Mohamedy cadinaly
JF-Expert Member
- Apr 24, 2012
- 2,449
- 2,245
Leteni mirejesho
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sikuiona mapema nilikua natengeneza wine ya ndizi na zabibu kwa ajili ya kunywa mimi mwenyewe na jamaa zangu. Tatizo na shindwa kumbuka vipimo ila kwa vile ninampango wa kutengeneza tena wiki moja au mbili zijazo ntaweka hapa kila kituWapendwa wana JF wenzangu,siku kadhaa zilizopita niliomba kupatiwa ufafanuzi wa namna ya kitengeneza wine ya ndizi,lakini kwa bahati mbaya sijafanikiwa kumaliza kiu yangu.Sasa leo naomba yeyote mwenye utaalamu wa kutengeneza wine ya ndizi na nanasi atupe somo hapa JF.TUSAIDIANE JAMAN!.
Mkuu tunasubiri mrejeshoSikuiona mapema nilikua natengeneza wine ya ndizi na zabibu kwa ajili ya kunywa mimi mwenyewe na jamaa zangu. Tatizo na shindwa kumbuka vipimo ila kwa vile ninampango wa kutengeneza tena wiki moja au mbili zijazo ntaweka hapa kila kitu
Nakumbuka mkuu ntaanza soon na ntaweka kila kitu hadharani
Asante sana MamndenyiUTENGENEZAJI WA MVINYO WA ROSELA
Mvinyo ni kinywaji kinachotengenezwa kutokana na juisi za matunda kama vile ndizi mbivu,machungwa,mapapai, mapera zabibu, malimao n.k, pia mvinyo unaweza kutengenezwa kwa kutumia juisi za matunda machanganyiko kama ndizi na karoti,zabibu na karoti na mchachungwa n.k
Mvinyo ni kinywaji kinachotengenezwa kutokana na juisi za matunda kama vile ndizi mbivu ,machunga ,mapapai,mapera ,zabibu,malimao n.k., pia mvinyo unaweza kutengenezwa kwa kutumia juisi za matunda mchanganyiko kama ndizi na karoti,zabibu na karoti na machungwa nk.
- MVINYO WA ROSELA
Ili kupata mvinyo ,kuna njia za kikemikali zinazoendelea wakati sukari na hamira vinapochanganyika vikasaidiwa na viambaupishi vingine vinavyotumika. viambaupishi vinavyotumika ni:
- VIFAA VITUMIKAVYO KATIKA KUZALISHA MVINYO
- Sufuria kubwa la kuchemshia juisi
- Chujio la plastiki au chuma cha pua
- Vyombo vya kuchachulia kama ndoo madumu nk.
- Mwiko wenye urefu wa kutosha
- Mirija ya kuchachulia
- Pima maji {hydrometer}
- Jagi la kuchukulia sampuli
- Chupa au kikombe cha kupimia majimaji chenye ujazo wa mililita 250 -500
- Kipimajoto
- Kipimatindikali
- Mizani 2,moja ya uzito wa gram 0- 250,nyingine kg 0-25
- Mrija wa kunyonyea wenye urefu wa mita 1.5
- Kitambaa cheupe cha pamba cha chujio {filter with filterpads}
- MAMBO YA KUZINGATIA
Matumizi ya mvinyo
- Osha vyombo sawasawa mara tu ukimaliza kuvitumia
- Tumia hamira inayofaa
- Wakati wote yeyusha sukari ndio utumie kutengenezea mvinyo
- Usizidishe sukari unapoanza kuchachua
- Chuja mvinyo katika vipindi na wakati muafaka ongeza campden tablets {saga na kuyeyusha katika maji kidogo} kila wakati unapochuja.
- Usifungashe mvinyo kwenye chupa mpaka uhakikishe umechachuka inavyotakiwa.
MVINYO WA ROSELA {Roselle Alcoholie Beverage}
- Kinywaji -kuongeza hamu ya kula na sacrament kanisani
- Dawa - kuongeza vitamin {B Complex} na kusafisha kidonda
- Kujipatia kipato
Viambaupishi kwa lita 10 za juisi ya rosella
Hamira mama
- Mauwa ya rosella……………………..200kg
- Sukari…………………………………3kg
- Hamira……………………………….20gm
- Chai………………………………….1 cup {250ml}
4. HATUA ZA UTENGENEZAJI
- Limao ……………………………………
- Chungwa…………………………………
- Hamira……………………………………
- Juisi ya rosella {1200ml katika nyuzi joto 300C
- Chambua mauwa ya rosella yaliyokauka kwa kuondoa uchafu na majani yaliyokauka kasha pima kujua uzito.
- Pima kiasi cha maji kinachotakiwa na weka kwenye sufuria na weka jikono ili yachemke.
- Weka mauwa ya rosella yaliyokwisha chambuliwa na kupimwa kwenye maji yaliyochemka na acha yachemke kwa muda wa dakika 5 huku ukikoroga vizuri ili kupata juisi.
- Ondoa jikoni na chuja ili kuondoa mauwa na kupata juisi ya rosella.
- Weka kiasi cha sukari kwenye juisi ya rosella kisha rudisha jikoni huku ukikoroga kuhakikisha sukari yote imeyeyuka
- Chuja na weka juisi kwenye chombo cha kuchachulia na iache ipoe hadi kufikia nyuzi joto 300C
- Weka hamira {hamira mama} kicha funika chombo cha kuchachulia vizuri na kuweka kifaa cha kutolea hewa ‘air lock’’
- Acha uchachukaji uendelee kwa siku ishirini na moja [21days|
N.B. Kwa siku saba koroga mara moja kila siku
9. Chuja na rudisha tena kwenye chombo cha kuchachulia kilichosafishwa na acha uchachuaji uendelee mpaka mwisho kwa kiasi kinachohitajika.
10. Chuja tena na mwisho fungasha kwenye chupa zilizosafishwa vizuri “sterilized bottle”
12. Weka mfuniko na kuweka lebo tayari kwa kuuza.
N.B. Ikumbukwe mvinyo uliokaa muda mrefu zaidi ndiyo unakuwa bora na ladha nzuri zaidi
Ile ya chenga ndiyo hutumika pia kwa kutengeneza wine. Ila unabidi kuwa mwangalifu maana inweza kuzalisha alcohol nyingi kuliko wine yeast. Somo ni refu kidogo. Nikjaliwa muda nitakuja kuelezea. Mimi nilisha tengeneza sana.Wakuu kuna utofauti wa hamira inayowekwa kwenye wine na ile ya maandazi?
Asante kwa jibu lako na karibu sana kuja kutupa elimu mkuu.Ile ya chenga ndiyo hutumika pia kwa kutengeneza wine. Ila unabidi kuwa mwangalifu maana inweza kuzalisha alcohol nyingi kuliko wine yeast. Somo ni refu kidogo. Nikjaliwa muda nitakuja kuelezea. Mimi nilisha tengeneza sana.
Leta maneno nasubiria nichukue notisiIle ya chenga ndiyo hutumika pia kwa kutengeneza wine. Ila unabidi kuwa mwangalifu maana inweza kuzalisha alcohol nyingi kuliko wine yeast. Somo ni refu kidogo. Nikjaliwa muda nitakuja kuelezea. Mimi nilisha tengeneza sana.