 2,moja ya uzito wa gram 0- 250,nyingine kg 0-25
- Mrija wa kunyonyea wenye urefu wa mita 1.5
- Kitambaa cheupe cha pamba cha chujio {filter with filterpads}
- MAMBO YA KUZINGATIA
- Osha vyombo sawasawa mara tu ukimaliza kuvitumia
- Tumia hamira inayofaa
- Wakati wote yeyusha sukari ndio utumie kutengenezea mvinyo
- Usizidishe sukari unapoanza kuchachua
- Chuja mvinyo katika vipindi na wakati muafaka ongeza campden tablets {saga na kuyeyusha katika maji kidogo} kila wakati unapochuja.
- Usifungashe mvinyo kwenye chupa mpaka uhakikishe umechachuka inavyotakiwa.
Matumizi ya mvinyo
- Kinywaji -kuongeza hamu ya kula na sacrament kanisani
- Dawa - kuongeza vitamin {B Complex} na kusafisha kidonda
- Kujipatia kipato
MVINYO WA ROSELA {Roselle Alcoholie Beverage}
Viambaupishi kwa lita 10 za juisi ya rosella
- Mauwa ya rosella……………………..200kg
- Sukari…………………………………3kg
- Hamira……………………………….20gm
- Chai………………………………….1 cup {250ml}
Hamira mama
- Limao ……………………………………
- Chungwa…………………………………
- Hamira……………………………………
- Juisi ya rosella {1200ml katika nyuzi joto 300C
4. HATUA ZA UTENGENEZAJI
- Chambua mauwa ya rosella yaliyokauka kwa kuondoa uchafu na majani yaliyokauka kasha pima kujua uzito.
- Pima kiasi cha maji kinachotakiwa na weka kwenye sufuria na weka jikono ili yachemke.
- Weka mauwa ya rosella yaliyokwisha chambuliwa na kupimwa kwenye maji yaliyochemka na acha yachemke kwa muda wa dakika 5 huku ukikoroga vizuri ili kupata juisi.
- Ondoa jikoni na chuja ili kuondoa mauwa na kupata juisi ya rosella.
- Weka kiasi cha sukari kwenye juisi ya rosella kisha rudisha jikoni huku ukikoroga kuhakikisha sukari yote imeyeyuka
- Chuja na weka juisi kwenye chombo cha kuchachulia na iache ipoe hadi kufikia nyuzi joto 300C
- Weka hamira {hamira mama} kicha funika chombo cha kuchachulia vizuri na kuweka kifaa cha kutolea hewa ‘air lock’’
- Acha uchachukaji uendelee kwa siku ishirini na moja [21days|
N.B. Kwa siku saba koroga mara moja kila siku
9. Chuja na rudisha tena kwenye chombo cha kuchachulia kilichosafishwa na acha uchachuaji uendelee mpaka mwisho kwa kiasi kinachohitajika.
10. Chuja tena na mwisho fungasha kwenye chupa zilizosafishwa vizuri “sterilized bottle”
12. Weka mfuniko na kuweka lebo tayari kwa kuuza.
N.B. Ikumbukwe mvinyo uliokaa muda mrefu zaidi ndiyo unakuwa bora na ladha nzuri zaidi